StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

Showing posts with label UDAKU. Show all posts
Showing posts with label UDAKU. Show all posts

November 12, 2012

MTOTO WA MIAKA MITATU ACHOMWA MOTO KISHA KULAZIMISHWA KULA KINYESI CHAKE MAJENGO JIJINI MBEYA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

MTOTO ANETH AKIWA AMEOKOLEWA NA WASAMARIA WEMA HUKO MAJENGO


HIVI NDIVYO ALIVYOUNGUZWA MTOTO ANETH NA MAMA YAKE MDOGO


HUYU NDIYO MAMA MDOGO WA ANETH AMEJULIKANA KWA JINA LA BAHATI LUKANGARA NDIYO ALIYEMUUNGUZA MTOTO ANETH




HAPA MAJIRANI WAKIJARIBU KUMUULIZA SABABU ZA KUMUUNGUZA HUYO MALAIKA WA MUNGU NINI SABABU YAKE MPAKA AKACHUKUA HATUA YA KUMUUNGUZA LAKINI KWA KIBURI CHA HUYO MAMA ALIKAA KIMYA KABISA BILA YA KUJIBU CHOCHOTE


MWENYEKITI WA MTAA HUO HABIBA MWAKITALU AMEMBEBA MTOTO ANETH TAYARI KWA KUMPELEKA HOSPITALI HUKU NYUMA AKIFUATIWA NA MWESHIMIWA DIWANI KATA YA MAJENGO SAMWELI


WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMCHUKUA MAMA HUYO NA KUMPELEKA KITUO CHA POLISI




MTUHUMIWA NA MGONJWA WANAINGIZWA KATIKA GARI LA MWESHIMIWA DIWANI TAYARI KWA KUPELEKWA POLISI

Katika hali isiyo ya Kawaida Mkazi wa majengo jijini Mbeya Ndugu Bahati Rukangara amemchoma moto mtoto mdogo wa mika 3 aliyefahamika kwa jina la Aneth kisha kumfungia Ndani na kumlazimisha ale kinyessi chake.

Akizungumza Mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Habiba Mwakitabu amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10 :30 asabuhi ambapo majirani na mwanamke huyo waligundua mara baada ya kusikia sauti ya mtoto huyo akilia kutokana na maumivu.

Amesema mara baada ya kusikia sauti hiyo walifika eno hilo na kunza kumhoji ili kufahamu kiini cha tatizo hilo ambapo alishindwa kutoa ushirikiano ndipo walipo anza kumpiga .
Amesema kutokana na hali hiyo majirani walilazimika kubomoa mlango ndipo walipo mkuta mtoto huyo akiwa uchi huku ameungua vibaya mwilini hasa katika upande mmoja eneo la mkono wa kushoto .

Amesema mara baada ya kumhoji mtoto huyo aliwaeleza kuwa mama yake mdogo alichukua nguo na mkumfunga mkononi kisha kumwagia maji ya moto pamoja na kumlazimisha ale kinyesi chake hali ambayo iliwafanya washindwe kuvumilia na kuanza kupiga kelele kwa lengo la kuomba msaada kwa watu wengine.

Kwa mujibu maelezo ya mwenyekiti huyo amesema kuwa Mtuhumiwa huyo amekuwa akifanya vitendo vya manyanyaso kwa mtoto huyo marakwamara ambapo wamekuwa wakimuonya lakini amekuwa si mtu wa kusikia.
Ameesema mtoto huyo si wa kwa kwakwe kwani amekuwa akiishi naye kwa muda mrefu sasa ambapo aliachiwa na dada yake ambaye hakufahamika kuwa nayishi wapi kwa sasa.

Hata Diwani wa kata hiyo Ndugu Samuel Mamboma alifika eneo hilo tukio na kutoa msaada wa usafiri kwa lengo la kumfikisha mama huyo polisi pamoja na mtoto huyo ambaye naye alikimbizwa Hospitali.
Hata hivyo amesema tukio hilo si la kwanza kutokea katika meaeno hayo kwani kumekuwepo na matukio mengi hasa ya utoaji mimba na kutupwa watoto.

November 2, 2012

ANGALI JINSI GARI YA JACKLINE WOLPER ILIVYOCHOMWA MOTO NA WATU WASIO JULIKANA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends






HII KAULI ALIYO ITOA MWENYEWE KUTOKANA NA TUKIO HILO
“kiukweli mimi kama Jacquline Wolper sina ubaya na mtu yeyote, ila nmeshangaa kuona watu nisiyo wajua kuja usiku wa manane na kunichomea gari yangu. Kiukweli siwezi kumuhisi mtu ila najua ni lazima atakua mtu asiependa maendeleo yangu ni ni mtu mbaya sana kwangu. Na inawezekana kabisa alipanga kunia lakni kwa bahati nzuri siku hiyo sikua nyumbani nilikua nimesafiri. Tukio lilitokea usiku wa tarehe 23/10/2012 ambapo mtu alitumia matambara yaliyo na mafuta ya taa au Petrol akiwa kwa nje ya ukuta wa nyumba yangu akiwa anarusha kwa ndani. Nimepeleka taarifa kituo cha Polisi kawe kwa kutaka msaada wa kiupelezi na nitakua nawapa taarifa za kila kinachoendelea. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwani niko salama”

October 30, 2012

Huyu ndiye Binti aliyewagonganisha Ronaldo, Boateng

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
MADRID, HISPANIA
HABARI kutoka Hispania zinasema kuwa Kevin-Prince Boateng amemtaka Cristiano Ronaldo aache kuwasiliana na mpenzi wake, Melissa Satta.

Mwanzoni mwa mwezi huu kulikuwa na habari kwamba nyota wa zamani wa Manchester United, Cristiano Ronaldo ambaye kwa sasa anachezea Real Madrid alikuwa akiwasiliana na mwanamke huyo kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu lengo likiwa ni kumnasa kimapenzi.

Lakini watu wa karibu na Boateng wamesema kuwa mchezaji huyo hajafurahishwa na jambo hilo na amemtaka Ronaldo aache tabia hiyo.

Habari zilizochapishwa katika gazeti la Novella 2000 la Italia zinasema kuwa katika siku za karibuni mchezaji huyo alionekana akiomba namba ya dada huyo.

Cristiano Ronaldo ni mpenzi wa Irina Shayk ambaye amekuwa naye kwa miaka miwili sasa.

Boateng anatarajia kufunga ndoa na Satta mwakani.

October 23, 2012

ANGALIA PICHA NAMNA WEMA SEPETU ALIVYOFANYA KUFURU YA SHOPPING YA NGUO ZENYE THAMANI YA 4.3 MILION.!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends




Mrembo huyo alinaswa hivi karibuni akifanya manunuzi ya nguo tu, zenye thamani ya Sh. milioni 4.3 katika duka la Amina Designer lililopo ndani ya Jengo la Quality Centre jijini Dar.

“Ni utamaduni wa kawaida kwangu kufanya shopping mara kwa mara. Sioni uchungu wa kutoa fedha, labda ni kwa sababu natumia kadi kulipia, ningekuwa natoa kwenye pochi na kuhesabu kumpa muuzaji, nisingeweza kufanya hivyo, fedha nyingi kama ile ukiishika mkononi na kulipa kununua nguo roho inauma,” alisema Wema

HIZI NDIZO SABABU ALIZOTOA AUNT EZEKIEL ZA KUANZA NA HARUSI KABLA YA KITCHEN PARTY NA SEND-OFF

Tweeted this Like this, be the first of your Friends




Wiki iliyopita picha za muigizaji wa filamu nchini, Aunt Ezekiel akifunga ndoa zilisambaa kwa kasi kwenye mtandao na kuzua maswali mengi kama iwapo amefunga ndoa kweli ama ni usanii tu. Wengi waliamini kuwa amefunga ndoa na wengi pia walikuwa na mashaka.

Waliokuwa na mashaka walihisi si kweli kutokana na sababu zifuatazo.

1. Aunt Ezekiel alikuwa akiendelea kukusanya michango ya harusi iweje aamue kufunga ndoa wakati bado anachangisha?

2. Kwanini harusi yake isihudhuriwe na watu wake wa karibu hata kama ni ya kiislamu? (kutokana na picha hizo)

3. Aliwahi kuhojiwa na kudai kuwa angefunga ndoa mwezi November

Lakini ukweli kuwa picha hizo zilimaanisha kuwa tayari amefunga ndoa. Lakini kuna sababu za harusi yake kuwa hivyo.

“Ni mchumba wangu na hakika yeye ndiye mwenye maamuzi nikaamua nifanye hivyo,” ameiambia ‘Movie Leo’ ya Clouds FM.

“Naweza sema bado yaani siko sawa mpaka nihakikishe hivyo vitu vyote vimeenda vimepita salama manake unajua shughuli yoyote hata kama ndogo lakini lazima unajua yaani unakaa ni pressure yaani sijui itakuaje sijui itakuwa vipi

Kwahiyo naweza kusema kwasababu ni mwanzo kwahiyo bado kiukweli naona yaani huko mbele kutakuaje.”

Kutokana na kufanya mchakato wake ‘kiflashback’ yaani kuanza na hatua ya mwisho ya harusi na kurudi nyuma, muigizaji huyo pia ameelezea jinsi Kitchen Party za Send-off zitakavyokuwa,“nataka nifanye vitu vya tofauti na kila kitu nataka kiwe tofauti na vile watu ambavyo wamezoea kuviona au wamewahi kwenda , kwahiyo mwisho wa siku nikisema niseme itakuaje, itakuwa hivi itakuwa hivi naweza nikawa nimezusha ugomvi.”

And by the way sasa jina lake ni Rahma baada ya kubadilisha dini na kuwa muislamu.

MH, HAYA SASA FARID.....NDOO INAMHUSU

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Kiongozi wa uamsho Zanzibar...

October 19, 2012

BAADA YA KUTIMULIWA NYUMBANI RAYUU ADAIWA KUJIHIFADHI KWA CHUZI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

WAKATI msanii wa bongo movie Rayuu, picha zakezinazoonesha sehemu kubwa ya mwili wake na tattoo kuvunja mtandaoni, ishu hiyo sasa imechukua sura mpya baada ya kudaiwa amefukuzwa kwao na sasa amepata makazi ya muda kwa mkurungezi wake Mr Chuzi ambaye mara nyingi amekuwa akimshauri kuachana na vitendo vinavyoweza kumchafulia jina lake.

Wazazi wake walizipata habari zake ndipo waliamua kuchukua hatua hiyo tena bila hata kumpa nafasi kujitetea na kuwaeleza mambo yalivyokuwa.

Hata hivyo inadaiwa kuwa wazazi wake awali hawakujua habari hiyo lakini kuna baadhi ya watu ambao walikuwa na kinyongo na msanii huyo ndiyo waliopeleka habari hizo pamoja na picha nyumbani kwa madai kuwa wanataka kumkomoa.

Msanii huyo alidai kuwa hakuwa na njisi kwani waliofanyan hivyo ni watu ambao mara nyingi wamekuwa wakifanya kazi pamoja lakini hajui ni kwanini wamefanya hivyo ingawa hataki kujua sababu kwa sababu anaweza kuchukua hatua nyingine ambayo si nzuri

October 16, 2012

AUNT EZEKIEL NA WEMA SEPETU WAOMBA RADHI WATANZANIA ILA WATAENDELEA KUVAA NGUO FUPI!!!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends






LICHA ya kuomba radhi kutokana na kuvaa nusu uchi katika matamasha ya Fiesta mwaka huu, wasanii wa filamu nchini, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wamesema wataendelea kuvaa nguo hizo.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam jana, wasanii hao walielezea kujutia tukio hilo ambalo hawakulitarajia kutokea.
Walisema wao kama wasanii wa filamu, wanalazimika kuvaa mavazi kulingana na wakati na tukio husika, ndiyo maana walivaa mavazi yale, lakini tatizo lilikuwa ni urefu wa jukwaa.
Mmoja ya wasanii hao, Aunt Ezekiel alisema kwamba kilichotokea ni bahati mbaya kwani hawana uzoefu na majukwaa ya muziki na matokeo yake kuwa hivyo.
“Yale mavazi huwa tunayavaa kila mara, lakini kwa bahati mbaya jukwaa lilikuwa refu na ndiyo maana tulionekana hivyo…tunaomba msamaha na tumeshajifunza.
Tunapenda kuchukua fursa hii kuiomba radhi jamii yote, ndugu jamaa na marafiki kwa tukio hili ambalo hatukulitarajia,” alisema Aunt Ezekiel.
Akizungumzia tabia yake ya kupiga picha za utupu, Aunt alikana na kudai kwamba; “Hizo picha wanazodai ni za utupu si kweli, bali nilipigwa mgongo kwa ajili ya jalada la filamu ya Young Millionea.
Hizo nguo fupi sijaanza kuvaa jana wala juzi, hivyo kwa tukio lile ilitokea bahati mbaya na kuanzia sasa nitakuwa makini na vitu kama hivyo,” alisema Aunt Ezekiel.
Naye Wema, pamoja nakuomba radhi aliitaka jamii kutowachukulia vibaya kutokana na mavazi hayo, kwani mara nyingi wanavaa kulingana na wakati na mahali.
Alisema baada ya dosari hizo kujitokeza, aliamua kuanza kuvaa suruali za jeans au kaptula ili kuepukana na kitendo hicho.
Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi alisema baada ya tukio la wasanii hao, waliwaita na kuzungumza nao na mwisho wa siku walikiri makosa na wakaomba radhi.

September 26, 2012

HUU NDIO UJUMBE WA RIHHANA KWA CHRIS BROWN KABLA YAKUTINGA KIZIMBANI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Rihanna.


Kama unakumbukumbu Chris Brown alishtakiwa kwa kumpiga Rihanna mwaka 2009,na kutokana na kosa ilo alitakiwa kufanya kazi za kijamii kwa kipindi cha miezi sita.

Siku ya Jumatatu Chris alipandishwa kizimbani kutoa nyaraka za kuwa ameshamaliza adhabu aliyopewa ya kuihudumia jamii kwa kipindi cha miezi sita.




Wakati bado wengi wanajiuliza mambo aliyofanya Chris Brown kwa miaka mitatu iliyopita, but masaa machache kabla ya kuingia mahakamani, Ex- girlfriend wa Chris Brown, Rihanna alitweet directly massage kwa Chris akisema:



 

Chris akuchukua muda alijibu hivi:


 

Baada ya Chris kujibu, Rihanna alituma massage ya jumla ikisema hivi: 



Na kama tunavyokumbuka week kadhaa zilizopita Rihanna alimwambia Oprah kuwa bado anampenda Chris kupitia kipindi chake cha next chapter , na sasa yamejitokeza haya, Isn’t it time for them to just get back together?

September 25, 2012

CHAZ BABA: WANAWAKE WENYE FEDHA NDIYO WANANIWEKA MJINI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Charles Baba ‘Chaz Baba’.

PRESIDENT wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Baba ‘Chaz Baba’, ameweka plain kuwa katika maisha yake huwa anapenda kulelewa na wanawake wenye fedha kwa sababu ndiyo wanaomuweka mjini.
Chaz Baba aliitonya Mbovumbovu za Mastaa kuwa, mademu wengi wamekuwa wakimuomba nafasi ya kuwa wapenzi wake wakidhani watajipatia fedha pasipo kujua yeye mwenyewe anapenda kupewa chapaa na wanawake.
“Mimi napenda kulelewa bwana tena anayenilea awe na fedha na si vinginevyo, mimi siyo mtu wa kuhongahonga hovyo,” alisema Chaz Baba.

SHILOLE: WATU WANATUCHUNGULIA NYETI ZETU TUKIWA JUKWAANI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa jukwaani.

STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema suala la kuripotiwa kuwa wanavaa utupu linasababishwa na baadhi ya watu wanaopenda kuwachungulia wasanii wanapokuwa jukwaani na kuwapiga picha.
Akizungumza na Mbovumbovu za Mastaa, Shilole amesema watu hao wanatabia ya kuwachungulia kwa chini huku ‘wakiwafotoa’ picha na ndiyo chanzo cha matatizo mengi ya skendo zinazopamba magazeti kila kukicha.
“Yaani hili nimelishuhudia kwa macho yangu mtu anakuchungulia kwa chinichini halafu akikuotea vizuri ndiyo madhara yanakuwa makubwa kama tulivyoona kwa baadhi ya mastaa,” alisema Shilole.

HUYU NDIYE MWANAFUNZI ALIYEAMBUKIZA UKIMWI WANAUME 90 KWA MAKSUDI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Huyu ndio msichana alie kiri kuwaambukiza Ukimwi wanaume 90 kwa makusudi Huko nchini kenya ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo nchini humo ..ameweka wazi kuwa alifanya ngono na watu hao bila kutumia kinga makusudi ..amesema anayo list ya wote inayo jumuisha wanafunzi, vigogo na watu wengine mbalimbali..upo Hapo??

September 24, 2012

VURUGU KANISANI: ASKOFU ANUSURIKA KIPIGO KUTOKA KWA WAUMINI, AOKOLEWA NA POLISI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Askofu Mkuu wa Angikana Tanzania,la Dk. Valentino Mkowa aliyevuliwa kofia ya kiaskofu akiwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia wakimtoa nje ya Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga baada ya kuzuka kwa vuguru kubwa jana. Picha na Mussa Mwangoka



Mmoja wa waumini wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote la mjini Sumbawanga akiwa na jazba wakati wa vurugu zilizoibuka jana mara baada ya kutolewa uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Waumini wa Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga jana wakipiga kelele kupinga uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulinzi wa polisi. Picha na Mussa Mwangoka


Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania la Dk. Valentino Mkowa leo amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika kupata kipigo kutoka kwa waumini wake waliokuwa wenye hasira kali.

Vurugu kubwa ziliibuka mara baada ya kusomwa kwa tamko lililothibitisha kuwa nyumba ya maaskofu inamtambua Askofu Canon Kasagara kuwa ni kiongozi wao halali wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote Jimbo la Ziwa Rukwa mjini Sumbawanga.

Katibu mkuu wa Anglikana Dk, Dickson Chilongani ndiye aliyesoma tamko hilo mara baada ya kumalizika kwa ibada iliyoongozwa na Askofu Mkuu Dk. Mokiwa.

Akisoma tamko hilo Katibu Mkuu alisema kuwa sehemu ya hoja za msingi kamati ya usimamizi wa kanisa hilo zilidai kuwa uchaguzi uliomweka madarakani Askofu Kasagara uligubikwa na rushwa,si za kweli na nyumba ya maaskofu imeshindwa kuthibitisha hilo hivyo Kasagara ni askofu wao halali.

Kutokana na kauli hiyo waumini hao, walianza kupiga kelele ya kupinga maelezo hayo hali iliyosababisha mjumbe wa Kamati ya kusimamia kanisa hilo Flugence Lusunzu aliposhika kinasa sauti na kueleza kuwa wanao ushahidi wa kutosha kuwa rushwa ilitumika kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi huo uliofanyika zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Alidai kuwa uamuzi wa nyumba ya maaskofu haukuwapa fursa ya kusikiliza upande wa walalamikaji ili hali ushahidi upo wazi, kutokana kauli hiyo zilianza fujo zilisababisha askofu Mokiwa kutolewa lugha chafu, kuvuliwa kufia yake ya kiaskofu, huku wengine warusha viti ambavyo alivikwepa hado alipoondolewa akiwa chini ya polisi waliokuwa wamevalia kiraia.

Hali hiyo iliharibu amani iliyokuwa imetawala ndani ya Kanisa hilo ambapo uligeuka kuwa uwanja wa vita huku waumini wakisikika wakidai kuwa ni heri kanisa hilo lifungwe kuliko Askofu Kasagara kuliongoza.

Awali tangu nyakati za asubuhi, polisi waliovaa kiraia walitanda katika viunga vya kanisa hilo ambapo Askofu Mokiwa aliwasili na kulakiwa vizuri na waumini wake waliokuwa wakishangilia kwa nyimbo na mapambio.

Hata hivyo tayari waumini wa Kanisa hilo walionya kwamba askofu Kasagara asikanyage kwenye eneo hilo, kwani kufanya hivyo kunge hatarisha amani onyo ambalo upande wa askofu Kasagara walitii hivyo askofu huyo mwenye makazi yake wilayani Mpanda alibaki katika nyumba moja ya kulala wageni alikokuwa amefikia.

Mmoja wa waumini Julius Michael alisema kwa kuwa waumini wa Jimbo la Rukwa hawamtaki askofu Kasagara hakuna sababu ya kuwalazimishwa lakini nyumba ya maaskofu inapaswa kuangalia uwezekano wa kuligawa jimbo hilo.

Tayari Serikali imegawa mkoa wa Rukwa na kuzaa ule wa Katavi sasa hakuna umuhimu wa kuwalazimisha waumini wampokee mtu wasiyemtaka nyumba ya maaskofu waanzishe jimbo katika mkoa huo mpya na aongoze Kasagara.

Alisema iwapo watatumia nguvu kumuweka Askofu huyo Rukwa haitasaidia kitu kwani hawezi kuwaongoza watu wasiotaka kushirikiana nae.

Mgogoro katika Kanisa hilo umedumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa ambapo siku za nyuma waumini hao walimzuia Askofu Mkuu, Dk Valentino Mkowa kumsimika Askofu huyo na badala yake alisikimkwa tarehe 16, Juni mwaka jana Mjini Mpanda.

Kutokana na kujitokeza kwa mgogoro huo, ilifunguliwa kesi mahakamani ya Hakimu Mkazi Sumbawanga na waumini wa anglikana, Fulgence Rusunzu na Rojas Bendera na wenzao 191 yenye namba 11/2011 wakipinga kuchaguliwa kwa askofu Kasagala kuwa kiongozi wa Dayosisi hiyo.

Ambayo iliondolewa baada ya pande mbili zinazovutana kukubaliana kuwa baraza la maaskofu ndilo lenye dhamana ya kutatua mgogoro huo.

HUYU NDIYE CHUCHU HANS ALIYEAPA KUWA HAWEZI KUTOKA NJE YA NDOA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 
Chuchu Hans.

PAMOJA na kukiri kupewa uhuru wa kutosha na mumewe Frank Mtao, mkali wa Bongowood, Chuchu Hans amefunguka kuwa hawezi kutoka nje kama mastaa wengine wanavyoandamwa na skandali hiyo.
Chuchu aliiambia Bongowood kuwa anajitambua yeye ni nani katika jamii hivyo skendo haiwezi kumpata hata siku moja kwani hana tamaa ya fedha kama wengine.

September 21, 2012

UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI, MWANAFUNZI AJIFUNGUA MTOTO AKIFANYA MTIHANI WA DARASA LA SABA MULEBA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Wanafunzi wakitoka darasani katika moja ya shule za msingi iliyoko wilayani Muleba, mkoa wa Kagera.

Mwanafunzi wa darasa la saba amejifungua wakati akifanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi wilayani Muleba mkoani Kagera.
Tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa nne na tano asubuhi katika Shule ya Msingi Kabiri katika Kijiji na Kata ya Kabirizi, Nshamba wakati mwanafunzi huyo, mwenye umri wa miaka 14 (jina na namba yake ya mtihani inahifadhiwa) akifanya mtihani wa pili na wenzake ndani ya chumba cha mtihani.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka shule hiyo, mwanafunzi huyo, alimwomba Msimamizi muda mfupi baada ya kuanza mtihani wa Hisabati, amruhusu kutoka nje kwa kuwa alikuwa akijisikia vibaya.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari kutoka eneo la tukio, baada ya mwanafunzi huyo kumwomba Msimamizi ruhusa, alimzuia akidhani ni ujanja wa kutaka kwenda kuchukua majibu, lakini baadaye aliona akijinyonganyonga.
"Msimamizi alimwuliza anaumwa nini akamwambia anaumwa tumbo na baada ya kuendelea kumhoji alimweleza wazi kwamba anaumwa uchungu, hali iliyomfanya Msimamizi aende kwa mmoja wa walimu wa shule hiyo na kumwomba msaada," alisema mmoja wa watahiniwa hao.
Aliongeza: "Walimchukua na kumwingiza kwenye nyumba ya mwalimu huyo na kumfuata mkunga wa jadi ambaye alimsaidia kujifungua salama mtoto wa kiume".
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mtoto huyo alipewa jina la OMR- mfumo mpya maalumu unaotumika kujibu maswali ya mtihani wa darasa la saba mwaka huu, ambapo mwanafunzi anaainisha jibu sahihi kwa kusiliba kwa kalamu ya risasi.
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Ofisa Elimu wa Wilaya ya Muleba, Savera Celestine alithibitisha binti huyo kujifungua, lakini hakutaka kulizungumzia kwa undani suala hilo, kwa madai kuwa mzungumzaji mkuu wa masuala yote ya mtihani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya.
"Ni kweli tukio hilo lipo, lakini mimi ndio nimefika hapa ofisini sasa hivi, sijapokea taarifa rasmi juu ya tukio hilo, lakini hata kama ningelikuwa nalo siwezi kulizungumzia kwa sababu anayepaswa kuzungumzia masuala yote ya mtihani huu ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, hebu mpigie atakupa taarifa," alisema Kaimu Ofisa Elimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mtihani ya Wilaya, Oliver Vavunge alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuzungumzia tukio hilo, hakukiri wala kukanusha kuwapo tukio hilo na kusisitiza, kwamba atazungumza baada ya kupokea taarifa ya wilaya nzima kuhusu mtihani huo.
"Kwa sasa niko huku kisiwani nashughulikia masuala ya mtihani, siwezi kuzungumzia jambo lolote la mtihani, natarajia kufanya hivyo kesho (leo) ambapo nitakuwa nimepata taarifa ya wilaya nzima, tena tutakuwa tumefanya majumuisho yote," alisema Vavunge.
Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Ally Rajabu naye kwa njia ya simu, alikiri kutokea tukio hilo na kueleza kwamba baada ya mwanafunzi huyo kujifungua, alionekana kuchoka na walimtoa kwenye nyumba ya mwalimu na kumpeleka kwao.
Alisema hata hivyo, alikuwa chini ya ulinzi wa askari waliokuwa wakimsubiri apate nguvu ili ikiwezekana arejeshwe shuleni kuendelea na mtihani, ambao alipaswa kumalizia Hisabati na kisha kufanya mtihani mwingine wa Kiswahili ambao ulikuwa ukifuata.
Mkuu wa Wilaya, Lembris Kipuyo naye alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa kwa mujibu wa taarifa alizopewa na vyombo vya ulinzi na usalama kupitia Msimamizi wa Mtihani shuleni hapo, Christina Didas, mwanafunzi huyo aliendelea na mtihani wa Hisabati na baadaye wa Kiswahili ambao ulikuwa wa mwisho kwa juzi.
"Ni kweli tumepatwa na tukio hilo na taarifa rasmi nilizonazo ni kwamba baada ya mwanafunzi huyo kujifungua salama, alipewa muda wa kupumzika na baadaye alirejea na kufanya mitihani yake yote na nimeelezwa kwamba leo (jana) pia kama hali yake itakuwa nzuri ataendelea na mitihani ya mwisho," alisema Kipuyo jana alipozungumza na gazeti hili kwa simu.
Katika tukio lingine, Kipuyo alibainisha kuwa katika Shule ya Msingi ya Kabitembe Kata ya Karambi, Kimwani, wanafunzi 18 waliokuwa wakifanya mtihani huo, walikumbwa na taharuki baada ya darasa walimokuwa wakifanyia mtihani kuezuliwa paa.
Alisema wakati wanafunzi hao wakiendelea na mtihani, mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali ilikuwa ikinyesha na ghafla uliezua na kubomoa sehemu ya ukuta wa darasa hilo na kusababisha karatasi za kujibia mtihani kuchafuka na kulowa.
"Hata hivyo, baada ya purukushani hiyo wasimamizi waliweka mambo sawa ikiwa ni pamoja na kuandaa darasa lingine ambapo wanafunzi walihamishiwa huko na kuendelea na mtihani wao, ingawa walichelewa kumaliza mtihani huo kutokana na tatizo lililokuwa limejitokeza," alisema Kivuyo.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema mtihani huo uliofanyika kwa siku mbili, umemalizika salama huku akibainisha kuwa usahihishaji mpya wa kompyuta utasaidia matokeo kutoka mapema.
Pia usahihishaji huo utasaidia kuipunguzia Serikali gharama kwa kutumia muda mfupi.
Hayo yalibainishwa jana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alipokuwa akizungumzia miihani huo uliomalizika jana mchana.
Akizungumzia Ofisi ya Makamu wa Rais, ambapo watahiniwa walitumia fomu maalumu za teknolojia hiyo, alisema wanafunzi walishafundishwa matumizi yake na kufanya majaribio kwa teknolojia hiyo.
"Kuanzia Julai, wanafunzi wote walikuwa wakifanya majaribio ya wiki kwa teknolojia hii mpya na walizoea, hivyo tuliwatayarisha … wanaolalamika wanatafuta sababu tu kwani huu ni mtihani," alisema Mulugo.
Alisisitiza kuwa mtihani ambao pia utasahihishwa kwa mashine maalumu ya kompyuta, utasaidia kupunguza gharama za usahihishaji wa mtihani na kufanya matokeo yatoke mapema.
Alitoa mfano kuwa mwaka jana walitumia walimu 3,890 kusahihisha mtihani huo na walitumia siku 40 jambo lililosababisha gharama kubwa kulipa walimu.
Pia mbali na gharama hizo, wanafunzi wengine waliokuwa wakiendelea na masomo walikosa fursa hiyo, kwani walimu walikuwa wakisahihisha mtihani.
Mulugo alisema tofauti na mwaka huu kwa teknolojia hiyo, usahihishaji utatumia siku 20 na watu 250 ambao nao watakuwa na kazi ya kuangalia kompyuta kama zitaleta matatizo na umeme kukatika.
Alisema nchi nyingi zinatumia teknolojia hiyo kama Ghana iliyoanza mwaka 1960, nyingine ni Kenya, Rwanda, Lesotho, Nigeria, Afrika Kusini na Zambia.
Mulugo alisema licha ya siku ya kwanza baadhi ya sehemu kuchelewa kufikiwa na mtihani, hakukutokea kuvuja huku waliosababisha uzembe huo, wakianza kujieleza leo.

September 20, 2012

YULE ALIYELAMBA MILLION 10 ZA TIGO BEATS HUYU HAPA...

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mkazi wa Kijiji cha magugu, Sungaji Kata, Wilaya ya Mvomero Mkoa Morogoro, Hamis Athuman (kushoto) akikabidhiwa mfano hundi ya  thamani ya Sh. milioni kumi kutoka kwa mwakilishi wa kapuni ya simu za mkononi Tigo,baada kushinda promosheni ya Tigo Beats

SHAKIRA ASUBIRIA KWA HAMU KUMPATA MTOTO WAKE WA KWANZA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Shakira will be a mom, the singer announced on her website on Wednesday.
"As some of you may know, Gerard and I are very happy awaiting the arrival of our first baby!" she wrote of boyfriend Gerard Pique, a Spanish soccer player. "At this time we have decided to give priority to this unique moment in our lives and postpone all the promotional activities planned over the next few days."

September 19, 2012

PICHA P-SQUARE, ANNIE IDIBIA, GENEVIEVE NA WENGINEO WENGI KATIKA BIRTHDAY YA 2FACE IDIBIA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

photo


photo
P SQUARE WAKIWA KATIKA PARTY HIYO

photo

photo

photo

photo

photo

CHEZEA USINGIZI WEWEEEE....!!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

September 18, 2012

HUYU NDIYE YULE KIJANA ALIYEFARIKI AKIJARIBU KUONGEZA UKUBWA WA MAUMBILE

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

DUNIA haikaukiwi matukio ya kustaajabisha, kwa hakika huu ni ulimwengu maridhawa na hawakukosea walionena kwamba dunia hadaa ulimwengu shujaa.

Stori ya kusikitisha, inatokea nchini Marekani ambako kijana Justin Street, amepoteza maisha akiwa kwenye jaribio la kuongeza ukubwa wa nyeti yake.

Habari kamili ipo hivi; Justin, 22, akiwa baba wa watoto wawili alikwenda kwa mwanamama Kasia Rivera ,35, aliyejitangaza kuwa ni mtaalamu wa tiba za kuongeza ukubwa wa nyeti za kiume.

Kasia aliweka matangazo barabarani kuwa anayo tiba ya kuongeza ukubwa wa nyeti za kiume, hivyo kumfanya Justin ahamasike kwenda kupata dawa hiyo ili kujiongezea ushababi.

Wanasema tamaa mbele mauti nyuma, ndivyo ilivyotokea kwa Justin, kwani baada ya kuomba dawa ya kuongeza ukubwa wa maumbile yake ya kiume, alidungwa sindano yenye madini ya silikoni.

Madini hayo, alidungwa kwenye nyeti yenyewe na baada ya muda mfupi, hali ya afya yake ilibadilika kuwa mbaya, alizorota na siku iliyofuata alifariki dunia.

Kutokana na tatizo hilo, Kasia alifikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji akituhumiwa kufungua zahanati bubu ndani ya nyumba yake iliyopo New Jersey, vilevile kutoa tiba za kiafya wakati hana taaluma hiyo wala leseni ya kuendesha kazi hiyo ya utoaji huduma za afya.

Kasia alipandishwa kizimbani wiki iliyopita, uchunguzi wa maiti umethibitisha kwamba Justin alifikwa na mauti baada ya madini ya silikoni aliyodungwa kwa sindano kuziba njia za mishipa ya damu.

Mmoja wa madaktari waliomfanyia uchunguzi Justin alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kusikia silikoni inayotumika kuongeza ukubwa wa matiti ya wanawake imetumika kwenye kuongeza ukubwa wa uume.Kasia, amekana kuhusika na mauaji hayo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat