StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

Showing posts with label UCHUMI. Show all posts
Showing posts with label UCHUMI. Show all posts

October 23, 2012

HAYA NDIO MENO YA TEMBO KUTOKA TANZANIA YALIYOKAMATWA HONG KONG

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Hong Kong authorities confiscated $3.4 million ($26.7 million in Hong Kong currency) worth of ivory found in two shipping containers this week.

The illegal goods weighed more than 8,000 pounds, making it one of the biggest seizures of ivory in Hong Kong.

The containers arrived from Tanzania and Kenya, according to Hong Kong customs officials. The agency seized a total of 1,209 pieces of ivory tusks and three pounds of ivory ornaments from the two containers.

Hong Kong Customs was on alert after a tip-off from Guangdong officials in China. On October 16, Hong Kong officers inspected a container from Tanzania claiming to carry plastic scrap and found $1.7 million worth of ivory. A day later, a second container from Kenya was seized with ivory valued at $1.7 million, according to Hong Kong Customs.

Seven people, including one Hong Kong resident, have been arrested by Chinese authorities in connection to the cases, said a customs spokeswoman.

Hong Kong is viewed as a transit point for the illegal ivory trade, feeding into increasing demands in China, according to a Time article published this week.

Elephants are being killed in Africa at an alarming rate as international demand soars for ivory. Much of the demand comes from increasingly affluent Asian countries, particularly China and Thailand.

The last major bust in Hong Kong occurred in 2011, when officials seized a shipment of ivory and rhino horns valued at $2.2 million in Hong Kong dollars. Priest embroiled in ivory smuggling controversy. Will elephants still roam earth in 20 years? SOURCE: CNN-HONG KONG

October 4, 2012

ZIARA YA RAIS KIKWETE YAZAA MATUNDA APATA BILIONI 24.1 KWA AJILI YA AFYA.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Matajiri wawili wakubwa duniani juzi, Jumanne, Oktoba 2, 2012, wameichangia Tanzania kiasi cha sh. bilioni 24.1 (sawa na dola za Marekani milioni 15.5) kwa ajili ya kuendeleza afya ya akinamama na kusaidia uzazi salama hasa katika maeneo ya vijijini.

Matajiri hao, Mheshimiwa Michael Bloomberg ambaye ni Meya wa Jiji la New York, Marekani na Mama Helen Agerup wa Sweden, wametangaza mchango wao huo mkubwa kwa Tanzania kwenye mkutano maalum wa waandishi wa habari uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.

Pamoja na matajiri hao kwenye mkutano huo wa waandishi wa habari walikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Kati ya fedha hizo, Meya Bloomberg wa Jiji la New York lenye wakazi milioni 8.4, anatoa kiasi cha dola za Marekani milioni nane kupitia Taasisi yake ya Bloomberg Philanthropies wakati Mama Agerup anatoa kiasi cha dola milioni 7.5 kupitia taasisi yake na mumewe ya H&B Agerup Foundation.

Meja Bloomberg amekuwa anasaidia afya ya akinamama na juhudi za uzazi salama katika maeneo ya vijijini katika Tanzania tokea mwaka 2006 wakati hii itakuwa mara ya kwanza kwa Taasisi ya H&B kuungana na Bloomberg Philanthropies kusaidia sekta ya afya katika Tanzania.

Akizungumza kwenye shughuli hiyo muhimu, Meya Bloomberg amesema kuwa yeye na taasisi yake wameamua kuendelea kuunga mkono jithada za Tanzania katika kuinua afya ya akinamama na kupunguza vifo vya uzazi kwa sababu ya matokeo mazuri ambayo yamepatikana tokea Bloomberg Philanthropies ianze kuunga mkono jitihada hizo za Serikali mwaka 2006.

Amesema kuwa taasisi yake inajihusisha katika maeneo mawili makubwa. Eneo moja ni kujenga na kukarabati vituo vya afya na zahanati katika maeneo ya vijijini na pili ni kutoa mafunzo kwa watu wasiokuwa watalaam wa afya pamoja na wakunga kuweza kusaidia uzazi salama vijijini. Mpaka sasa taasisi hiyo imefundisha kiasi cha watu 106 kuweza kufanya kazi ya uzazi salama na ukunga chini ya msaada wake kwa Tanzania.

“Tunaona matokeo ya kuvutia sana. Hata kama idadi ya akinamama wanaopoteza maisha haijawa ya chini –akinamama 13 kati ya 1,000- kama ile ya Marekani lakini dhahiri kuwa idadi inapungua kwa kiasi cha kutia moyo”.

Ameongeza Meja Bloomberg: “Zaidi tunaifanya kazi hii katika Tanzania kwa sababu tunashughulika na Rais Kikwete, kiongozi mbunifu, kiongozi mkweli na muadilifu, kiongozi mchapakazi na anayetaka kuonyesha tofauti katika maisha ya wananchi wake.”

Naye Mama Helen Agerup amesema kuwa alitembelea Tanzania mwaka jana baada ya kushawishiwa na binti yake ambaye alikuwa ametembelea Tanzania mapema na kuvutiwa na jitihada za Serikali na zile za Taasisi ya Bloomberg kuhusu afya ya akinamama.

“Nilivutiwa sana na kazi inayofanywa na Serikali ya Tanzania na Taasisi ya Bloomberg kuzuia vifo vinavyosababishwa na mambo yanayoweza kuzuilika yaani kutokwa damu kupita kiasi na magonjwa ya kuambukiza kutokana hasa na tatizo la ukimwi,” amesema mama huyo.

Naye Rais Kikwete ameshukuru sana Meya Bloomberg na Mama Agerup akisema kuwa misaada yao inaleta tofauti kubwa katika afya za akinamama katika Tanzania.

“Katika nchi ambako uwiano wa daktari mmoja na wagonjwa ni daktari mmoja kwa wagonjwa 30,000 na mganga mmoja kwa wagonjwa 23,000 na ambako akinamama waja wazito wanatembea zaidi ya kilomita tano kwenye uchungu, misaada ya namna hii ni muhimu sana kwa nchi yetu. Tunawashukuru sana.”

Amesema kuwa umuhimu wa kuboresha afya ya akinamama ni moja ya maeneo ya kipaumbele cha Serikali na hali hiyo itaendelea mpaka tatizo la vifo vya uzazi litakapopungua sana.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

3 Oktoba, 2012

MAAFISA WA VYOMBO VYA ULINZI USALAMA WAFANYA OPARESHENI KUIKAGUA MELI MPYA YA AZAM SEALINK-1.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi -Zanzibar

 Maafisa wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini pamoja na Mamkala ya Bandari Zanzibar, wamefanya oparesheni maalum ya ukaguzi wa meli ya AZAM Sealink -1 iliyoingia nchini juzi kuangalia kama ina ubora na kukidhi vigezo vya usafirishaji wa abiria na mizigo majini yakiwemo magari.

Maafisa waliofanya ukaguzi huo ni kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Usalama wa taifa, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Mamlaka ya Usalama Bandarini na Huduma za Meli Zanzibar (ZMA) na Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA).

Pamoja na kuangalia ubora na vigezo vingine, Maafisa hao pia wamepata maelezo toshelezi juu ya ubora wa meli hiyo kutoka kwa Kampuni ya RFI iliyopewa dhamana ya kuisafirisha Meli hiyo kutoka nchini Ugiriki hadi hapa nchini.

Akizungumza na Ujumbe huo ndani ya Meli hiyo iliyoweka nanga nje kidogo ya Bandari ya Zanzibar, Mkurugenzi wa RFI Bw. Stefan Nedkoff, alisema kuwa meli hiyo imeweza kusafiri yenyewe kutoka nchini Ubeligiji hadi hapa nchini pasipo msaada wowote wa kiufundi.

Amesema kuwa katika maeneo waliyopitia walipambana na kila aina ya dharuba na kuvuka vikwazo vya mikondo mikubwa ya bahari kwenye kina kirefu na Meli hiyo iliweza kuhimili hali hiyo.

Alisema Meli hiyo inayoongozwa kwa mifumo ya kompyuta, ina uwezo mkubwa wa kuhimili misukosuko ya hali ya bahari na kusafiri umbali na kina kirefu cha maji baharini pasipo shaka.

Bw. Nedkoff amesema kuwa, mbali ya kuwa meli hiyo ilisafiri ikiwa tupu, lakini itahimili vishindo zaidi vya baharini pale itakapokuwa na abiria na mizigo ya kutosha.

Amesema kuwa mbali ya uwezo wake wa kubeba abiria 1,500, lakini pia meli hiyo inauwezo wa kuchukua mizigo yakiwemo magari 200 kutoka eneo moja kwenda jingine vyote vikiwa na uzito wa tani 500 bila ya kuwa na tatizo lolote la kiusalama.

Maafisa walioitembelea meli hiyo, wameonyeshwa njia maalum za kujiokolea pamoja na vifaa muhimu vya kiusalama vinavyoweza kutumika kwa uokozi wakati itokeapo ajali majini.

Meli hiyo pia ina vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa na abiria watakaojisikia kupumzika wakati wanapokuwa safarini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zanzibar mara baada ya kuwasili kwa Meli hiyo, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Coastal Ferry inayomiliki Boti ziendazo kasi za Kilimanjaro, Bw. Hussein Mohammed Saidi, alisema meli hiyo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Zanzibar na Pemba.

Amesema Kampuni yake ambayo ipo kihuduma zaidi, pia itaangalia uwezekano wa kuweka viwango vya nauli itakayomfanya kila mtu kusafiri yeye pamoja na jamaa ama watoto wake bila ya kujinyima.

Bw. Hussein alisema watoto wenye umri wa kuanzia saa moja hadi mika mitano watasafirishwa bure na wanafunzi watatozwa nusu ya nauli ya mtu mzima kwa kila safari.

IKULU: WENYE ARDHI BONDE LA KILOMBERO KUSAIDIWA KUZALISHA MPUNGA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Serikali ya Tanzania imefanikiwa kuainisha (identify) kiasi cha hekta 100,000 za ardhi ya wakulima wadogo ambao watasaidiwa kuongeza uzalishaji wa mpunga ili kuiwezesha Tanzania kuzalisha kiasi cha tani milioni moja za mpunga katika mwaka mmoja katika hatua ya kwanza ya kuleta mageuzi ya kilimo nchini.

Zoezi hilo ni sehemu ya mipango ya Serikali kuainisha kiasi cha hekta 200,000 za wakulima wadogo ili wasaidiwe kuongeza uzalishaji wa mpunga katika maeneo mbali mbali nchini, na hasa katika Bonde la Mto Kilombero, chini ya mipango mbali mbali ya kukuza kilimo kwa haraka, kuongeza uzalishaji wa mazao mbali mbali na kuwatoa wananchi katika umasikini.

Hayo yameelezwa jana, Jumanne, Oktoba 2, 2012, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhesimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kimataifa ya Maendeleo la Marekani (USAID), Bwana Rajiv Shah (pichani kulia), katika Hoteli ya JW Marriott, mjini New York, Marekani ambako Rais Kikwete amefikia katika ziara yake ya siku mbili.

Rais Kikwete na Bw. Shah wamejadili mipango mbali mbali inayosaidiwa na USAID, washirika wengine wa maendeleo na makampuni binafsi ya kimataifa katika jitihada za Tanzania kukuza kilimo na kupunguza umasikini ukiwamo ule wa SACGOT, Grow Africa na New Alliance for Agriculture.

Rais Kikwete amemweleza Shah kuwa mkulima mdogo na ardhi yake, hata ni ndogo kiasi gani, ni muhimu na ni sehemu maalum ya mipango ya Serikali katika kuendeleza kilimo kwa kumwinua mkulima huyo mdogo kutoka kwenye umasikini kwa kumsaidia kuboresha kilimo chake na uzalishaji wake.

“Kwa hakika, mkulima mdogo ni kiungo muhimu sana katika jitihada zetu. Lazima tutamsaidia kumtoa kwenye umasikini kwa kuongeza thamani kwenye ardhi yake, hata kama ni ndogo kiasi gani. Wakipewa pembejeo na misaada mingine wanaweza kuonyesha maajabu,” amesema Rais Kikwete.

Rais Kikwete pia amemweleza Bw. Shah kuhusu mipango ya Serikali ya kuanzisha Soko la Mazao ambalo litakuwa mkombozi kwa mkulima wa Tanzania na pia kuunda chombo maalum cha kushughulikia mageuzi katika kilimo cha Tanzania.

Bw. Shah amemwahidi Rais Kikwete kuwa Serikali ya Marekani kupitia USAID itakuwa tayari kusaidia jitihada hizo za Serikali katika kuunda vyombo hivyo viwili ili kumsaidia mkulima na kilimo cha Tanzania.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

3 Oktoba, 2012

WAZIRI WA FEDHA AZINDUAHUDUMA YA FARAJA BIMA KUPITIA M-PESA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Waziri wa fedha Dk. William Mgimwa akiongea wakati wa uzinduzi wa kutumia huduma ya Faraja Bima kupitia M-pesa kwa kushirikiana na Heritage Insurance,uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa huduma ya Faraja Bima itakayopatika kupitia M-pesa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Heritage Insurance Bw.Paul Lewis akisema machache wakati wa uzinduzi huo.

Ofisa Mkuu wa M-Biashara wa Vodacom Jacques Voogtz (Katikati) akimuonyesha Waziri wa fedha Dk. William Mgimwa namna ya kujiunga na kutumia huduma ya Faraja Bima kupitia M-pesa baada ya kuizindua jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza. Kupitia Faraja bima mteja anweza kulipia bima yake kwa M-pesa.

Waziri wa fedha Dk.William Mgimwa akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza na Mkurugenzi Mtendaji wa Heritage Insurance Bw.Paul Lewis.

Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa kushoto akimsikiliza jambo Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu, watatu toka kushoto wakati wa uzinduzi wa kutumia huduma ya Faraja Bima kupitia M-pesa,wapili kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania Bw.Salum Mwalim na kulia ni Angela Sompet.

TURKISH AIRLINES SET TO LAUNCH ISTANBUL – KILIMANJARO ROUTE ON 4TH DECEMBER

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Turkish Airlines set to launch Istanbul – Kilimanjaro route on 4th December

TURKISH Airlines is set to begin scheduled services to Kilimanjaro International Airport (KIA) from December 4 following an aggressive marketing strategy for the airport spearheaded by the Kilimanjaro Airport Development Company (KADCO). KADCO, the company that manages operations of the KIA has already secured $ 30 million from a Netherlands-based firm, Orion Grand Facility in a bid to transform KIA into a fully- fledged tourist's gateway by 2014.

According to the KADCO Acting Managing Director Bakari Murusuri, the agreement had been reached during the 18th World Route Development Forum, the largest global event held in Abu Dhabi (UAE) on Tuesday that sought to chat way forward on determining the future of air services.Murusuri said Turkish Airlines will operate five times a week with a B737-900 on the Istanbul Ataturk – Kilimanjaro – Mombasa route.

"This will be yet another milestone in our quest to be on a competitive edge. The landing of the airline will help connect Tanzania and other neighboring countries to markets in the US, Canada and Europe through Turkish Airlines network.

“We believe the airline’s entry will help open up provides more opportunities especially in the tourism sector since the region is home to unique tourist attractions,” he said. Turkish Airlines joins other global airlines that include Qatar Airways, KLM, Edelweiss air, Condor air and Ethiopian Airlines to fly to the northern located international airport.

October 3, 2012

BEI ZA PETROLI NA DIZEL ZASHUKA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei kikomo mpya, ambazo zitaanza kutumika leo nchini kote zikiwa zimeshuka kwa Sh. 306 kwa lita ya petroli, Sh. 192 kwa lita moja ya dizeli, huku mafuta ya taa bei zikibaki bila kubadilika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo, bei za mafuta ya petroli kwa Dar es Salaam zitakuwa Sh. 1,994 kwa lita moja ikiwa imeshuka kutoka Sh. 2, 300 ya bei ya Septemba, huku mafuta ya dizeli bei yake ikishuka hadi kufikia Sh. 1,950 kutoka Sh. 2,142, wakati mafuta ya taa yakibaki Sh. 1,993 kutokana na kutoingia meli yoyote ya mafuta hayo.

Taarifa hiyo ilisema bei hizo zitaendelea kuongezeka kutokana na gharama za usafirishaji kutoka Dar es Salaam kwenda mikoani, ingawa kwa jumla katika kila eneo punguzo litakuwa ni Sh. 306 na Sh. 192 kwa petroli na dizeli kwa lita moja.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, Kaguo alisema bei za bidhaa za mafuta ya petroli, zitaendelea kupangwa na soko na Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

“Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuzi wa bidhaa za mafuta kulingana na bei anayoiona mteja inamfaa,” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza:

“Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo. Na kama mfanyabiashara atakiuka atapewa adhabu ya kulipa Sh. milioni tatu.”

Taarifa hiyo ilivitaka vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana ili kumfanya mteja afanye uchaguzi wa kununua mafuta akiwa anajua bei halisi ya mafuta katika kituo husika.

October 2, 2012

HII NDIO MELI MPYA YA KISASA YA AZAM MARINE YENYE UWEZO WA KUBEBA ZAIDI YA WATU 1000 NA MAGARI 200 YAWASILI NCHINI.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Meli ya Azam Marine inayoitwa Azam SeaLink 1 ikiwasili katika bandari ya Visawani Zanzibar kwa mara kwanza.

Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakipiga picha Meli hiyo iliyowasili Visiwani Zanzibar leo.

Mzee Said Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo.

Sehemu ya Parking yenye uwezo wa kuingiza magari 200.

Muonekano wa ndani wa Lounge ya kumpzikia wasafiri.

Muonekano wa nje. (Picha na Omar Said wa Kampuni ya Bakheresa).

Na Father Kidevu Blog, Zanzibar
Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake.

Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu za mamlaka mbalimbali.

Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.

Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari.

Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.

Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara.

Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.

October 1, 2012

SEKTA YA RELI KUFUFUKA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Rais Jakaya Kikwete, akionesha njia za reli katika ramani ya Tanzania ujumbe toka kampuni ya Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC), uliomtembelea Ikulu, Dar es salaam jana, kumweleza nia yao ya kutaka kuwekeza katika sekta ya reli nchini. Picha na Ikulu

MAONYESHO YA ASALI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Maandalizi ya MAONYESHO YA ASALI YA DAR ES SALAAM (DAR ES SALAAM HONEY  EXHIBITION) ambayo yatafanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) Dar es Salaam tangu tarehe  3 hadi 7 Oktoba 2012 yamekamilika. Wananchi wanakaribishwa kuhudhuria maonyesho hayo ambayo hayatakuwa na kiingilio. Katika maonyesho hayo watu wataelimika kuhusu manufaa yatokanayo na asali, pia watapata utaalam wa kufuga nyuki na wataonja na kununua asali bora kwa bei nafuu.
Kaulimbiu ya maonyesho hayo ambayo ni ya kitaifa ni ASALI KWA AFYA NA USTAWI (HONEY FOR HEALTH AND PROSPERITY). Maonyesho hayo yameandaliwa  kwa ushirikiano wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  na wadau wengine wa Sekta ya Ufugaji Nyuki. Lengo kuu la maonesho ni kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao ya nyuki.
Tarehe 3 Oktoba ni siku iliyotengwa maalum kwa ajili ya kufanyika Kongamano la Ufugaji Nyuki. Hivyo wafugaji nyuki, wataalam na wadau mbalimbali wa Sekta hiyo wanakaribishwa kuhudhuria kungamano hilo ambalo litafanyika katika ukumbi wa J. M. Kikwete ulioko kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere .
Ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo utafanyika tarehe 5 Oktoba 2012  ambapo Mgeni Rasmi anategemewa kuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb).
Waonyeshaji waliothibitisha kushiriki ni Halmashauri za Wilaya zote, kampuni zinazonunua asali, watengenezaji wa mizinga na vifaa vingine vya kisasa  vya ufugaji nyuki, na watengenezaji wa bidhaa zinaotumia asali na nta kama malighafi.
Inategemewa kuwa katika maonyesho hayo waonyeshaji watajitangaza ili waweze kupata wanunuzi wa asali na mazao mengine ya nyuki. Pia wanunuzi wa mazao ya nyuki watapata fursa ya kuwafahamu wafugaji. Aidha inategemewa kuwa utaundwa mtandao ambao utawaunganisha wazalishaji, wafanyabiashara, wataalam na wadau wa sekta ya nyuki.
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
30 Septemba 2012
                                                   Simu: +255 784 468047

September 24, 2012

UN ANNOUNCES COMMITMENT TO SUPPORT ANTI CORRUPTION EFFORTS TO TANZANIA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Director General of Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) Dr. Edward Hosea speaking at the stakeholders meeting to validate the Evaluation Report of national Anti-Corruption Strategy and Action Plan (NASCAP) II where he said this process is a solid commitment from the Government, The Private Sector, Civil Society and Development Partners to collectively share the responsibility of tackling the challenges of corruption at its root cause.

The Controller and Auditor General (CAG), Mr Ludovick Utouh (left) with other Stake Holders during the meeting.

Director General of Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) Dr. Edward Hosea speaking at the stakeholders meeting to validate the Evaluation Report of national Anti-Corruption Strategy and Action Plan (NASCAP) II where he said this process is a solid commitment from the Government, The Private Sector, Civil Society and Development Partners to collectively share the responsibility of tackling the challenges of corruption at its root cause.

HII NDIO ADHA WANAYOIPATA WASAFIR WAKATI HUU WA UJENZI WA BARABARA YA IRINGA-MAFINGA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Magari yakiwa katika foleni katika kipande cha barabara ambacho kampuni ya Ujenzi ya AARSLEFF-INTERBETON JV inaendelea kukujengwa kwa kiwango cha lami. Ujenzi huo wa barabara ni kutoka Iringa hadi Mafinga. Kampuni hiyo pia ilijenga kipande cha barabara kutoka Iyovi hadi Iringa na kile kipande kidogo cha kuingia Iringa mjini “access road”.


Madereva wamekuwa wakilala mika kusimama kwa muda mrefu katika maeneo hayo na kuchelewa safari.

Barabara ikiwa imefunguliwa na magari ya upande mmoja kuruhusiwa kupita.
Wakiendelea kusubiri wenzao wapite

Mafundi wa kampuni ya Ujenzi ya AARSLEFF-INTERBETON JV wakiendelea na ujenzi

September 18, 2012

NOTI MPYA ZATUMIKA KUTENGENEZEA POMBE NA KUVUTIA SIGARA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends  
BAADA ya kuzuka mtindo wa kuzikataa Sarafu za Shilingi 10 na Shilingi 20 kutotumika huku Benki kuu ikikaa kimywa, baadhi ya wananchi wameanza kuziharibu kwa makusudi noti za shilingi 500 na 2000 kwa kuondoa mstari(ufito) unaong'aa na unaohalalisha pesa hizo na kisha kuutumia katika pombe za kienyeji au bia ili kuongeza kileo wakidai kuwa husaidia kuokoa pesa kwani hulewa kwa muda mfupi.


Wananchi hao pia wanachomoa ufito huo na kuchanganya na sigara au tumbaku ambapo hudai hulewa haraka.

Hali hiyo ambayo imeambatana na uadimikaji wa noti hizo, imeshika kasi maeneo mengi nchini likiwemo eneo la Kijiji cha Maleza,Kata ya Kipeta,Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.


Athari hiyo pia imevikumba vijiji vya Kilangawana na Kamsamba hali ambayo imefanya kuwepo kwa ugumu wa upatikanaji wa fedha hizo.


Hata hivyo wananchi kadhaa ambao hawakupenda majina yao kutajwa,wamethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kuitaka Serikali na Benki Kuu kuchukua hatua za haraka ili kukomesha vitendo hivyo.


Katika hali ya kuhalalisha noti hizo zilizoharibiwa wahalifu hao hutumia gundi kwa kutumia uzi wa mifuko ya mbolea ili ziendelee kutumika.

HII NDI HOTELI ILIYOCHUKUA TUZO NAMBARI MOJA KWA UBORA ILIYOPO SERENGETI TANZANIA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Hoteli ya Singita Grumeti Reserves.

Watu maarufu waliofika katika hotel hii ni bill gates, bill clinton, Jay z, angelina jolie, na wengineo wengi...
HOTELI ya Singita Grumeti Reserves, iliyopo Serengeti, Mara, Tanzania, inathibitisha kufuru ya utajiri uliopo Tanzania.
Singita ndiyo hoteli nambari moja duniani, ikichukua tuzo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na taasisi maarufu ya Marekani, US Travel + Leisure ambayo ‘hudili’ na viwango vya biashara ya utalii duniani.
Hoteli hiyo, inathibitisha kwamba thamani ya Tanzania ipo juu mno, ndiyo maana mwekezaji kutoka Afrika Kusini, Luke Bailes, aliamua kufanya uwekezaji wa hali ya juu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Matokeo hayo, yaliandikwa Agosti mwaka huu kwenye jarida maarufu kwa kuchapisha matukio ya biashara za utalii, linaloitwa T+L Magazine. Jarida hilo linamilikiwa na Taasisi ya US Travel + Leisure.
Tangu kufunguliwa kwake, Singita Grumeti imekuwa kivutio cha viongozi, matajiri na watu maarufu ambao mara kwa mara hutinga kujivinjari, vilevile kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Kwa mujibu wa US Travel + Leisure, sababu ya kuipa Singita hadhi ya kuwa hoteli namba moja duniani, inatokana na muundo wake, huduma zinazotolewa, kuwa ndani ya mbuga kubwa kabisa ya wanyama duniani (Serengeti), vilevile wageni mashuhuri inaopokea.
Inaelezwa kwamba Singita Grumeti ndiyo hoteli inayoongoza kwa sasa duniani kwa kupokea wageni wenye hadhi ya daraja la kwanza, wakiwemo marais, matajiri, wanamichezo, wasanii, viongozi mbalimbali maarufu ulimwenguni na kadhalika.

HAWA WANATAJWA KUJIVINJARI SINGITA
Marais wa 42 na 43 nchini Marekani, Bill Clinton na George W. Bush, kwa nyakati tofauti wamefikia kwenye hoteli hiyo baada ya kuvutiwa na sifa zake zinazotikisa duniani.
Bilionea wa Kirusi anayemiliki Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich, alipotembelea nchini Septemba 2009, inaelezwa kwamba alilala kwenye hoteli hiyo.
Bilionea wa Kihindi, Mukesh Ambani ambaye kwa sasa ni tajiri namba 19 duniani, alifika nchini mwaka jana na kufikia kwenye hoteli hiyo.
Wakati alipowasili nchini, Mekesh alikuwa tajiri namba nne duniani. Ripoti ya mwaka 2011, ilimtaja kuwa tajiri namba tisa na sasa anashika nafasi ya 19.
Mke wa zamani wa mwanasoka anayechezea Chelsea ya England, Ashley Cole, Cheryl, alipofika nchini miaka miwili iliyopita, inaelezwa pia kwamba alifikia kwenye hoteli hiyo.
Mwanamitindo aliye pia mcheza sinema maarufu wa Hollywood, Marekani, Angelina Jolie na mumewe Brad Pitt, waliripotiwa kufika nchini na moja kwa moja makazi yao yakawa Singita Grumeti.
Wengine ambao wanatajwa kuwahi kupumzika kwenye hoteli hiyo ni mwanamuziki wa Marekani, Sean Carter ‘Jay Z’, mwanasoka Thierry Henry, Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa orodha ya wageni wanaofikia Singita ni kubwa mno, tatizo hufanywa siri kwa sababu watu wengi mashuhuri ulimwenguni huwa hawapendi ijulikane kama wamefikia kwenye hoteli hiyo kwa sababu za kiusalama.

SIFA ZA HOTELI HIYO
Ni hoteli yenye eneo kubwa, kutoka ‘loji’ moja hadi nyingine, inabidi utumie usafiri maalum.
Imegawanywa kwenye ‘loji’ mbili, moja inaitwa Ebony na nyingine ni Boulder.
Hoteli hiyo, pia inaundwa na ‘loji’ nyingine inayoitwa Castleton Camp ambayo inaweza kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Bei ya chini kabisa kwa mtu kulala kwenye hoteli hiyo ni shilingi 2,000,000 na bei hiyo hutegemea na msimu.
Bei zimetofautiana kati ya ‘loji’ moja hadi nyingine na mtu kulala kwenye Castleton Camp, inaweza kugharimu mpaka shilingi milioni 23 kwa siku moja.
Singita Grumeti ni moja kati ya hoteli za Singita za nchini Afrika Kusini.

September 14, 2012

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI YAFANYA MKUTANO WA UANZISHWAJI WA ENEO HURU LA MAGONJWA YA MIFUGO KATIKA MKOA WA RUKWA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Picha ya pamoja kati ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang'a na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Winston Mleche pamoja na wataalamu wa Mifugo kutoka Mikoa ya Rukwa, Njombe, Katavi, Tabora, Mbeya, Singida, Shinyanga, Mwanza, Kigoma, Iringa, Kagera, Mara, Simiyu na Geita katika kikao kilichowashirikisha wataalamu hao katika kujadili mpango wa kuanzishwa eneo huru la magonjwa ya mifugo katika Wilaya za Sumbawanga na Nkasi Mkoani Rukwa kwa lengo la kuwezesha kufanyika kwa biashara ya mifugo na mazao ya mifugo kwa kufuata vigezo na masharti ya kimataifa.


Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambae pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla akiwakaribisha wageni hao Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufanya mkutano huo muhimu kwa maendeleo ya sekta ya mifugo mkoani Rukwa na Taifani kwa ujumla.


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Moshi Chang'a ambae pia ni Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kalambo akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya ambaye yupo safarini kikazi. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Winston Mleche ambae pia ni Mkurugenzi wa huduma za mifugo nchini. Katika hotuba yake hiyo alielezea changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi ikiwemo uimarishaji wa mifumo ya usafirishaji, uchukuzi na mawasiliano, kuboresha miundombinu ya masoko ya mifugo, kuendelea kuboresha aina ya mifugo na mifumo ya uzalishaji mifugo, kuboresha taratibu za umiliki wa ardhi na kuzuia magonjwa mbalimbali ya mifugo. Hata hivo Mkoa wa Rukwa umepiga hatua kubwa katika kupambana na magonjwa hatarishi ya mifugo ambayo kwa sasa yapo kwa kiwango kidogo sana.


Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa kitengo cha Uchumi na Uzalishaji Ndugu Respitch Maengo na Katibu Tawala Msaidizi kitengo hicho kutoka Mkoa jirani wa Katavi Ndugu Sesemkwa.


Daktari wa Mifugo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Loomu akiwasilisha mada ya fursa za mifugo zinazopatikana Mkoani Rukwa. Zipo fursa nyingi Mkoani Rukwa ikiwemo mifugo mingi na ya aina tofauti yenye afya pamoja na wafugaji mahiri wadogo na wakubwa. ,Maeneo ya malisho, uwepo wa kiwanda cha kisasa cha nyama cha Saafi kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndaji ni fursa nyingine.


Baadhi ya wadau wa Mkutano huo wakifuatilia mada tofauti ndani ya Ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kikao hicho kitadumu kwa muda wa siku mbili ambapo maazimio mbalimbali yantegemewa kufikiwa kwa ajili ya kufanikisha adhma hiyo ya kuufanya Mkoa wa Rukwa eneo huru la magonjwa ya mifugo kuimarisha bishara ya mazao ya mifugo kimataifa. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

JAPANI YASAIDIA UJENZI WA MABWENI 4 WILAYA ZA NACHINGWEA NA RUANGWA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea,Arbogast Kiwale kwa pamoja na Balozi wa Japan
Nchini Tanzania ,Masaki Okada wakitia saini mkataba wa kusaidia Ujenzi wa Mabweni mawili ya shule ya sekondari ya kutwa ya wasichana Nachingwea wenye thamani ya dola za marekani 122,333...Mkataba huo
umesainiwa mbele ya Wabunge wa mkoa wa Lindi,Wakuu wa wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri huku Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Katibu Tawala mkoa akishuhudia

Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkowe wilayani Ruangwa mwl Shannel Nchimbi akikabidhi hati ya makubaliano ya msaada wa mabweni 2 kwa shule hiyo kwa Balozi wa Japan,Masaki Okada hii katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi

Wabunge wa Mkoa wa Lindi nao wakishuhudia kuwekwa kwa saini mikataba ya Kusaidia ujenzi wa Mabweni 2 ya shule ya sekondari ya Nkowe wilayani Ruangwa Pamoja na Mabweni mawili ya Shule ya kutwa ya wasichana Nachingwea

Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Lindi wakishuhudia tukio hilo la msaada wa kuinua kiwango cha elimu

Picha ya pamoja baada ya kusainiwa mikataba hiyo. Serikali ya Japan imetoa Jumla ya dola za kimarekani 243,698 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni 4 kwa shule za sekondari za Nkowe wilayani Ruangwa Na Shule ya kutwa ya Wasichana wilayani Nachingwea Hatua hiyo imekuja katika jitihada za Nchi ya Japan kukuza Ushirikiano na Tanzania Balozi wa Japan Nchini Masaki Okada amelala wilayani Ruangwa Mkoani Lindi ambapo leo atatembelea shule ya sekondari NKOWE na Baadae kuelekea Wilayani Nachingwea. Picha na Habari toka kwa Mdau Abdulaziz video rec,Ruangwa

September 12, 2012

MH. MIZENGO PINDA AKIZINDUA MRADI WA NYUKI GEITA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa ufugaji nyuki wa Bugulula wilayani Geita akiwa katika ziara ya mkoa wa Geita Septemba 10, 2012.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mradi wa ufugji nyuki wa kijiji cha Bugulula baada ya kuufungua Septemba 10, 2012. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Geita, Magalula Maglula.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na wanawake wa kijiji cha Bugulula baada ya kufngua mradi wa ufugaji nyuki akiwa katika ziara ya mkoa wa Geita, Septemba 10, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

September 11, 2012

HUYU NDIYE MCHINA ALIYETIWA MBARONI KWA KUCHIMBA MADINI KWENYE PORI LA AKIBA LA LWAFI WILAYANI NKASI.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mtambo wa kuchimbia madini ambao Raia wa China walikamatwa wakiutumia katika pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkansi kinyume cha sheria.Raia huyu wa china amehukumiwa kulipa faini na kuamriwa kuondoa mtambo huo katika pori hilo.

Baadhi ya raia wa China na Watanzania wakishirikiana kuchimba madini katika pori la Akiba la Lwafi,wilayani Nkansi kinyume cha sheria,ambapo raia hao wa china walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kulipa faini.Picha naTabu Ndziku


Mkurugenzi wa Kampuni ya REDore Mining mwenye asili ya Asia Chaoxian Zhou amehukumiwa kwenda jela miaka minne au kulipa faini jumla ya Shilingi 1,350,000/= kwa kukutwa na makosa mbalimbali likiwemo lakuchimba madini ndani ya hifadhi ya Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi kinyume cha sheria .

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama pori Paul Sarakikya, mtuhumiwa amelipa faini na kuachiwa huru.Makosa megine aliyopatikana nayo ni pamoja na kuingia ndani ya Pori la Akiba Lwafi kinyume na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009 kifungu cha 15 na kuharibu mimea ndani ya Pori la Akiba kwa kukiuka kifungu cha 18 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori.

Makosa mengine ni pamoja na kuchimba madini ndani ya Pori la Akiba bila kibali kinyume na Kifungu cha 20 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori na kuchimba madini ndani ya hifadhi kinyume na kifungu cha 95(1) (c) cha Sheria ya madini Na. 14 ya mwaka 2010.

Mshtakiwa alikiri makosa yote mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Richard Kasele na Mwendesha Mashtaka Bwana Prosper Rwegerera na kupatikana na hatia ya kuchimba madini katika eneo la Kanyamakaa lililoko katika Wilaya ya Nkasi kinyume cha sheria ya Kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mshitakiwa ameamriwa kuondoa mitambo iliyokutwa ndani ya Pori la Akiba la Lwafi na kufukia mashimo na mitaro yote iliyochimbwa kutokana na shughuli za Kampuni hiyo ndani ya siku saba. Aidha Madini yaliyokuwa yamechimbwa katika eneo hilo ambayo thamani yake bado haijajulikana yametaifishwa na Serikali.

Chaoxian Zhou na mwenzake Wei Lyu ambao wote ni raia wa China walikamtwa Julai 25, 2012 ambapo iligundulika kuwa Wei Lyu hakuwahi kwenda mkoani Katavi wala katika Hifadhi hiyo ya Lwafi na kuchimba madini hivyo aliachiwa huru.

TRENI YA KWANZA YA DAR-UBUNGO YAFANYIWA MAJARIBIO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Kichwa cha treni pamoja na mabehewa sita ya awamu ya kwanza,yakisubiri kufanyiwa majaribio kwa Safari zitazoanzia Station ya Dar es Salaam Mpaka Ubungo mnamo mwezi wa kumi. Majaribia hayo yameongozwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Dk Charles Tizeba(Mb) ambaye alipanda treni hiyo kuanzia Station Dar es Salaam Mpaka Ubungo.Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bil 4.75 kwa ajili ya ukarabati wa njia,injini na mabehewa.

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(Mb),akipanda treni wakati wa majaribio ya Mabehewa sita ya treni kati ya mabehewa kumi na mbili yanatogemewa kutumika na Shirika la reli Tanzania(TRL). Treni hizo zitakayofanya safari zake kutoka Station Dar es Salaam mpaka Ubungo,mapema mwezi wa Kumi.

Baadhi ya wananchi wakipanda katika behewa moja kati ya Sita yaliyofanyiwa majaribio mapema leo kutokea Station mpaka Ubungo(km 12).

Mchuma huo unaondoka

Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania(TRL) wakiwa na furaha ndani ya mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio leo abubuhi.

Abiria wa majaribio
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat