Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
KOCHA Roy Hodgson amesema mshambuliaji wake, Wayne Rooney alishindwa
kutimiza matarajio ya mashabiki wa England kwa sababu hakuwa fiti,
lakini akasisitiza hali hiyo siyo sababu kubwa ya England kutolewa
kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya.
Hodgson alisema
alifahamu matarajio ya wengi kutaka kumuona Rooney akicheza kwenye
kiwango cha juu baada ya kushindwa kucheza mechi mbili za kwanza
kutokana na kukabiliwa na adhabu aliyopewa kwa kosa alilofanya Oktoba
mwaka jana, kwenye mchezo dhidi ya Montenegro.
Lakini baada ya
kufunga bao la ushindi dhidi ya Ukraine, Rooney alikuwa chini ya kiwango
kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Italia na kufungwa kwa mikwaju
ya penalti 4-2 baada ya dakika 120 za mchezo uliomalizika bila kufungana
mjini Keiv.
Hodgson alisema: "Tatizo tuliweka matarajio mengi kwa Wayne.
"Alipokosa michezo miwili ya kwanza, tuliamini mchezo wa tatu, Wayne Rooney atatupeleka kwenye ubingwa.
"Nadhani
matarajio yalikuwa zaidi ya uwezo wake pamoja na kwamba alijitahidi.
Hakucheza kwenye kiwango chake. Nadhani hata yeye atakiri hali hiyo."
Aliongeza:
"Tuweke matumaini makubwa kwa Rooney? Sawa nakubali, lakini timu
zingine zina wachezaji pia, si ndiyo? "Nadhani kama (Andrea) Pirlo
angecheza vibaya usiku ule, angegharimu kiwango kilichoonyeshwa na
Italia."
"Nafikiri timu zote kubwa kuna wachezaji wawili, au watatu ambao kila mmoja anawatambua kwa michango yao kwenye timu.
"Unapokuwa
kwenye mashindano unategemea wachezaji hao wataonyesha kiwango
kuthibitisha ubora wao kama ilivyowahi kutokea kwa Maradona
aliyeiwezesha Argentina kutwaa ubingwa wa dunia."
Rooney alikwenda
mapumziko Las Vegas, Marekani mara baada ya ligi ya England kumalizika
na alipigwa picha akijirusha kwenye klabu ya usiku mida ya alfajiri.