StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 19, 2012

DUH, MKOA WA ARUSHA NDIO UNAOONGOZA KATIKA WIZI NA UDANGANYIFU KATIKA MITIHANI YA KITAIFA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends  

Mkoa wa Arusha umetajwa kuwa umeongoza katika udanganyifu na wizi wa mitihani kwa asilimia 48 kati ya asilimia 61 ya wanachama 31 wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa shule za msingi.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa shule na Vyuo visivyo vya Serikali (Tamongsco), Benjamin Nkonya, alitoa kauli hiyo jana kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Alisema wizi wa mitihani ni saratani inayotafuna ubora wa elimu nchini, kamwe hali hiyo ikiendelea upo uwezekano wa Taifa kutumbukia kwenye umaskini wa kukosa uelewa na kushindwa kupata maendeleo ya kweli ya kiuchumi.

Nkonya alisema Tamongsco ina uhakika kwamba maendeleo ya kweli ya uchumi yanapatikana kwa kuboresha elimu, lakini kwa udanganyifu uliojitokeza wa mitihani ni ndoto maendeleo hayo kupatikana.

“Wizara ya elimu imetuarifu rasmi kuwa Mkoa wa Arusha ni kinara wa wizi na udanganyifu wa mitihani, ukifuatiwa na Kagera kwa asilimia 13, Dar es Salaam na Mara asilimia sita na mikoa mingine uliyobaki ina asilimia 3 kila mmoja,” alisema.

CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat