StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 29, 2012

MAONYESHO YA SARAKASI YA MAMA AFRIKA YAENDELEA KURINDIMA NEW WORLD CINEMA DAR

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



“Karibuni watanzania wote muone sarakasi na utamaduni wa kitanzania”.



Trade Marketing Supervisor wa kampuni ya simu za mkononi ya TIGO ambao ndio wadhamini wakuu wa maonyesho ya ‘Sarakasi ya Mama Afrika’ yanayoendelea katika viwanja vya New World Cinema Bw. Gaudens Mushi akiwakaribisha wageni waliohudhudhuria onyesho hilo. kushoto ni Afisa Mahusiano wa TIGO.



Pichani Juu na Chini ni mfululizo wa maonyesho ya sarakasi ya ‘Mama Africa Circus’.













Picha Juu na Chini ni baadhi ya wadau walioshiriki maonyesho hayo wakifurahia.

MAREHEMU MEJA JENERALI MSTAAFU, ANATORY RUTA KAMAZIMA KUAGWA LEO SEPT. 29 LUGALO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Marehemu Meja Jenerali Mstaafu, Anatory Ruta Kamazima

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Meja Jenerali Mstaafu, Anatory Ruta Kamazima (pichani), ambaye amefariki dunia mwanzoni mwa wiki hii, ataagwa rasmi katika Hospitali ya Lugalo leo tarehe 29 Septemba, 2012 saa saba mchana (7.00 mchana) Nyumbani kwa marehemu eneo la Tegeta - Kibaoni baada ya soko la Nyuki Maruku Cottage.

Imetolewa na
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPT 29

Tweeted this Like this, be the first of your Friends







MANISPAA YA ILALA KUWAHUSISHA WANAHABARI NA WAKAZI KATIKA KAMPENI YA USAFI.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia swala la kuweka jiji katika hali ya usafi akisema kuwa Manispaa ya Ilala inakusudia kuingia ubia na wanahabari katika kufanikisha lengo la kuwa Manispaa safi ukizingatia ndio kitovu cha mji wa Dar es Salaam.

Ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kugharamia usombaji wa taka kwani wengi wao wamekuwa wakiona gharama wanazotozwa kwa ajili ya kubeba taka ni kubwa lakini watambue kuwa kwa siku taka zinazokusanywa hufikia hadi tani 1088.



Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Ilala wakati akizungumzia mikakati ya Manispaa hiyo kuhakikisha inakuwa mfano wa kuigwa kwa usafi jijini.



Pichani Juu na Chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakichangia maoni yao namna ya kuboresha Usafi katika Manispaa hiyo.





Afisa Usafishaji wa Manispaa ya Ilala Bw. Samuel Bubegwa akitoa Elimu kwa wanasemina kuhusiana na jinsi Manispaa hiyo inavyotumia mbinu mbadala baada ya kukusanya taka ambapo huzichambua na kuziweka katika makundi tofauti na nyingine kutumika kuzalishia mbolea ambayo inauzwa na kukuza kipato cha kuendeshea huduma mbalimbali ndani ya manispaa hiyo.



Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala Bi. Pamela Mugaruka akielezea matumizi ya sheria ndogo ambazo zimetungwa mwaka 2011 kwa watu wanaozikiuka wakiwemo wanaogoma kulipa ada na kufafanua makosa, adhabu ikiwemo faini zitakazowakabili kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha sheria hizo.



Mwenyekiti wa Kata ya Mwenbe Madafu Wifred Kipondya akielezea mafanikio yaliyofikwa na kata yake kutokana na utaratibu waliojiwekea wa kukusanya kodi ambapo sasa wameweza kufikia kukusanya hadi shilingi Milioni 70.



Chati ya mapato na matumizi kwa mwezi kwa mwaka 2009 iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kata ya Mwembe Madafu Bw. Wifred Kipondya iliyopo ndani ya Manispaa ya Ilala wakati wa semina ya waandishi wa habari.



Baadhi ya maafisa wa Manispaa ya Ilala na waandishi wa habari waliohudhuria semina hiyo leo jijini Dar es Salaam.

MGAMBO WATAKA KUWAPIGA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


wakati sakata la kuwatoa wamachinga jijini Arusha mjini likiendelea waandishi wa habari wamenusurika kugeuzwa mboga na wanamkambo wanaofanya kazi hiyo.


Waandishi hao ambao majina yanaifathiwa ambapo mmoja wapo anatoka katika gazeti la Nipashe na mungine Majira wamenusurika kupigwa pamoja na kuvunjiwa kamera zao wakati walivyokuwa wakiendelea na majukumu yao katika eneo la golden rose jijini Arusha.


Mdau wetu wa libeneke la kaskazini alishuhudia tukio hilo likifanyika wakati waandishi hao wakijaribu kupiga picha wakati mgambo hao wajiji wakiwa wanakusanya vibanda vya wafanya biashara wadogo vilivyokuwa vimewekwa pembezoni mwa barabara.


Mgambo hao wakati waandishi hao wakijaribu kuchukuwa picha hizo za mgambo hao majira ya saa kumi na mbili na nasu jioni mgambo hao waliwavamia na kutaka kuwanyanganya kamera zao ,mara baada ya kupewa amri hiyo na mtu ambaye alikuwa akipita na gari la matangazo akiwasihi machinga kutoa vitu vyao barabarani.

"wakamateni hao waandishi wanaopiga picha wawekeni kwenye gari chukueni na kamera zao "sauti hiyo ilikuwa ikitajwa na mc huyo ambaye alikuwa anatangaza barabarani

Kufuatia tukio hilo lilifanya wananchi wajitokeze kwa wingi na kuanza kuwarushia maneno makali mgambo hao huku wakisema kuwa wanataka kuwafanya kama walivyomfanya mwandishi wa chanel ten


Wakati vurugu hiyo ikiendelea baadhi ya waandishi wa habari walikuja na kuamua tatizo hilo na ndipo mgambo hao wakaondoka mara baada ya kupewa amri na mmoja wa askari aliyekuwa kwenye gari la polisi ambao walikuwa wakiwawanasindikiza gari hilo la mgambo.

MHESHIMIWA RAIS DKT J. KIKWETE AWAAGA MABALOZI JIJINI DAR ES SALAAM

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Cuba nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Ernesto Gomes Dias leo Septemba 28, 2012 Ikulu jijini DAr es salaam Dar es salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Iran nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Mohsen Movahhedi Ghomi leo Septemba 28, 2012 Ikulu Dar es salaam

HIVI NDIVYO KOCHA WA YANGA ALIVYO WASILI USIKU HUU

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Brandts wa pili kutoka kulia, akiwa na viongozi wa Yanga. Kulia ni Seif Magari. Kushoto kwake ni Bin Kleb na Majjid


Anapakia mizigo kwenye gari la Bin Kleb


Anazungumza na Waandishi wa Habari


Akiwa na viongozi wa Yanga


Kulia kwake Bin Klerb, kushoto Mwalusako


Anatoka Uwanja wa Ndege

Millionfortune Dar es salaam,
KOCHA mpya wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, beki wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya Holanzi, amewasili usiku huu (saa 3:45) katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na ndege ya KLM tayari kusaini mkataba na kuanza kazi katika klabu hiyo.
Brandts amepokewa na Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako na viongozi wengine, Abdallah Ahmad Bin Kleb, Seif Ahmad ‘Magari’ na Majjid Suleiman na amesema anaijua Yanga ni timu nzuri, kubwa hana shaka ataiwezesha kufanya vizuri katika medani ya soka Afrika.
Yanga, imetimiza malengo yake ya kuwa kocha mpya, kabla ya kucheza na wapinzani wao wa jadi, Simba SC, Oktoba 3, mwaka huu baada ya kumfukuza Mbelgiji, Tom Saintfiet, kutokana na kuwasili makubaliano na Brandts, ambaye ataanza kazi mara moja kesho.
Mholanzi huyo aliyefukuzwa APR ya Rwanda baada ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Agosti mwaka huu amepewa ukocha wa Yanga, baada ya Mbrazil Marcio Maximo kukataa nafasi hiyo kwa mara ya pili.
Mtaalamu huyo, alizaliwa Februari 3, mwaka 1956 mjini Nieuw-Dijk, Gelderland, mbali na PSV Eindhoven, alichezea pia Roda JC Kerkrade, MVV Maastricht na De Graafschap.
Brandts aliichezea mechi 28 timu ya taifa ya Uholanzi na kuifungia mabao matano na pia alicheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1978.
Katika fainali hizo, Raundi ya pili kwenye mechi na Italia, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyezifungia mabao timu zote katika mechi moja kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Alianza kujifunga dakika ya 18, kisha akaisawazishia Uholanzi dakika ya 50 katika mechi ambayo, mchezaji mwenzake Arie Haan baadaye aliifungia timu yake bao la ushindi na kutoka kifua mbele kwa mabao 2–1.
Alipostaafu soka akawa kocha na katikati ya msimu wa 2007–2008, Brandts aliambiwa hataongezewa mkataba NAC-Breda, licha ya matokeo mazuri ya kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie), ingawa uamuzi huo haukuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo na nafasi yake akapewa Robert Maaskant kuanzia msimu wa 2008–2009.
Akateuliwa kuwa Kocha wa Rah Ahan mwaka 2009, kabla ya kufukuzwa Desemba 2009 na kuibukia APR ya Rwanda mwaka 2010, ambako ‘riziki’ yake imeisha miezi miwili iliyopita na sasa amepata maisha mapya Yanga.
Akiwa APR, Brandts alifungwa mechi zote mbili na Yanga iliyokuwa ikifundishwa na Mbelgiji Tom Saintfiet katika Kombe la Kagame, moja ya makundi 2-0 na nyingine ya Nusu Fainali 1-0. Yanga iliibuka bingwa, ikiifunga Azam FC 2-0 kwenye fainali.
Brandts atakutana na wachezaji wake wa zamani wawili Yanga, beki Mbuyu Twite anayeanza msimu wa kwanza katika klabu hiyo na kiungo Haruna Niyonzima anayeingia katika msimu wa pili, ambao alifanya nao kazi APR.

September 28, 2012

HIVI NDIVYO HALI ILIVYO KWA SASA BAADA YA WAMACHINGA KUVAMIA ENEO LA MTU KILOMBERO ARUSHA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



Wafanyabiasha wadogowadogo maarufu kama wamachinga ambao walivamia  maaneo ya kufanyia biashara, katika eneo la stendi ya zamani ya Kilombero. Wamachinga hao bado mpaka mchana huu wameonekana wakitapakaa maeneo hayo licha ya kuzuiwa na vyombo husika mpaka muafaka utakapopatikana kuhusu eneo watalopewa kufanyia biashara zao rasmi.

MSHIKAMANO WAHITAJIKA BAINA YA NCHI ZILIZOENDELEA NA NCHI MASKINI ILI KUMSAIDIA MTOTO WA KIKE KIELIMU

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mama Kikwete (kulia) akiwa mkutanoni New York nchini Marekani
Na Anna Nkinda – Maelezo, New York
MSHIKAMANO wa pamoja unahitajika baina ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea ili kuhakikisha mtoto wa kike ambaye hajapata nafasi ya kwenda shule anapata elimu, kuwainua wanawake kiuchumi na kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto vinavyotokana na tatizo la uzazi na ugonjwa wa kansa.
Hayo yamesemwa jana na Mke wa rais Mama Salma Kikwete wakati akichangia mada kwenye mkutano wa The RAND African First Ladies Initiative uliofanyika makao Makuu ya Taasisi ya Ford mjini New York nchini Marekani.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za kiserikali zinafanya jitihada kubwa ya kuhakikisha kuwa zinawasaidia wanawake wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha tatizo lililopo ni upungufu wa rasilimai fedha za kuweza kukabiliana na changamoto hizo hivyo basi ushirikiano wa pamoja unahitajika ili kuweza kufanikisha malengo hayo.
Aliendelea kusema kuwa watoto wa kike wakipata elimu ya kutosha watakuwa na silaha muhimu katika maisha yao ya kuweza kupambana na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na maradhi, ujinga na umaskini kwani elimu ni nguzo muhimu katika maendeleo ya taifa lolote Duniani bila ya watu kuwa na na elimu nchi haiwezi kuendelea.
“Ukimuelimisha mtoto hasa mtoto wa kike ambaye amekosa nafasi ya kupata elimu ni faida kwa mtoto, Taifa na Dunia kwa ujumla kwani hivi sasa tumejionea wanawake wengi wakishika nafasi za juu za uongozi kitaifa na Dunia pia wameweza kujikwamua kiuchumi tofauti na miaka ya nyuma”, alisema Mama Kikwete.
Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya WAMA alisema kuwa nchini Tanzania watoto wengi wa kike ambao ni yatima na wanaishi katika mazingira hatarishi wameshindwa kupata elimu sawa na watoto wengine hivyo basi aliamua kuanzisha taasisi hiyo ili aweze kuwasaidia watoto hao, kuwainua wanawake kiuchumi na kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto na wanaougua ugonjwa wa kansa kwa kutoa elimu kwa wananchi na vifaa tiba katika vituo vya afya na Hospitali .
Mkutano huo wa siku moja ulihudhuriwa na wake wa marais na wakuu wa Serikali wa Afrika, mke wa rais mstaafu wa Marekani Laura Bush na mke wa waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Cherie Blair, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na mashirika binafsi kutoka nchi wa Afrika na Marekani.
Katika mkutano huo mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na kuangalia jinsi gani wake wa maraisi na wakuu wa Serikali wanaweza kuleta mabadiliko katika nchi zao katika kuimarisha afya ya mwanamke, kuhakikisha kuwa mtoto wa kike anapata elimu na na kuwainua wanawake kiuchumi pamoja na changamoto wanazoweza kukabiliana nazo

WASANII WA SANAA MAONESHO WAPEWA CHANGAMOTO BAGAMOYO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Baadhi ya sanamu zilizochongwa na wasanii.

WASANII wa sanaa za maonesho nchini wamepewa changamoto ya kutambua kuwa watalii ni hadhira ambayo wanaweza kuilenga katika ubunifu wa kazi zao ili kukuza utalii wa kiutamaduni, ambao utasaidia kuongeza mapato kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TAsuBA), Juma Bakari wakati akiwalisisha mada ya ‘Sanaa za Maonesho kama Kivutio cha Utalii Tanzania’ kwenye Kongamano la Tamasha la 31 la Sanaa na Utamaduni lililofanyika Uwanja wa Taasisi hiyo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.

Alisema sanaa za maonesho ni kivutio kikubwa cha utalii hivyo kuna kila sababu ya wasanii kuwa na mtazamo huo ili kuangalia fursa zilizopo. Alisema wasanii lazima watambue watalii ni hadhira ambayo wanaweza kuwalenga kwa kuwafahamu kwa makundi.

Alitolea mfano kuwa katika kipindi cha mwaka 2005 sekta ya utalii imeingiza mapato makubwa na imekuwa chanzo cha mapato ya fedha za kigeni,ambapo nchi yetu ilipata dola za Marekani bilioni 1.8 na inatarajia kupata dola za Marekani bilioni tatu ifikapo mwaka 2015.

Aliongeza kuwa ni vizuri wasanii hao wakajifunza kutoka kwa wenzao wa Kenya na Uganda ambao wamefanikiwa kuhamasisha utalii huo kwa kutumia ngoma na muziki wa asili. Mkuu huyo wa taasisi hiyo alisema Lugha ya Kiswahili inaweza kuwa ni kivutio cha watalii ikiwa wasanii hao watatayarisha tamthilia za lugha kwa maneno mepesi.

Akizungumzia kuhusu changamoto zinazowakabili katika kukuza utalii huo, alisema zaidi ya vikundi 4000 vilivyosajiliwa, hakuna hata kimoja kinachoonyesha kukuza utalii huo. Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa elimu ya biashara na ujasiriamali hali inayosababisha vikundi vingi kutegemea wafadhili hatimaye kuanzishwa halafu vinakuwa havipo.

Aidha alifafanua kuwa kampuni za kitalii nazo zinachangia kutokuza utalii huo kwa kuwa kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Maliasili za mwaka 2011-2012 kampuni hizo ziko 385, kati ya hizo 85 ni za kigeni . Pia kulingana na utafiti uliofanywa hata zilizobakia zinaendeshwa na wageni ambao sio jambo rahisi kwa wao kuukuza kwa vile hawaufahamu.

Taarifa Muhimu kwa Umma Kutoka Wizara ya maliasili na utalii

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Na: Tulizo Kilaga

Wizara ya Maliasili na Utalii itawachukulia hatua wale wote watakaokiuka sheria, kanuni na taratibu zinazotawala utekelezaji wa mchakato wa kuwapata wawekezaji kwenye vitalu vilivyopo kwenye Maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori (WMAs).


Akifungua warsha ya mafunzo kuhusu mchakato wa kufungua maombi ya uwekezaji kwenye vitalu vya WMAs iliyofanyika katika Ukumbi wa Blue Peel jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Bw. Paul Sarakikya alisema mchakato husika utahusisha watu wenye uwezo wa fedha hivyo unaweza kusababisha uwepo wa mazingira ya rushwa.

Alisema mchakato huo ni nyeti na unahitaji uadilifu na umakini mkubwa katika kuutekeleza. Kushindwa kuzingatia vigezo vitakavyokubalika katika mchakato huo kutasababisha migogoro isiyo ya lazima hivyo kudhoofisha maendeleo ya Jumuiya na kukatisha tamaa vijiji vilivyotenga maeneo kuanzisha WMAs. “Napenda kusisitiza kuwa, Kanuni za WMAs zinazitaka Jumuiya kufanya uteuzi wa wawekezaji kwa kutumia vigezo vilevile vilivyotumiwa na Wizara kuwapata wawekezaji kwa kutumia vigezo vilivile vilivyotumiwa na Wizara kuwapata wawekezaji kwenye vitalu vyake.

Vigezo hivyo viko kwenye Kanuni za Uwindaji wa Kitalii (2010) kifungu cha 10(2). Hivyo washiriki watapata fursa ya kuvipitia na kuviwekea alama kwa kuzingatia mahitaji na hali halisi ya WMAs, alisema Bw. Sarakikya.Aliongeza kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii itashirikiana na vyombo vya dola kufuatilia utekelezaji wa mchakato huu na haitasita kuwachukulia hatua wale wote walioshindwa kuweka mbele maslahi ya Jumuiya zao na ya Taifa kwa Ujumla,” alisema Bw. Sarakikya. Bw. Sarakikya alisema kwa kutambua umuhimu wa mchakato wa ugawaji vitalu hivyo Wizara ya Maliasli na Utalii imetoa Afisa kutoka Kitengo cha Matumizi Endelevu ya Wanyamapori ili kutoa mafunzo. Hivyo Wizara inatarajia wajumbe wote watakubalina na kuhitimisha hatua za kimchakato zitakazotumika, na hatimaye kuwa na mwongozo utakaotumika na Kamati zitakazo fungua maombi hayo.


Warsha ya Mafunzo kuhusu Mchakato wa Kufungua maombi ya uwekezaji kwenye vitalu kwenye maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori imelenga kuwawezesha wajumbe kupata uelewa wa pamoja wa nini cha kufanya baada ya Jumuiya zilizo nyingi kuwa zimepokea maombi ya uwekezaji kwanye vitalu vya WMAs kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 na Kanuni za WMAs 2012.

BREAKING NEWS: KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA, NI BEKI WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA UHOLANZI ALIYEWEKA REKODI KOMBE LA DUNIA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends





Brandts kulia akiwa na Saintfiet wakati wa Kagame

Na Mahmoud Zubeiry
BEKI wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya Holanzi, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, ndiye kocha mpya wa Yanga na atawasili wakati wowote kuanzia kesho kusaini mkataba na kuanza kazi.
Mholanzi huyo aliyefukuzwa APR ya Rwanda baada ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Agosti mwaka huu amepewa ukocha wa Yanga, baada ya Mbrazil Marcio Maximo kukataa nafasi hiyo kwa mara ya pili.
Mtaalamu huyo, alizaliwa Februari 3, mwaka 1956 mjini Nieuw-Dijk, Gelderland, mbali na PSV Eindhoven, alichezea pia Roda JC Kerkrade, MVV Maastricht na De Graafschap.

TAZAMA SOKO LA KILOMBERO ARUSHA PALIVYOCHAFUKA KWA MABOOM NA MOTO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Wamachinga zaidi ya mia mbili katika eneo la soko la kilombero mkoani Arusha walivamia eneo lililokuwa na uzio na kuvunjwa uzio huo na kuingia katika eneo hilo na kung'oa mabati na miti iliyokuwepo katika eneo hilo na kucanza kuchoma moto. Kwa maelezo ya wamachinga hao wanadai kwamba lilikuwa ni eneo la wazi kwa muda mrefu lakini baadaye eneo hilo likauzwa na madiwani bila kushirikisha serikali ya mtaa, kesi ikapelekwa mahakamani na ayeuziwa eneo hilo akasimamishwa kujenga na kesi ipo mahakamani, Jana asubuhi wafabiashara ndondogo maarufu kama wamachinga waliamua kuvunja uzio wa eneo hilo na kujigawia eneo hilo na polisi walikuja wakawa wanaangalia tuu baada ya kuona wingi wa wamachinga hao. Lakini baadae askari waliongezeka na kuanza kupiga mabomu ya machozi ili kuwasambaratisaha wamachinga hao....


Hali inavyoonekana kwa sasa Eneo la kilombero jijini arusha wananchi waamua kuchoma matairi
Wabomoa uzio wa eneo hilo lililokuwa limezungushiwa mabati

 Fire wamesha fika kwa ajili ya kudhibiti madhara yoyote ya moto

 Lilifika Gari moja kwanza

Polisi wakiwa eneo la tukio
Sasa Yamekuwa matatu na yote yamejaa FFU kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi..

MH. ZITTO KABWE ATANGAZA KUTOGOMBEA TENA UBUNGE BADALA YAKE ATAGOMBEA URAIS MWAKA 2015

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais.


Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma.


Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.

“Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi.


“Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.


“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu.


“Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.”

Atangaza kugombea urais


Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

“Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea.

Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya.”


“Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,” alisema Zitto


Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46.

Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa.


“Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.

“CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto.


Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat