Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
DIDIER Drogba anaweza kufanya uhamisho wa kushangaza kuhamia
Barcelona ya Hispania ikiwa ni muda mfupi tangu kusaini mkataba wa
kuichezea timu ya Shangha Shenhua ya China.
Nyota huyo wa Ivory
Coast, aliachana na klabu yake ya Chelsea aliyoiwezesha kutwaa taji la
Klabu Bingwa Ulaya na kuamua kwenda China.
Alitarajia kwenda mjini
Barcelona kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Wakurugenzi wa klabu hiyo.
Mazungumzo hayo yalipangwa kufanyika Jumanne wiki hii.
Drogba (34) alitarajia kulipwa mshahara wa pauni 200,000 (Sh483 Milioni) kwa wiki na klabu hiyo ya China.
Aliposaini
alisema: "Nathibitisha nimesaini kucheza klabu ya Shanghai Shenhua ya
China kwa miaka miwili na nusu. Nitarejea kujiunga na klabu Julai.
"Nimetafakari
ofa zote nilizopewa wiki kadhaa zilizopita, lakini nadhani Shanghai
Shenhua ni sehemu sahihi kwangu kwenda kwa muda huu.
"Najiandaa
kukutana na changamoto mpya na kujifunza utamaduni mpya pia. Lakini pia
nafurahia kusikia maendeleo ya Ligi Kuu China.
"Chelsea
ilipokwenda China mwaka jana, tulikuwa na fursa nzuri na mashabiki
walitufurahia. Natarajia kuitangaza ligi ya China duniani kote," alisema
Drogba.