StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

Showing posts with label MCHANGANYIKO. Show all posts
Showing posts with label MCHANGANYIKO. Show all posts

September 22, 2012

TANZANIA NA MAGAZETI YA JUMAMOSI YA LEO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends














September 21, 2012

HUYU NDIYE MSHITAKIWA ALIYETAPELI KAMPUNI KWA KUTUMIA JINA LA DR. ASHA ROSE MIGIRO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Mshitakiwa katika kesi ya utapeli dhidi ya Kampuni ya wakala wa kupakia na kupakua mizigo bandarini ya Mokha Agency Co. Ltd ya Dar es Salaam, aliyedaiwa kutumia jina la aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk Asha-Rose Migiro, Sharifa Kalala (nyuma) akiongozwa na askari wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam kwenda kupanda karandinga baada ya kusomewa mashitaka mahakamani hapo jana.

September 20, 2012

BEYONCE NA JAY-Z WAKUSANYA DOLA MILLION 4 KWAAJILI YA OBAMA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

After an appearance on the Late Show With David Letterman in New York on Tuesday, President Barack Obama picked up a cool $4 million at a fundraiser hosted by Jay-Z and Beyoncé at the 40/40 Club.

One hundred donors in suits and dresses sat on sofas in a large, dark glassy room at Jay-Z's exclusive club, according to a pool report. Each paid $40,000 to attend the event.

"I can't tell you how proud we are to host tonight's event with President Obama," Beyoncé, wearing a red cocktail dress, told the crowd. "We believe in his vision."

Obama thanked them when he took the stage. "To J and B, thank you so much for your friendship."

The president told the crowd that "Michelle, Sasha and Malia are mad at me because they aren't here."

He said the couple has been so generous to his children: "Beyoncé couldn't be a better role model for our daughters because she carries herself with such class and poise and has so much talent."

Obama also said he and Jay-Z have a lot of common. "We both have daughters and our wives are more popular than we are. So, you know, we've got a little bond there. It's hard but it's okay."

HUYU NDIYE RISHED BADE ALIYETEULIWA NA RAIS JK KUWA NAIBU KAMISHNA MKUU WA TRA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished Bade (pichani), kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Taarifa iliyotolewa Jumatano, Septemba 19, 2012 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais - Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo umeanza Jumatatu wiki hii, Septemba 17, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Bade alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Mortgage Finance Co. Ltd.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Septemba, 2012

September 19, 2012

MITAMBO YA TAHADHARI YA VYOMBO VYA USAFIRI BAHARINI TAYARI KWA MAJARIBIO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Usizame logo 
Usizame inafuraha kuwatangazia kuwa mitambo yake ya ufumbuzi ya kutumia ujumbe mfupi wa SMS za bure kwa wasafiri wanaotumia vyombo vya usafiri vya baharini Tanzania vipo tayari kwa majaribio.

Kikosi cha Usizame kitafanya majaribio ya mitambo yake iliotengezwa kwa ufundi mkubwa na wataalamu wakujitolea wanaotumia maandishi maalum ambayo ambayo yataweza kuchanganywa na ujumbe mfupi wa SMS. Na baadae mitambo hiyo itafanya maribio yak echini ya kiwango kidogo katika hatua za awalai na majaribio hayo yatakuwa baina ya Unguja, Pemba na Dar es Salaam.

Umuhimu wa kuwajuvya watu kwa kupitia vipeperushi na kupitia kwenye vyombo vyengine vya habari kama vile redio na TV, hali kadhalika tutawashuru wale wote watakaotoa msaada wao katika kuwafikishia watu ujumbe huu.

Mpango huu umesarifiwa kwa ajili ya kukuza usalama wa abiria baada ya ajali mbili mbaya za baharini uliotokea chini ya mwaka mmoja, ajali ambazo zimepelekea vifo vya watu wengi. Mpangilio wa utaratibu huu utawezesha kuweka vifaa kwenye vyombo vya baharini ambavyo vitapelekea abiria kwa umoja wao kuhakikisha chombo wanachosafiria kipo tayari kwa safari za baharini.



Picha za majaribio kwa toleo hili zipo tayari kwenye database ya Usizame.

Usizame pia imekwisha maliza kazi ya kusarifu mtandao wake na tayari kwa matumizi kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea mtandao ili kuona vipi mitambo hiyo ifanyavyo kazi, na pia kujua kazi zilizofanyika katika mradi huu.



Kwa sasa mitambo hii inaweza kutumia ujumbe mfupi wa maandishi wa SMS utakaoweza kuandikisha abiria watakaokuwa wanasafiri na pia kuweza kuwajuulisha wenyewe kuwa wamesajiliwa kama wasafiri kwa wakati huo. Mara tu hatua nyengine ya mitambo hii itakapokamilika, taarifa zitatolewa kwa jamii nzima kwa ujumla.

Hivyo tunawasisitiza watu wote kufikisha ujumbe huu kwa jamii nzima, na kila atakaeona ama kusoma matangazo haya kuwaarifu wenzao, marafiki, ndugu, wafanyakzi wenzako, mawakala wa usafiri, waendeshaji wa vituo vya utalii na nyumba za wageni. Vile vile tunawaomba wote kujiandikisha kwenye mtandao wetu ili kuweza kupokea taarifa zote kwa wakati Usizame ipo hewani. Na tuifanye bahari ni sehemu ya usalama ya usafiri.

KAMERA YETU KITAANI...

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Wakazi wa Dar es Salaam wakipita jirani na paa la kituo cha daladala cha Magomeni Mikumi lililoanguka. Toka jana...

JENERALI SAID SHAABAN AZINDUA MFUMO WA DORIA WA WANAMAJI JWTZ

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Meja Jenerali Saidi Shaaban Omar akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mfumo wa doria wa wanamaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kituo cha Wanamaji Kigamboni Dar es Salaam jana.


MH. RAIS KIKWETE KATIKA UZINDUZI WA UJENZI WA BARABARA YA BAGAMOYO-MSATA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Msata uliofanyika katika kijiji cha Kiwangwa wilayani Bagamoyo leo mchana.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Pwani ambaye pia ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik(Wapili kushoto),Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli(wanne kushoto) na kulia ni Waziri wa Mazingira Mhe. Theresa Hoviza.

Sehemu ya Barabara ya Bagamoyo Msata iliyojengwa kwa kiwangi cha lami ambayo ujenzi wake ulizinduliwa Rasmi(picha na Freddy Maro)

September 17, 2012

MAUAJI YA WANAWAKE WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA UKAHABA SASA NI 15, WATATU WAMEUWAWA USIKU WAKUAMKIA LEO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Rwanda Police publicist Theos Badege says investigations into the killings are underway


Polisi nchini Rwanda wanaendelea na uchunguzi wa mauaji ya wanawake wanaodhaniwa kujihisisha na biashara ya kuuza miili yao ambao mpaka sasa imefikia 15. Uchunguzi huo umechukua mtizamo mpya hasa baada ya mashirika ya kimataifa yanayohusika na haki za binadamu kuingilia kati.
Mmoja wa wakazi wa mji wa Kigali karibu na Nyumba za wageni wanamofanyia biashara hizo amezungumza haya na mdau wetu mjini kigali
"Wanawake hao wamekuwa wakiwaibia watu mali na fedha nyingi hivyo wanaume hao wanavinyongo, wanaume hao wengi unakuta wanawajua wanawake hao kwa sura lakini wao hawawajui kwani wanawateja wengi na hawawezi kuwakumbuka wote, hivyo wanaume hao wanapokuja kulipiza kisasi huja kama wateja wa kawaida na hapo ndipo huwaua wakiwa faragha"


Polisi mjini kigali inawashikilia watu watatu mpaka sasa kuhusiana na mauaji hayo yanayoendelea.

Ex-prostitutes sing and dance to religious songs in Muhanga district

SERIKALI YA KIJIJI YAAMURU KUTOLALA CHUMBA KIMOJA NA MAMA YAKE BAADA YA KUBAINIKA ANA UHUSIANO WA ...

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



Mwenyekiti wa kijiji cha Dilifu Pichani kata ya Itenka wilayani mlele mkoa wa katavi Elineo Mbaruku akitoa maelezo kwa mwandishi wa habari hizi kuhusiana na maamuzi ya uongozi wa kijiji hicho cha Dilifu kutoa uamuzi wa kumtenganisha kijana mmoja aliyejulikana kwa la Kwimba (28) kulala chumba kimoja na mama yake mzazi. uamuzi huo wa serikali ya kijiji umefuatia tuhuma za mama na mwanae kuwa na mahusiano ya kimapenzi mwenyekiti huyo wa kijiji alisema tayari kwimba ametii agizo hilo na amekwisha hama kwenye nyumba hiyo na amepanga chumba kijijini hapo.
Picha na Walter Mguluchuma- Katavi yetu Blog

PICHA NA MATUKIO YA YANAYOJIRI UCHAGUZI WA BUBUBU, KAMA KAWAIDA POLISI...

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Kumekuwa na vurugu za hapa na pale, Polisi kupambana na vijana kwenye kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi mdogo kumchagua Mwakilishi wa jimbo la Bububu Zanzibar leo. (pichani) Polisi wa kuzuia ghasia wakisaidiwa na kikosi cha Valantia kuwaondoa vijana waliojikusanya karibu na kituo cha kupigia kura kwenye Shule ya Bububu.


















Baadhi ya mawakala wa vyama wakifuatilia upigaji kura.

Kijana akitumbukiza kura yake kwenye kisanduku cha kupigia kura jwenye kituo cha Shule ya Bububu Zanzibar

Kiongozi wa chama cha siasa (kushoto) akizungumza na wandishi wa habari nje ya kituo cha kupigia kura.Picha zote na Martin Kabemba.

September 15, 2012

JK AZINDUA MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI DAR

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa anuani ya makazi ya Ikulu na Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijukawakati uzinduzi wa mfumo wa anuani Mpya za Makazi na nembo ya Simbo (Post code) uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

RIHANNA AKIFURAHI NA WANAFAMILIA UFUKWENI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Water babe: Rihanna holds on tight to her brother Rajad as they mess about in the water



She's the one: Rihanna finally got to enjoy some downtime, as she holidayed in Barbados and spent the day at the beach with her brother Rajad





Catch me if you can: Rihanna makes the most of her trip to Barbados as she played with her brother


Water fight: Rihanna and her brother battle with one another in the sea...


...they both end up crashing into the waves together



Family bonding: Rihanna very nearly had a wardrobe malfunction while cuddling her brother

HUYU NDIYE MWANDISHI AFUKUZWA UANACHAMA BAADA YA KUWASALITI WENZAKE.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

MUSOMA
CHAMA cha Waandishi wa Habari mkoani Mara MRPC, kimemfukuza uanachama wa chama hicho, mwandishi wa habari wa radio Free Afrika mkoani Mara Bw Maxmilian Ngesi baada ya kukiuka makubalino ya chama hicho yaliyofikiwa juzi ya kutoandika kabisa habari za jeshi la polisi mkoani humo.

Akizungumzia kufukuzwa kwa Mwandishi huyo mwenyekiti wa chama hicho Bw Emmanuel Bwimbo,alisema kuwa Ngesi amekiuka makubaliano ya waandishi wenzake na chama kwa ujumla baada ya kusikika akitangaza habari za jeshi la polisi kwa kumkariri kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara.

“ Sisi kwa kauli moja tumekubaliana kutofanya kazi na Jeshi la Polisi Mkoani Mara baada ya Matukio kadhaa likiwemo ya kuuawa kwa mwandishi wa habari mkoani Iringa na kutunyima kibali cha Maandamano yetu ya Amani kupinga Mauaji hayo” alisema Bw Bwimbo

Bw Bwimbo alisema kuwa kitendo hicho kinaonyesha jinsi gani mwandishi huyo alivyokiuka makubaliano ya pamoja na kuwasaliti wenzake ambao wamekubaliana kwa pamoja kuwa hawataandika habari za jeshi hilo kutokana na kuzuiwa waandishi kutoandamana katika maandamano ambayo yaliitishwa nchini kote kulaani kitendo cha mauaji ya mwandishi wa kituo cha chanel Ten mkoani Iringa Daud Mwangosi.

Alisema Ngesi kama mwanachama alitakiwa kutii maamuzi ya chama na tamko la chama chake kwa vile tamko hilo limewataka wananchama wote na siyo kwa mkoa wa Mara tu lakini pia baadhi ya mikoa imetoa matamko na misimamo hiyo lakini cha kushangaza yeye amekaidi na kwenda kinyume.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema kamwe chama hicho hakiwezi kuvumilia mwandishi atakaye kiuka agizo hilo na hatua ambayo imechukuliwa kwa Ngesi ni mfano kwa waandishi wengine hadi hapo tamko hilo litakapo tenguliwa.

Jumatatu wiki hii waandishi wa habari walifanya maandamano nchi nzima wakilaani mauaji ya mwandishi mwenzao Daudi Mwangosi ambapo kwa mkoa wa Mara maandamano hayo yaliuzuiwa na polisi hali iliyofanya chama cha waandishi wa habari kukataa kuandika habari za jeshi hilo mkoani Mara.

September 13, 2012

KWELI MAREHEMU HANA HAKI HEBU SOMA HABARI YA MTOTO HUYU WA DARASA LA 4 ALIYEGONGWA ILALA BOMA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Tarehe 23, august 2012 nilipost habari ya ajali mbaya iliyotokea eneo la ilala boma na kijana mmoja ambaye kwa wakati huo hatukuweza kupata jina lake aligongwa na kupasuliwa kichwa na lori na dereva wa lori hilo kukimbia. Mpaka wakati napost habari hiyo hatukuwa tumepata majina kamili ya kijana huyo aliyegongwa wala dereva. Huyo mtoto aliyegongwa anaitwa ABDULKARIM MOHAMED MDEE, alikuwa na miaka 11 mwanafunzi wa darasa la 4 katika shule ya msingi ILALA BOMA....baada ya kumgonga dereva wa roli alikimbia na kujisalimisha polisi na kesi yake imetajwa tarehe 3-9-2012 ambapo amehukumiwa kulipa faini 50000TSH au jela miezi 6. Shukrani za kipekee zikufikie popote ulipo Zennat Khamis.

Picha za tukio hilo hizi hapa chini (viewer discresion is advised)



Baadhi ya wananchi wakiwa wanaangalia mwili wa marehemu ambaye amepoteza maisha papo hapo mara baada ya kugongwa na lori na kukanyagwa kichwa na hatimaye kupelekea kichwa kupasuka na ubongo kumwagika chini leo majira ya saa tisa mchana eneo la ilala boma



Mwili wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ukiwa umefunikwa na kanga huku pembeni vipande vya ubongo wake vikiwa pembeni mara baada ya kugongwa na lori na kukanyangwa kichwa na kupelekea kichwa kupasuka na ubongo wote kumwagika chini leo majira ya saa tisa mchana eneo la Ilala Boma. Kijana huyu anasadikiwa kuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Saba katika shule ya Msingi Msimbazi.

Askari wa Usalama barabarani akisaidiana na baadhi ya wananchi kuubeba mwili wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ili kuupakia katika gari dogo tayari kuupeleka hospitali ya Amana.Kijana huyu anakadiriwa kuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi Msimbazi.


 Baadhi ya wananchi wakiutazama mwili wa marehemu ambaye amegongwa na gari na kupelekea kupasuka kichwa na kupoteza maisha papo hapo.


Mwili wa marehemu ukifunikwa vizuri kwaajili ya kupelekwa hospitali ya amana.Pembeni ya mwili wa marehemu ni vipande vya ubongo mara baada ya kukanyangwa na lori


September 11, 2012

HUYU NDIYE MCHINA ALIYETIWA MBARONI KWA KUCHIMBA MADINI KWENYE PORI LA AKIBA LA LWAFI WILAYANI NKASI.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mtambo wa kuchimbia madini ambao Raia wa China walikamatwa wakiutumia katika pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkansi kinyume cha sheria.Raia huyu wa china amehukumiwa kulipa faini na kuamriwa kuondoa mtambo huo katika pori hilo.

Baadhi ya raia wa China na Watanzania wakishirikiana kuchimba madini katika pori la Akiba la Lwafi,wilayani Nkansi kinyume cha sheria,ambapo raia hao wa china walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kulipa faini.Picha naTabu Ndziku


Mkurugenzi wa Kampuni ya REDore Mining mwenye asili ya Asia Chaoxian Zhou amehukumiwa kwenda jela miaka minne au kulipa faini jumla ya Shilingi 1,350,000/= kwa kukutwa na makosa mbalimbali likiwemo lakuchimba madini ndani ya hifadhi ya Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi kinyume cha sheria .

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama pori Paul Sarakikya, mtuhumiwa amelipa faini na kuachiwa huru.Makosa megine aliyopatikana nayo ni pamoja na kuingia ndani ya Pori la Akiba Lwafi kinyume na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009 kifungu cha 15 na kuharibu mimea ndani ya Pori la Akiba kwa kukiuka kifungu cha 18 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori.

Makosa mengine ni pamoja na kuchimba madini ndani ya Pori la Akiba bila kibali kinyume na Kifungu cha 20 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori na kuchimba madini ndani ya hifadhi kinyume na kifungu cha 95(1) (c) cha Sheria ya madini Na. 14 ya mwaka 2010.

Mshtakiwa alikiri makosa yote mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Richard Kasele na Mwendesha Mashtaka Bwana Prosper Rwegerera na kupatikana na hatia ya kuchimba madini katika eneo la Kanyamakaa lililoko katika Wilaya ya Nkasi kinyume cha sheria ya Kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mshitakiwa ameamriwa kuondoa mitambo iliyokutwa ndani ya Pori la Akiba la Lwafi na kufukia mashimo na mitaro yote iliyochimbwa kutokana na shughuli za Kampuni hiyo ndani ya siku saba. Aidha Madini yaliyokuwa yamechimbwa katika eneo hilo ambayo thamani yake bado haijajulikana yametaifishwa na Serikali.

Chaoxian Zhou na mwenzake Wei Lyu ambao wote ni raia wa China walikamtwa Julai 25, 2012 ambapo iligundulika kuwa Wei Lyu hakuwahi kwenda mkoani Katavi wala katika Hifadhi hiyo ya Lwafi na kuchimba madini hivyo aliachiwa huru.

September 8, 2012

KUTOKA SRI-LANKA: SPIKA ANNE MAKINDA AHUDHURIA MKUTANO WA 58 WA CPA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Ndg. Dimitries Mgalami akimsindikiza Mhe. Spika katika hotel itakayofikia wakati wote wa Mkutano huo wa CPA.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda amewasili Mjini Colombo nchini Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola Dunian (CPA). Mkutano huo wa mwaka unafanyika Nchini humo kuanzaia tarehe 7 hadi 15 Septemba, 2012, ambapo zaidi ya wabunge 1000 na Maspika wa Mabunge zaidi ya 80 kutoka nchi mbalimbali wananchama wa jumuiya ya Madola watahudhuria mkutano huo wa mwaka.


Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo unaongozwa na Mhe. Spika ambaye pia ataongoza wabunge wengine kutoka tawi la CPA Tanzania ambo ni Mhe. Ziito Kabwe, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mhe. Beatriace Shelukindo, Mhe. Hamad Rashid Mohamad na Mhe. Muhonga Ruhanya ambapo jumla ya mada 9 zinatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo.

kamimu Katibu wa CPA kanda ya Afrika na Mkuu wa Sehemu ya Itifaki na uhusiano wa Kimataifa kutoka Bunge la Tanzania Ndg. Dimitries Mgalami akiteta jambo na Mhe. Spika mara baada ya kumpokea alipowasili Colombo Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa mwaka wa CPA unaofanyika Nchini humo kuanzaia tarehe 7 hadi 15 Septemba, 2012.

Mjumbe wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Zitto Kabwe akiteta jambo na Mhe. Okupa Elijah kutoka Bunge la Uganda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege colombo Sri lanka kuhudhuria mkutano wa 58 wa CPA. aliyeko pembeni ni Mbunge kutoka Uingereza.Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat