Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Ndg. Dimitries Mgalami akimsindikiza Mhe. Spika katika hotel itakayofikia wakati wote wa Mkutano huo wa CPA.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda amewasili Mjini Colombo nchini Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola Dunian (CPA). Mkutano huo wa mwaka unafanyika Nchini humo kuanzaia tarehe 7 hadi 15 Septemba, 2012, ambapo zaidi ya wabunge 1000 na Maspika wa Mabunge zaidi ya 80 kutoka nchi mbalimbali wananchama wa jumuiya ya Madola watahudhuria mkutano huo wa mwaka.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo unaongozwa na Mhe. Spika ambaye pia ataongoza wabunge wengine kutoka tawi la CPA Tanzania ambo ni Mhe. Ziito Kabwe, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mhe. Beatriace Shelukindo, Mhe. Hamad Rashid Mohamad na Mhe. Muhonga Ruhanya ambapo jumla ya mada 9 zinatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo.
kamimu Katibu wa CPA kanda ya Afrika na Mkuu wa Sehemu ya Itifaki na uhusiano wa Kimataifa kutoka Bunge la Tanzania Ndg. Dimitries Mgalami akiteta jambo na Mhe. Spika mara baada ya kumpokea alipowasili Colombo Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa mwaka wa CPA unaofanyika Nchini humo kuanzaia tarehe 7 hadi 15 Septemba, 2012.
Mjumbe wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Zitto Kabwe akiteta jambo na Mhe. Okupa Elijah kutoka Bunge la Uganda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege colombo Sri lanka kuhudhuria mkutano wa 58 wa CPA. aliyeko pembeni ni Mbunge kutoka Uingereza.Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge.
September 8, 2012
KUTOKA SRI-LANKA: SPIKA ANNE MAKINDA AHUDHURIA MKUTANO WA 58 WA CPA
Millionfortune.com
MCHANGANYIKO,
SIASA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!