StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts

November 16, 2012

KUTOKA KWA WANAFUNZI WA TANZANIA NCHINI URUSI: WAKOSA CHAKULA NA MALAZI HALI YAO MBAYA, PATA HABARI KAMILI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Sisi wanafunzi wa kitanzania nchini Urusi ,tunakosa huduma za msingi kama vile malazi , chakula na bima ya afya. Serikali kupitia bodi ya mikopo ya elimu ya juu na Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ,kwania njema iliamua kusomesha wanafunzi wa kitanzania katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Urusi.

Lakini kutokana na utendaji mbovu na ubinafsi wa baadhi ya watendaji wa Bodi ya mikopo, kumekua na ucheleweshwaji wa ulipaji wa pesa za kujikimu , malazi na bima ya afya kwa zaidi ya miezi mitatu sasa bila sababu za msingi toka kuanza kwa mwaka wa masomo 2012/13.

Hali hii imetupelekea wanafunzi kuanza kufukuzwa katika hosteli tunazoishi pamoja na kutopatiwa huduma za afya pindi tunapo ugua.Ikumbukwe kuwa katika nchi za ulaya huwezi pata matibabu kama huna bima ya afya.

Shukrani zetu za dhati ziende kwa Ubalozi wa Tanzania nchi Urusi kwa kushirikiana bega kwa bega na Wanafunzi katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili linalotukabili katika kipindi hiki kigumu pamoja na majuku mengi waliyonayo, pamoja na jitihada hizo mpaka sasa hakuna ufumbuzi wowote uliopatikana.
Tunaandika waraka huu kwa huzuni na masikitiko makubwa sana kwa sababu kutopatiwa mikopo mpaka sasa sio tu kunafanya wanafunzi waishi maisha magumu na hatari, vilevile kunatia aibu Taifa kwa kutolipa ada kwa wakati.

Tunaamini kabisa Serikali kupitia bodi ya mikopo ,wizara ya elimu na mafunzo stadi na ufundi na ubalozi wa Tanzania Nchini Urusi una nia njema kabisa kusomesha vijana wake nje ya nchi, ispokua tu kuna baadhi
ya watendaji wa bodi ya mikopo wamekua wazembe na kutowajibika kwani wamekua wakitoa majibu ya uongo na jeuri kwa uongozi wa wanafunzi na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Urusi.

Ombi letu kwenu ni kutufikishia ujumbe huu kwa wahusika na watendaji wa ngazi za juu za bodi ili waweze kutusaidia sisi wanafunzi wa Urusi ambao tupo hatarini huku ugenini.

Tunatumaini kutokana na Uzito wa tatizo letu wahusika watalishughurikia na kulitatua tatizo hili kwa haraka zaidi na kutupa ufafanuzi wa ucheleweshwaji wa mikopo ya wanafunzi kwa zaidi ya miezi mitatu(3).

November 2, 2012

BREAKING NEWS: WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI WAGONGWA NA ROLI NA KUFARIKI PAPO HAPO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Miili ya wanafunzi wa shule ya msingi imezu ikichukuliwa na wanausalama watoto hao walikuwa wakivuka barabara akielekea shuleni ndipo roli hilo lilipowagonga na kukimbia huku miili ya watoto hao ikiwa imetawanyika vipandevipande ajali hiyo imetokea mida ya saa moja na nusu asubuhi

Watoto hao wamegongwa katika barabara kuu itokayo Zambia kwenda dsm maeneo ya imezu inyara wilaya ya mbeya vijijini
 



October 31, 2012

HILI NDILO TUKIO ZIMA LA WANAFUNZI WA SEKONDARI WALIONDAMANA JANA WAKAPIGWA MABOMU NA KUOKOTA MOJA LIKIWA HALIJALIPUKA MJINI ARUSHA JANA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
KAMANDA wa Oparesheni Maalum, Peter Mvulla, akiwa amemnyang'anya bomu
hilo, mwanafunzi huyo, baada ya kuonyesha, huku akisikika akisema
halijalipuka na ni hatari kuendelea kulishika, sababu lilianguka kwa
bahati mbaya


MMOJA wa wanafunzi hao ambaye hakujulikana jina lake mara moja, akiwa
anaonyesha wenzake bomu linalodaiwa kutolipuka, mbele ya Mkuu wa Mkoa
Arusha,ambalo alidhani ni ganda limeangkuka baada ya kulipuka.


WANAFUNZI wakiwa mbele ya jengo la Mkuu wa Mkoa Arusha, Magesa
mulongo, wakimsubiri kumpa malalamiko yao.

WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Kimnyaki, Wilayani Arumeru, wameandamana wakiwa na mabango mbalimbali hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha na kusababisha vurugu kubwa kutokea barabara ya Ngaramtoni, nje kidogo ya Jiji la Arusha, hali iliyolazimisha jeshi la Polisi kutumia nguvu kwa kuwatawanya kwa kuwapiga mabomu ya machozi.

Aidha katika vurugu hizo, mmoja wa wanafunzi aliokota bomu lililokuwa halijalipuka, akidhani kuwa ni ganda la bomu lililotumika, huku akimwonyesha mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo, hali iliyosababisha Kamanda wa Oparesheni Maalum, Peter Mvulla kumnyang’anya haraka, kabla ya kuleta madhara.

Maandamano hayo yalikuwa ya kushikiza kufukuzwa kwa Mwalimu Mkuu wa shule Marium Chamle kwa sababu ya kuchelewesha wanafunzi wa kidato cha nne kutoingia chumba cha mitihani.

Blog hii ilishuhudia wanafunzi hao katika hali isiyo ya kawaida kila mmoja alikuwa na chupa ya maji, ambayo walikuwa wakinawa wakati wa mabomu hayo na kusonga mbele hadi ofisi hizo. Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa mulongo,kwa niaba ya wenzake, Mesharck Lomnyaki alisema mwalimu mkuu huyo amesababisha baadhi wa wanafunzi wa kidato cha nne kuchelewa kufanya mitihani yao ya baraza la mitihani (NECTA), kwa kuzuia kuingia katika chumba cha mitihani toka saa mbili asubuhi na kuwaruhusu kuingia saa 4.30.

Aidha alisema Oktoba 16 mwaka huu, walinyimwa mwongozo wa kujibu swali la tano, lenye alama kumi, kwenye somo la Chemia , ambao hawakupata kulingana na muda na kusababisha usumbufu ndani ya chumba cha mtihani na kusababisha kukata tamaa kwenye somo la Fizikia. Pia alidai tatizo la kufanana na hilo limejitokeza kwa wanafunzi wa kidato cha pili, kwenye mtihani wa Moko, ambapo aliwafukuza wanafunzi hao kutomaliza mtihani huo, kwa sababu ya kutolipa michango na kusababisha wanafunzi 46 kutofanya kabisa mtihani huo. Alisema matokeo ya kuzuia wanafunzi hao yalisababisha kushuka kwa
kiwango cha ufaulu, hali iliyosababisha mwalimu huyo kutoa lugha za kashfa na kujenga woga kwa wanafunzi  hao wanaotarajia kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili, utakaofanyika mwaka huu.
“Lakini tunasikitika badala ya kutusikiliza kero zetu, Polisi wanatupiga mabomu barabarani ili tusiandamane na baadhi yetu tumeokota ganda hili hapa la bomu,”alisema Mara baada ya kuonyesha ganda hilo, ndipo Kamanda wa Oparesheni Maalum, Peter Mvulla, aliposhituka na kumnyang’anya bomu mtoto aliyeshika, akidai hilo lilikuwa ni bomu halikulipuka na lilikuwa na hatari ya kulipuka endapo lingeshikwa shikwa kwenye chuma maalum cha kushitua.
Alisema bomu hilo lilianguka kwa bahati mbaya, katika vurugu za kuwatuliza kuandamana, ambapo wanafunzi hao waliwapiga mawe Polisi hao na kulazimisha kutumia nguvu ndogo tu ya kujaribu kuwatuliza, lakini hawakusikia, waliandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Naye mwanafunzi mwingine Ezekiel Memiri, alitaja kero zingine kuwa ni unyanyasaji wa wanafunzi, ambapo wengi hufukuzwa kwa makosa madogo
madogo, bila udhibitisho wa bodi ya shule. “Hili limesababisha wanafunzi aidi ya 20 kufukuzwa shule na baadhi kusimamishwa na baadhi ya waalimu kuwatumikisha wanafunzi majumbani mwao kwa kuwafulia nguo hadi za waume zao,”alisema.
Alisema kutokana na hilo wameomba Mkuu wa Mkoa kuingilia kati na kumbadilisha Mkuu wa shule hiyo kwa sababu matokeo yao yanazidi kushuka kitaaluma. Naye Mkuu wa Mkoa Arusha, Magesa Mulongo, aliwasikilia wanafunzi hao, huku akigeuka kuwa mbogo na kuamuru Polisi kukamata wanafunzi wao wawili waliokuwa wanatoa maelezo kwa niaba ya wenzao ambao ni Mesharck Lomnyaki na Daudi aliyeptikana jina moja, kwa madai wao ndio viongozi wa maandamano hayo .
Alisema kuwa kwa sasa anashangaa kumezuka tabia ya wanafunzi shuleni Mkoani Arusha kuandamana hata kwa makosa yasio na sababu hadi ofisini kwake jambo ambalo amelikemea na kutoa onyo kwa shule zote Mkoani hapo kuacha tabia hiyo vinginevyo atazifungia. “Shule zitakazoandamana kuanzia leo nitazifungia ili mkose kabisha masomo, maana hamtaki kusoma na leo ningefanya hivi, lakini nimeonea huruma watoto wa kike walio wengi ambao tunapigania wapate elimu, ila hawa viongozi wenu wapelekwe ndani iwe fundisho la tabia hii,”alisema. Mulongo alitoa hadi kufika saa tisa jioni ya jana, wanafunzi hao wawe wamerejea shuleni kwao, kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na Afisa Elimu, vinginevyo atawafungia shule yao.

“Nashangaa kupigwa mabomu, mnashangaa nini wakati mmeandamana bila kibali, mlitegemea nini mnavunja sheria na mkivunja sheria kwa kudai haki, hata haki mnayotaka hamtapata,sababu ya kuvunja sheria”alisema.

Hata hivyo ilichukua muda wanafunzi hao kutawanyika kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa, wakishinikiza kuachiwa kwa wenzao wawili waliokamatwa na Polisi, hadi pale Polisi walipoamua kutoweka kwa gari namba PT. 1834 na kuwaacha kwenye mataa wanafunzi hao wakibaki hawana cha kufanya,zaidi ya kuondoka hadi makao Makuu ya Polisi kusubiri wenzao kuachiwa.

October 24, 2012

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VYA AFYA NGAZI YA CHETI, DIPLOMA NA ADVANCED DIPLOMA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Ministry of Health and Social Welfare
Majina ya Wanafunzi Wapya na Vituo Walivyopangiwamwaka 2012/13


October 5, 2012

WALIMU WATANGAZA KUTOADHIMISHA "SIKU YA WALIMU DUNIANI"

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba

Wakati ulimwengu ukiadhimisha ‘Siku ya Walimu Duniani’ leo, walimu wa Tanzania hawatakuwa na maadhimisho yoyote kutokana na madai yao kutotimizwa pamoja na ahadi, ambazo wamekuwa wakiahidiwa na serikali kila mwaka kwa miaka sita sasa.

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, alisema tofauti na miaka mingine wataadhimisha siku yao wakiwa kazini na wakiwa wamekata tamaa kutokana na mwajiri wao, ambaye ni serikali kushindwa kuwatimizia madai yao ya msingi.

Alisema madai yao kwa serikali, ambayo hayajatimizwa hadi sasa, ni kuboreshewa mazingira ya kazi, nyongeza ya mishahara inayokidhi hali halisi kwenye utumishi wa umma pamoja na kuongezwa posho ya kufundishia.

Aliitaka serikali kukubali ushauri wa Bunge na uamuzi wa Mahakama ya Kazi uliozitaka pande mbili kukaa kwenye meza ya majadiliano ili kuendeleza mazungumzo ya namna ya kutatua mgogoro uliopo unaohusu madai ya walimu nchini.

September 26, 2012

NAIBU WAZIRI AMFUKUZA MWALIMU WA SEKONDARI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Naibu waziri wa elimu na ufundi ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI akiwa anaongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilboru

Naibu Waziri wa elimu na ufundi Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi mwalimu wa shule ya Sekondari ya vipaji Maalumu ya Ilboru Mkoani Arusha mara baada ya kukutwa akiwa amelewa wakati wa kazi shuleni hapo

Hatua hiyo imekuja mara baada ya waziri huo kufanya ziara ya kawaida shuleni hapo kutafuta ufumbuzi wa tatizo la wanafunzi kupelekea kuandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kugoma kuingia darasani hivi karibuni

Majaliwa alilazimika kufanya hivyo wakati akiongea na walimu wa shule hiyo juu ya nini chanzo cha mgogoro huo,ambapo mwalimu huyo,Potin Jovita Sumawe, alinyanyuka na kuanza kuongea kama mtu aliyechanganyikiwa mbele ya Waziri huyo

“Nimemuagiza afisa utumishi kumpeleka hospitalini kwaajili ya kupimwa kama anamechanganyikiwa na ripoti iliyoletwa kwangu nikuwa alikuwa amelewa hivyo tunamsimamisha kazi na kuanza kupitia faili lake tuone kama anaweza kuonyeka ama laa!”alisema Majaliwa

Aidha aliongeza kuwa watumishi wote hawatakiwi kwenda kazini wakiwa wamekunywa au wametumia kilevyi cha aina yeyote huku akisisitiza kuwa mahali pa kazi sio mahali pa kunywa pombe kwa kufanya hivyo nikuvunja sheria ya utumishi wa umma

“Kama mtumishi wa umma anavunja sheria kwa kunywa pombe kazini atachukuliwa sheria kwa kuwa hata Yule mtoto aliyekabidhiwa kumfundisha anamfundisha kwa misingi ipi?wafanye kazi kwa maadili mema”alisema Majaliwa

Aliongeza kuwa hii sio hapa tu bali sehemu yeyote mfanyakazi wa serekalini au sekta binafsi haruhusiwi kufanya kazi akiwa amelewa hivyo mtu yeyote akikutwa hivyo anastaili kufukuzwa kazi.

September 25, 2012

MWALIMU AFUNGWA MIAKA MITATU JELA KWA KOSA LA KUMPA MWANAFUNZI MIMBA.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mwalimu wa shule ya msingi, Daniel Lukindo mwenye umri wa miaka 24, amekukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi, Halima Rashidi, wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kwaluguru.
Kimaadili, sitetei alichokifanya, ila kisheria ni sawa kwa mtu kwenda jela kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne? Sijui kama umri umebadilika siku hizi lakini tulipokua kidato cha nne, mimi na wanafunzi wenzangu wote tulikua na umri kati ya miaka kati ya 16 na 18. Ingawa tulikua wanafunzi, tayari tulikua watu wazima na tulijua mabaya na mazuri, na tulijua tunachokifanya. Nilivyodhani mimi, sheria kama hizi ni za kuwalinda wasichana/wavulana wenye umri mdogo ambao hawajapevuka kiakili; lakini kwa mtu aliyekua kidato cha nne, akipata mimba ni uzembe wake maana ana umri wa kutosha kujua anachokifanya. Na sidhani kama kazi ya sheria ni kulinda uzembe wa watu. Au mnaonaje? Na kama mwl. Lukindo anakwenda jela kwa miaka mitatu, je huyo msichana naye ataadhibiwa maana na yeye alishiriki katika tendo hilo na ana umri wa kutosha kutambua athari za anachokifanya?
Anyway, back to the story, akisoma mashtaka katika shauri hilo, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Elibaliki Polanjo, aliiambia mahakama kuwa kati ya Novemba mwaka jana na Februari mwaka huu katika Kijiji cha Magamba, mwalimu huyo, wa shule ya msingi ya Magamba iliyopo Handeni, Tanga, alikuwa akifanya mapenzi na mwanafunzi huyo na baadaye, kumpa ujauzito.
Katika kesi hiyo iliyokuwa chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni, Patrick Maligana, mshtakiwa alikiri kosa lake, akikubaliana na maelezo yote yaliotolewa na mwendesha mashtaka.
Kufuatia hatua hiyo, Hakimu Maligana, alimtia hatiani na kumhukumu kutumikia adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Akifafanua kuhusu adhabu hiyo, Maligana alisema mshtakiwa alitenda kosa baya na hasa ikizingatiwa kwamba ni mwalimu anayepaswa kuwa mfano mzuri katika jamii, kwa kuzuia na kukomesha wimbi la matukio ya wanafunzi wa kike kupata mimba.
“Sheria inasema mwanaume yeyote atakayempa mimba mwanafunzi atakuwa ametenda kosa na kama atapatikana na hatia, atastahili kutumikia kifungo kisichopungua miaka mitatu jela na kisichozidi miaka sita. Kwa hiyo sheria hiyo inalinda wasichana kutokana na status yao, ya kama ni wanafunzi au la, na sio kutokana na umri wa kuelewa/kutoelewa athari ya kinadhofanyika? Ina maana ni sawa kufanya mapenzi na msichana wa miaka 14 asiyekuwa mwanafunzi lakini ni kosa kufanya mapenzi na msichana wa miaka 18 aliyekua mwanafunzi? Naomba mnielimishe mnaoelewa sheria hii maana kwangu it doesn’t make sense at all)
Kwa Kosa hili halitakuwa na nafasi ya kulipa faini,” alisema Maligana. Aliongeza kuwa adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa walimu na wanaume wengine wenye tabia ya kupenda kufanya mapenzi na wanafunzi wa kike. (Vipi kuhusu mwalimu wa kike akifanya ngono na mwanafunzi wa kiume enh? Sheria hapo inasemaje? Hmm?)

September 24, 2012

MTOTO MARTHA MAZURA ALIYESHINDA SHINDANO LA NATIONAL BOOK FESTIVAL MAREKANI HUYU HAPA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Martha Mazura (11), mshindi wa shindano la national Book Festival akipiga picha ya pamoja na baba yake mzazi, Bw. Amos M. Cherehani baada ya kupokea tuzo la uandishi bora wa insha lilioandaliwa na the Library of Congress, jijini Washington DC nchini Marekani Jumapili, September 23, 2012 ambapo kati ya washiriki zaidi ya 200, ni washiriki 19 tu ndiyo walioshinda shindano hilo akiwemo Martha ambaye ni Mtanzania pekee kwa mwaka huu kushinda tuzo hilo.

Martha Mazura, Mtanzania aliyeshiriki shindano La uandishi wa insha lilioandaliwa na Library of Congress liitwayo ‘National Book Festival 2012” na kutunukiwa cheti pamoja na zawadi nyingine akipiga picha ya pamoja na waandaaji wa shindano hilo Jumapili, September 23, 2012. Martha ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya St. Anthony Catholic School mjini Washington DC.

Martha Mazura akifurahia ushindi wake

September 21, 2012

HII NDIO FURAHA YA KUMALIZA SHULE, WAHITIMU DARASA LA SABA WALONGA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam wakifurahia na sahani zao za chakula baada ya kumaliza mtihani wa kuhitimu darasa la saba shuleni hapo jana. (Picha na Fadhili Akida).
 
KILA MMOJA KIONYESHA FURAHA KWA KUMALIZA SALAMA ELIMU YA MSINGI

HONGERENI SANA WANAFUNZI WOTE MLIOMALIZA DARASA LA SABA!

UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI, MWANAFUNZI AJIFUNGUA MTOTO AKIFANYA MTIHANI WA DARASA LA SABA MULEBA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Wanafunzi wakitoka darasani katika moja ya shule za msingi iliyoko wilayani Muleba, mkoa wa Kagera.

Mwanafunzi wa darasa la saba amejifungua wakati akifanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi wilayani Muleba mkoani Kagera.
Tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa nne na tano asubuhi katika Shule ya Msingi Kabiri katika Kijiji na Kata ya Kabirizi, Nshamba wakati mwanafunzi huyo, mwenye umri wa miaka 14 (jina na namba yake ya mtihani inahifadhiwa) akifanya mtihani wa pili na wenzake ndani ya chumba cha mtihani.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka shule hiyo, mwanafunzi huyo, alimwomba Msimamizi muda mfupi baada ya kuanza mtihani wa Hisabati, amruhusu kutoka nje kwa kuwa alikuwa akijisikia vibaya.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari kutoka eneo la tukio, baada ya mwanafunzi huyo kumwomba Msimamizi ruhusa, alimzuia akidhani ni ujanja wa kutaka kwenda kuchukua majibu, lakini baadaye aliona akijinyonganyonga.
"Msimamizi alimwuliza anaumwa nini akamwambia anaumwa tumbo na baada ya kuendelea kumhoji alimweleza wazi kwamba anaumwa uchungu, hali iliyomfanya Msimamizi aende kwa mmoja wa walimu wa shule hiyo na kumwomba msaada," alisema mmoja wa watahiniwa hao.
Aliongeza: "Walimchukua na kumwingiza kwenye nyumba ya mwalimu huyo na kumfuata mkunga wa jadi ambaye alimsaidia kujifungua salama mtoto wa kiume".
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mtoto huyo alipewa jina la OMR- mfumo mpya maalumu unaotumika kujibu maswali ya mtihani wa darasa la saba mwaka huu, ambapo mwanafunzi anaainisha jibu sahihi kwa kusiliba kwa kalamu ya risasi.
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Ofisa Elimu wa Wilaya ya Muleba, Savera Celestine alithibitisha binti huyo kujifungua, lakini hakutaka kulizungumzia kwa undani suala hilo, kwa madai kuwa mzungumzaji mkuu wa masuala yote ya mtihani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya.
"Ni kweli tukio hilo lipo, lakini mimi ndio nimefika hapa ofisini sasa hivi, sijapokea taarifa rasmi juu ya tukio hilo, lakini hata kama ningelikuwa nalo siwezi kulizungumzia kwa sababu anayepaswa kuzungumzia masuala yote ya mtihani huu ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, hebu mpigie atakupa taarifa," alisema Kaimu Ofisa Elimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mtihani ya Wilaya, Oliver Vavunge alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuzungumzia tukio hilo, hakukiri wala kukanusha kuwapo tukio hilo na kusisitiza, kwamba atazungumza baada ya kupokea taarifa ya wilaya nzima kuhusu mtihani huo.
"Kwa sasa niko huku kisiwani nashughulikia masuala ya mtihani, siwezi kuzungumzia jambo lolote la mtihani, natarajia kufanya hivyo kesho (leo) ambapo nitakuwa nimepata taarifa ya wilaya nzima, tena tutakuwa tumefanya majumuisho yote," alisema Vavunge.
Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Ally Rajabu naye kwa njia ya simu, alikiri kutokea tukio hilo na kueleza kwamba baada ya mwanafunzi huyo kujifungua, alionekana kuchoka na walimtoa kwenye nyumba ya mwalimu na kumpeleka kwao.
Alisema hata hivyo, alikuwa chini ya ulinzi wa askari waliokuwa wakimsubiri apate nguvu ili ikiwezekana arejeshwe shuleni kuendelea na mtihani, ambao alipaswa kumalizia Hisabati na kisha kufanya mtihani mwingine wa Kiswahili ambao ulikuwa ukifuata.
Mkuu wa Wilaya, Lembris Kipuyo naye alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa kwa mujibu wa taarifa alizopewa na vyombo vya ulinzi na usalama kupitia Msimamizi wa Mtihani shuleni hapo, Christina Didas, mwanafunzi huyo aliendelea na mtihani wa Hisabati na baadaye wa Kiswahili ambao ulikuwa wa mwisho kwa juzi.
"Ni kweli tumepatwa na tukio hilo na taarifa rasmi nilizonazo ni kwamba baada ya mwanafunzi huyo kujifungua salama, alipewa muda wa kupumzika na baadaye alirejea na kufanya mitihani yake yote na nimeelezwa kwamba leo (jana) pia kama hali yake itakuwa nzuri ataendelea na mitihani ya mwisho," alisema Kipuyo jana alipozungumza na gazeti hili kwa simu.
Katika tukio lingine, Kipuyo alibainisha kuwa katika Shule ya Msingi ya Kabitembe Kata ya Karambi, Kimwani, wanafunzi 18 waliokuwa wakifanya mtihani huo, walikumbwa na taharuki baada ya darasa walimokuwa wakifanyia mtihani kuezuliwa paa.
Alisema wakati wanafunzi hao wakiendelea na mtihani, mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali ilikuwa ikinyesha na ghafla uliezua na kubomoa sehemu ya ukuta wa darasa hilo na kusababisha karatasi za kujibia mtihani kuchafuka na kulowa.
"Hata hivyo, baada ya purukushani hiyo wasimamizi waliweka mambo sawa ikiwa ni pamoja na kuandaa darasa lingine ambapo wanafunzi walihamishiwa huko na kuendelea na mtihani wao, ingawa walichelewa kumaliza mtihani huo kutokana na tatizo lililokuwa limejitokeza," alisema Kivuyo.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema mtihani huo uliofanyika kwa siku mbili, umemalizika salama huku akibainisha kuwa usahihishaji mpya wa kompyuta utasaidia matokeo kutoka mapema.
Pia usahihishaji huo utasaidia kuipunguzia Serikali gharama kwa kutumia muda mfupi.
Hayo yalibainishwa jana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alipokuwa akizungumzia miihani huo uliomalizika jana mchana.
Akizungumzia Ofisi ya Makamu wa Rais, ambapo watahiniwa walitumia fomu maalumu za teknolojia hiyo, alisema wanafunzi walishafundishwa matumizi yake na kufanya majaribio kwa teknolojia hiyo.
"Kuanzia Julai, wanafunzi wote walikuwa wakifanya majaribio ya wiki kwa teknolojia hii mpya na walizoea, hivyo tuliwatayarisha … wanaolalamika wanatafuta sababu tu kwani huu ni mtihani," alisema Mulugo.
Alisisitiza kuwa mtihani ambao pia utasahihishwa kwa mashine maalumu ya kompyuta, utasaidia kupunguza gharama za usahihishaji wa mtihani na kufanya matokeo yatoke mapema.
Alitoa mfano kuwa mwaka jana walitumia walimu 3,890 kusahihisha mtihani huo na walitumia siku 40 jambo lililosababisha gharama kubwa kulipa walimu.
Pia mbali na gharama hizo, wanafunzi wengine waliokuwa wakiendelea na masomo walikosa fursa hiyo, kwani walimu walikuwa wakisahihisha mtihani.
Mulugo alisema tofauti na mwaka huu kwa teknolojia hiyo, usahihishaji utatumia siku 20 na watu 250 ambao nao watakuwa na kazi ya kuangalia kompyuta kama zitaleta matatizo na umeme kukatika.
Alisema nchi nyingi zinatumia teknolojia hiyo kama Ghana iliyoanza mwaka 1960, nyingine ni Kenya, Rwanda, Lesotho, Nigeria, Afrika Kusini na Zambia.
Mulugo alisema licha ya siku ya kwanza baadhi ya sehemu kuchelewa kufikiwa na mtihani, hakukutokea kuvuja huku waliosababisha uzembe huo, wakianza kujieleza leo.

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA/WALIOPATA MIKOPO MAJINA YAO HAYA HAPA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
TCU
SELECTED APPLICANTS FOR THE 2012/2013 ADMISSIONS


The Tanzania Commission for Universities (TCU) in Collaboration with the National Council for Technical Education (NACTE) is announcing the names of Applicants who were seleted into various programs for the 2012/2013 Admissions. However, the list of some applicants who were selected into various programs but obtained no loan, applicants who were returned by some institutions, and selected applicants who asked for transfer, will be announced before 21 September 2012

To view selected applicants with Loans, please click here...

To view selected applicants through Mozambique Scholarships, please click here...

To view selected applicants with Loans but subject to verification with HESLB (Previous Lonee),please click here ...

WANAFUNZI WALIOPATA MIKOPO 2012/2013 BOFYA HAPA

Click the Links Below to view the list (arranged by the University Code alphabetically):

September 20, 2012

SIMPLE WAY TO SUCESS via @millionfortune on twitter

Tweeted this Like this, be the first of your Friends #SIMPLEWAYTOSUCESS:
#SIMPLEWAYTOSUCESS

September 19, 2012

JUST IN: KUTOKA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB) WANAFUNZI 3,900 WATAKOSA MKOPO WA ELIMU YA JUU KWA MWAKA 2012/13

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Bodi ya Mikopo wa elimu ya juu (HESLB) jana ilitangaza kwamba zaidi ya waombaji 3,900 ambao wametimiza vigezo kwa mikopo hawataweza kupata fedha kutokana na upungufu wa bajeti ya serikali.

Walioomba mkopo kwa ujumla wao ni 49,895.

Asangye Bangu, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB alisema kuwa kati ya wanafunzi hao, 33,050 ndio ambao walitimiza vigezo kwa ajili ya kupata mikopo, na kwamba waombaji 29,113 tu ndio watakaopewa mkopo kwa mwaka 2012/2013.

Bangu alisema hata hivyo mpaka sasa bodi imefanikiwa kutenga mikopo kwa waombaji 28,454 kati ya 29,113 amabao watafanikiwa kupata mikopo hiyo.

Alisema kulikuwa na waombaji 659 ambao wanasubiriwa kusahihisha baadhi ya makosa katika maombi yao ndani ya siku 14.

"Baada ya kutathmini majina ya waombaji ambao walitimiza vigezo, ilitulazimu kuwaacha baadhi yao kwasababu bajeti haitoshi" alisema akieleza kwamba bajeti ndogo ilikuwa bado ni changamoto.

Kipaumbele kwa mwaka huu tumetoa kwa wanafunzi wanaosoma sayansi ya matibabu(medicine), elimu(education), masomo ya sayansi na hisabati(science & mathematics), ujenzi(construction) na uhandisi umwagiliaji(irrigation engineering).

Kwa mwaka huu, Serikali imetenga 345,000,000,000 / - kwa ajili ya mikopo ya mwanafunzi wa elimu ya juu, kutoka 317,800,000,000 / - kwa mwaka jana. idadi ya wanafunzi waliofuzu kwa ufadhili imeongezeka kwa karibu 12% ikilinganishwa na mwaka jana wanafunzi 26,000 walipata mikopo.

Wa waombaji ambao waliohitimu kwa mikopo, 9088 walikuwa wanawake, wakati 19,366 walikuwa wanaume.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat