Francis Kaswahili katibu kamati ya uchaguzi ya Yanga akiongea asubuhi ya leo katika kipindi cha michezo ndani ya Hello Tanzania Uhuru fm . |
Uzinduzi wa kampeni kwa wagombea wa
nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu ya Yanga unafanyika leo leo
katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo makutano ya mitaa Twiga na
Jangwani kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza asubuhi hii katika kipindi
cha HelloTanzania cha Redio Uhuru katibu wa kamati ya uchaguzi ya klabu
ya Yanga Fransis Kaswahili amesema wanataraji kuanza uzinduzi huo saa
10:00 jioni ambapo wagombea wote watakuwepo na kwamba fursa ya kujieleza
na kutangaza sera itatolewa kwa wagombea wote.
Kaswahili amesema kikubwa ni kutolewa
maelezo ya namna ya kufanya kampeni na utaratibu mzima utakavyo kuwa
wakati wote wa kipindi cha kampeni ambazo zitafikia kikomo Julay 14 saa
12:00 jioni.
Aidha amesema kwa ujumla wagombea
watatembea matawi takribani 100 ndani ya kipindi hicho huku muda wa
kujieleza mbele ya wanachama wa klabu ukiwa ni si zaidi ya dakika tano.
Wakati
huo huo kocha mpya wa Yanga Thom Seintfeit anatarajia kuanguka siani
ndani ya Klabu hiyo hii katika shughuli ambayo itafanyika pia makao
makuu ya klabu hiyo.Taarifa zaidi tufuatilie mtandao huu baadae.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!