Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
MABINGWA wa Kombe la Kagame, Yanga ya jijini Dar es Salaam,
watamtangaza kocha wao mpya Ijumaa wiki hii, ambapo ataanza kazi rasmi
mara baada ya michuano ya Kombe la Kagame baadaye mwezi ujao.
Kwa
maana hiyo, Kocha Msaidizi, Fred Minziro ndiye atakayeketi kwenye benchi
na kuiongoza timu hiyo inayovaa jezi za rangi ya njano na kijani
kutetea taji hilo.
Awali, Yanga ilibainisha kuwa inasaka kocha
mwenye uzoefu na soka la Afrika pamoja na mazingira yake kama ilivyokuwa
kwa kocha aliyeondoka, Kostadin Papic raia wa Serbia.
Kiongozi wa
usajili wa Yanga, Seif Ahmed alithibitisha kuwa kocha toka Ubelgiji, Tom
Saintfiet ni miongoni mwa wawili wenye nafasi kubwa kutua Jangwani.
Na
kwa upande wa Katibu wa Yanga, Selestine Mwesigwa ambaye ndiye Mtendaji
Mkuu wa klabu hiyo kwa sasa, alisema kuwa majina ya makocha watatu
yameshapitishwa.
"Kulikuwa na maombi ya makocha 25, baada ya mchujo
tumechagua makocha watatu ambao tunawachuja na kumtangaza mmoja wiki
hii," alisema.
Alisema timu inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa
Kaunda tayari kwa maandalizi ya michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza
Julai 14 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakati
huohuo, Kelvin Yondani aliyejiunga Yanga toka Simba, amesema katika
kipindi kifupi alichofanya mazoezi klabu yake hiyo mpya, amebaini kuwa
hakufanya makosa kutua Jangwani.
Yondani alisema kuwa, maisha ya
Jangwani ni mazuri hasa ukizingatia kuwa amepata mapokezi na ushirikiano
mzuri na wachezaji na viongozi.
Pia ametumia fursa hiyo kuitaka
Simba kumsahau kwani yeye tayari ni mali ya Yanga na hakuna jitihada
zozote za kujaribu kumrudhisha Simba zitakazofanikiwa.
Uhamisho wa
Yondani ulizua utata mkubwa baada ya klabu yake ya zamani kudai ni
mchezaji wao halali, huku Yanga na mchezaji wenyewe wakisema tofauti.
"Sifahamu
kwanini Simba bado wanazungumza mambo haya. Mimi nimeshamaliza kila
kitu na Yanga, ni vizuri wakaniacha nifanye kazi Yanga," alisema
Yondani.