Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi-Zanzibar
Jeshi
la Polisi Zanzibar linawashikilia wafanyakazi sita wa meli ya MV Skagit
akiwemo mmiliki wake Bw. Said Abdulrahman pamoja na Nahodha wa meli
hiyo Bw. Mussa Makame Mussa na wanahojiwa kufuatia tukio la ajali ya
meli hiyo iliyosababisha vifo vya baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri
kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Bandari ya Zanzibar.
Watuhumiwa
hao walikuwa wakihojiwa katika Ofisi za Upelelezi Makao Makuu ya Jeshi
la Polisi mjini Zanzibar ambapo Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai
Zanzibar, ACP Yusuph Ilembo, amesema watuhumiwa hao wawataweza
kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Kamanda
Ilembo amesema kuwa Makachero wa Jeshi la Polisi wanaendelea na
uchunguzi na kutafuta taarifa nyingine zinazohusiana na tukio hilo.
Hata hivyo, Nahodha wa zamu siku ya tukio hilo la kupinduka na kuzama kwa meli hiyo ya MV Skagit, Bw.Mussa Makame
Mussa, ameelezea kwa ufupi jinsi ajali hiyo ilivyotokea na namna yeye alivyonusurika katika ajali hiyo.
Amesema
kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya kupigwa na dharuba na mawimbi
yaliyoambatana na upepo mkali, ambapo yeye alinusurika kufa maji baada
ya kuruka kwa kutumia mlango wa mbele wa meli hiyo na kuanza kuogelea
ambapo alijichanganya pamoja na na abiria wengine walionusurika na
kuokolewa na vyombo vya uokozi.
Wakati
huo huo, Wapiga mbizi wa Vikosi vya Ulinzi na usalama leo wamefanikiwa
kuzupata maiti ngingine za watu watano akiwemo mwanamke mmoja na wanaume
wanne.
Katika
upekuzi wa maiti hizo, Makachero wa Polisi walibaini kitambulicho cha
kupigia kura kutoka kwa mmoja ya mwili wa marehemu kitambulicho
kilichokuwa na jina la Philip John Busiya aliyezaliwa mwaka 1977 katika
kijiji cha
Mapilinga kilichopo katika Kata ya Igokelo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Kupatikana
kwa miili hiyo mitano, kunaifanya idadi ya maiti kufikia 73. Maiti
nyingine 68 zilipatikana siku za mwanzo baada ya kutokea kwa ajali hiyo
ambapo kati ya hizo, maiti 54 zilitambuliwa na kuchukuliwa na ndugu na
jamaa kwa ajili ya mazishi.
Idadi
ya miili ya watu waliopoteza maisha katika boti ya MV Skagit,
imeongezeka kutoka 68 na kufikia 73, baada ya vikosi vya uokozi,
kufanikiwa kuopoa miili ya watu watanao, katika eneo la tukio karibu na
kisiwa kidogo cha Chumbe, kilichopo pembezoni mwa mji wa Zanzibar.
Maiti
hiyo iliyopewa namba 72, pamoja na maiti nyingine nne, zimezikwa katika
makaburi ya pamoja ya Kama yaliyopo nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Eneo
hilo la Kama pia lilitumika kwa kuwazika watu wengine waliokosa ndugu
wakati wa ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea Septemba 9, mwakaja
2911.
Kupatikana
kwa miili hiyo, kumetokana na juhudi zinazoendelea kwa kuvishirikisha
vikosi vya ulinzi na usalama, wazamiaji wa makampuni binafsi pamoja na
Mamlaka ya Bandari Zanzibar wakati wakiwa katika harakati za kuitafuta
boti hiyo, ili kuweza kubaini kama kuna miili mingine iliyosalia kwenye
Meli hiyo chini ya Bahari.
Aidha,
juhudi za kutaka kuiibua Meli hiyo zinaendele ambapo wazamiaji wa JWTZ,
Polisi, KMKM, JKU, Bandari na wale wa Makampuni binafsi na wale wa
kujitegemea wakiendelea na kazi ya kutafuta mahali ilipo meli hiyo ili
kuona kama wataweza kupata miili mingine iliyonasa kwenye vyumba vya
meli hiyo ambayo imekokotwa na maji kutoka eneo ilipozama meli hiyo.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!