Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
KIKOSI cha timu ya Taifa Hispania, kinaongoza orodha ya timu za taifa
zinazoundwa na wachezaji bora na wenye thamani kubwa katika fainali za
Kombe la Mataifa ya Ulaya zinazoendelea nchini Poland na Ukraine.
Wachezaji
23 wanaounda kikosi hicho kilichotinga hatua ya nusu fainali, kina
thamani ya pauni 579.7 milioni (Sh1.4 Trilioni), ambazo ni sawa na
bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kwa kipindi cha miaka
31.
Kwa kipindi cha mwaka 2010/2011, wizara hiyo ilitengewa fungu
la Sh18.7 Bilioni, ambazo kati ya hizo, Sh14.2 Bilioni zilikuwa kwa
ajili ya matumizi na Sh4.4 Bilioni zilitengwa kwa ajili miradi ya
Maendeleo.
Thamani ya kikosi hicho ni sawa pia na bajeti ya mwaka
mzima ya Wizara ya Elimu, ambayo ni Sh1.2 Trilioni bila kubadilika kwa
viwango vya kubadilisha pesa za kigeni.
Katika taarifa yake,
Transfermarkt imetoa mchanganuo unaoonyesha wastani wa thamani ya kila
mchezaji, ambayo ni pauni 25.2 milioni (Sh60.2 Bilioni), isipokuwa
Andres Iniesta, ambaye peke yake ametajwa kuwa na thamani ya pauni 57
milioni (Sh137 Bilioni), sawa na bajeti ya mwaka mzima ya Wizara ya
Mambo ya Nje.
Hata hivyo thamani ya Iniesta (28), haina mjumuisho
na ada ya uhamisho kwa vile yuko Barcelona kwa miaka 16. Cristiano
Ronaldo wa Ureno ndiye mchezaji mwenye thamani kubwa kuliko wote Euro
2012, akitajwa kuwa na thamani ya Sh191.1 Bilioni.
Kikosi cha
Ujerumani kiko nafasi ya pili kikiwa thamani ya Sh977.6 Bilioni, huku
kila mchezaji akiwa na wastani ya Sh42.2 bilioni.
England
inafuatia Sh 834.8 Bilioni na wastani wa thamani ya kila mchezaji Sh36.2
Bilioni, Ufaransa Sh723.5 na Ureno Sh716.2 Bilioni. Wastani wa thamani
ya kila mchezaji Sh31.2 Bilioni.
Katika orodha ya 5-bora, timu
tatu zimevuka kucheza hatua ya nusu fainali, ambazo ni Ujerumani, Ureno
na Hispania, huku Ufaransa na England zikiishia hatua ya robo fainali.
June 27, 2012
Kikosi cha timu ya Taifa Hispania bajeti ya Wizara Michezo miaka 31
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget