StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

August 31, 2012

CHECK IT OUT: T-MARC NA BIDHAA MPYA YENYE MUONEKANO WA KIPEKEE

Tweeted this Like this, be the first of your Friends






Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Mhe. Seif S Rashid (Mb) (wa pili kulia) akiongea wakati akizindua Kinga ya magonjwa ya zinaa na Ukimwi ya Dume, iliyoandaliwa na taasisi ya T-MARC, chini ya kauli mbiu ya “Mwanaume wa Kweli”.



Mama Alisa Cameron wa (USAID) akitoa hutuba yake kwa umma.





Mkurugenzi Mtendaji wa T-Marc Tanzania Bi. Diana Kisaka akiongea na washiriki wa uzinduzi huo.



Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Mhe. Seif S Rashid (Mb) (wa pili kulia) akifuatilia kwa makini hotuba ya mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania.



Sehemu maalum ya wageni waalikwa kuchukua zawadi baada ya uzinduzi huo.

Na Datus Boniface.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid amesema licha ya jitihada kubwa za serikali kupunguza maambukizi ya Ukimwi lakini bado maambukizi hayo yako juu.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kinga ya magonjwa ya zinaa na Ukimwi ya Dume, iliyoandaliwa na taasisi ya T-MARC, chini ya kauli mbiu ya “Mwanaume wa Kweli”.

Waziri amesema kuna haja ya kuongeza elimu kwa Wananchi juu ya matumizi sahihi ya kinga wakati wa kujamiana.

Hata hivyo amewapongeza T-MARC kwa kuweza kutengeza kinga ya kujamiana ya Dume ambayo inaweza kutumika kwa Wananchi wa rika tofauti.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa T-MARC Diana Kisaka amesema lengo la kuzindua kinga hiyo ni kuleta ushawishi kwa Wanaume na marafiki wao kutumia kinga.

Ameitaka serikali kuhakikisha kinga zinawafikia Wananchi wote hasa maeneo ya vijijini.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat