StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

November 10, 2012

SIJAKUBALIANA NA MAAMUZI YA SPIKA-JOHN MNYIKA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Ikiwa ulipata fursa ya kusikiliza (audio na text ya RIPOTI NZIMA, bofya hapa) Spika alipomaliza kusoma ripoti ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mhe. Ngwilizi kuhusu tuhuma za rushwa dhidi ya Wabunge na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, utakuwa ulimsikia Mhe. John Mnyika akitaka kuzungumza lakini hakupata fursa hiyo.

Baadaye kwenye ukurasa wake wa facebook na twitter, Mnyika aliandika hivi:
Picture
Taarifa ya John Nditi, Morogoro via HabariLeo --

BAADHI ya wastaafu wa utumishi wa umma na sekta binafsi wanadaiwa kufariki Dunia mapema pale wanapostaafu kwa sababu mbalimbali ikiwa ya kuishiwa fedha za kiinua mgongo baada ya ajira zao kukoma.

Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA), umebainisha hayo katika utafiti wake uliofanyika hivi karibuni.

Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kupitia Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) imeanza kuwajengea uwezo watumishi wanaokaribia kustaafu kwa kuwapatia mafunzo na mbinu mbalimbali za kufanya shughuli za ujasiliamali. Lengo ni kuwawezesha wakabiliane na changamoto za maisha baada ya ajira zao kutoka kwenye utumishi wa umma utakapokoma.

Mratibu wa Mafunzo kupitia Wakala huo, Anslim Namala, alisema hayo juzi wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu yaliyoshirikisha wafanyakazi kutoka Mashirika ya Umma, Serikali kuu na Taasisi binafsi nchini.

Kwa mujibu wa Mratibu huyo, hali hiyo inatokana na wastaafu hao kukata tamaa na maisha kutokana na mtazamo hasi, kuwa kustaafu ni kikomo cha maisha.

Hata hivyo alisema, katika utafiti uliofanywa na kabla ya kuanzisha mafunzo hayo imebainika wastaafu wengi walikuwa wakipoteza maisha yao kutokana na hofu ya kushindwa kumudu maisha.
UPDATES from CNN blog

[Updated at 4:52 p.m.] Acting CIA Director Michael Morrell will testify next week before the Senate Intelligence Committee about the fatal attack in Benghazi instead of David Petraeus, according to the office of that committee's chairwoman, Sen. Dianne Feinstein.

[Updated at 4:25 p.m.] U.S. Sen. John McCain extolled Petraeus as one of "America's greatest military heroes," expressing his gratitude for his "decades of work on behalf of our nation, our military and our security." McCain, an Arizona Republican and the ranking member of the Senate Armed Services Committee, added, "His inspirational leadership and his genius were directly responsible - after years of failure - for the success of the surge in Iraq."

[Updated at 3:59 p.m.] Sen. Dianne Feinstein, the head of the Senate Intelligence Committee, said, "I wish President Obama had not accepted this resignation, but I understand and respect the decision."

The California Democrat praised Petraeus for giving the CIA "leadership, stature, prestige and credibility both at home and abroad," calling him reliably in "command of intelligence issues" and "especially cooperative with Congress."

[Updated at 3:53 p.m.] The chairman of the House Homeland Security Committee praised outgoing CIA Director David Petraeus, saying, "I regret his resignation and wish him and his family the very best."

"Gen. Petraeus is one of America's most outstanding and distinguished military leaders and a true American patriot," said Rep. Peter King, a Republican from New York.

[Updated at 3:41 p.m.] David Petraeus met with President Barack Obama on Thursday, at which time the then CIA director offered his resignation, a senior administration official said. The president then formally accepted Petraeus' resignation in a phone call Friday afternoon, according to the same official.

[Updated at 3:38 p.m.] President Obama said, in a statement, that today he accepted Petraeus' resignation as CIA director.

The president added he is "completely confident that the CIA will continue to thrive and carry out its essential mission," now under the leadership of Acting Director Michael Morrell.

Obama lauded Petraeus for his "extraordinary service to the United States for decades," calling him "one of the outstanding general officers of his generation" and praising his work as CIA director.

The president concluded by saying, "Going forward, my thoughts and prayers are with Dave and Holly Petraeus, who has done so much to help military families through her own work. I wish them the very best in this difficult time." Holly Petraeus led the Consumer Financial Protection Bureau’s Office for Servicemembers Affairs.

[Updated at 3:17 p.m.] Shortly before Petraeus' resignation was announced, White House press secretary Jay Carney told reporters that "the president thinks Gen. Petraeus has done an excellent job."

When asked about the general's job status, Carney reiterated that President Obama approves of the job done by the CIA director while adding, "I don't have personnel announcements to make from here today."

[Updated at 3:13 p.m.] Petraeus issued a statement announcing his resignation, saying, "After being married for over 37 years, I showed extremely poor judgment by engaging in an extramarital affair.

"Such behavior is unacceptable, both as a husband and as the leader of an organization such as ours. This afternoon, the president graciously accepted my resignation."
Picture
(photo courtesy, the library of politico.com)
WASHINGTON (AP) -- David Petraeus has resigned as director of the CIA after admitting he had an extramarital affair.

According to his letter of resignation, Petraeus asked President Barack Obama on Thursday to allow him to resign and on Friday the president accepted.

Petraeus said in a statement that he had shown "extremely poor judgment" in having the affair.

Petraeus has been married for 37 years to Holly Petraeus, whom he met when he was a cadet at the U.S. Military Academy at West Point.

The retired four-star general led the military campaigns in Iraq and Afghanistan, then took the helm of the CIA in September 2011.

The CIA had no immediate comment.

source: The Associated Press
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Jumuiya ya watumiaji wa huduma mbalimbali nchini kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter imezindua rasmi shindano la kusaka kampuni zinazotoa huduma na bidhaa mbovu kwa wateja nchini Tanzania.

Jumuiya hiyo inawajumuisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati, waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na wateja wa huduma na bidhaa mbalimbali nchini Tanzania.

Lengo la jumuiya hiyo ni kushinikiza wafanyabiashara nchini kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja na kuwakumbusha umuhimu wa wateja. Kauli mbiu ya wanajumuiya hao ni Mteja ni Mfalme.

Katika wiki ya kwanza tangu jumuiya hiyo kuzinduliwa jumla ya makampuni 21 yameingizwa katika shindano hilo kwa wateja wao kuwasilisha malalamiko yao. Kwa taarifa zaidi kuhusu ni fuatilia akaunti ya Twitter @HudumambayaTz au kundi la Facebook linalojulikana kama HUDUMA BONGO.

Ili kuweza kupiga kura yako unahitajika kuwa na akaunti hai (yenye mawasiliano mara kwa mara) katika mtandao wa Twitter au Facebook na kujiunga na jumuiya hiyo. Mara tu utakapowasilisha kero yako utaifanya kampuni unayoilalamikia kuingia katika mchuano mkali wa kumsaka bingwa wa huduma mbovu kwa wateja nchini.

Huduma Bongo inatoa wito kwa makampuni yote kuboresha huduma na bidhaa zao ili kuweza kuwapatia wateja kilicho bora zaidi katika soko hili la ushindani.

Imetolewa na Mshauri wa Habari wa Huduma Bongo - hudumabongo@gmail.com

Novemba 9, 2012
Picture
Hiki kipeperushi kiliokotwa Dodoma hoteli (picha: Lukwangule blog)
Picture
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Agustino Matefu akiongea na waandishi wa habari Mjini Dodoma. Anasema bilioni tano zimetengwa kumng'oa Mwenyekiti wa CCM (picha: Lukwangule blog)
Picture
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Kikwete akiteremka kwenye ndege leo Dodoma.
Picture
Rais Kikwete akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Dodoma leo.
Picture
Rais Kikwete akiwasili Dodoma leo,kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Imeandikwa na Sifa Lubasi, Dodoma via HabariLeo

MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ameibua tuhuma nzito na kusema kuwa kuna mpango mchafu unaosukwa kwa lengo la kuhakikisha Mwenyekiti wa Taifa Rais Jakaya Kikwete anang’olewa nafasi hiyo kwa kupigiwa kura za hapana.

Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma jana, Mjumbe huyo Agustino Matefu alisema kuwa wamegundua baadhi ya vipeperushi ambavyo vitasambazwa siku moja kabla ya uchaguzi na kuwataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kutounga mkono uchafu huo na uhuni unaoongozwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi.

Mmoja wa vipeperushi hivyo ambavyo gazeti hili lina nakala yake kilikuwa Kimeandikwa: “Ndugu Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Chama chetu kinayumba eti kwa pamoja tumpunguzie mzigo mheshimiwa Rais kwa kumvua kofia moja ya Uenyekiti, kwa pamoja tutashinda piga kura ya hapana kwake,” kilisema moja ya kipeperushi hicho chenye nembo ya Chama Cha Mapinduzi.

Alisema kuwa moja ya vipeperushi hivyo kilikutwa Dodoma Hotel ambapo Hussein Bashe na wenzake watatu walipokuwa kwenye kikao usiku wa kuamkia jana na walifika hapo baada ya kupata taarifa ya kikao hicho na kufuatilia.

Aliwataja wengine hao kuwa Beno Malisa, Martine Shigela na Fred Lowassa. Alipohojiwa Bashe alikanusha kuhusika na kampeni za kumng’oa Kikwete wala vipeperushi hivyo na kusema kuwa hizo ni fitina za kisiasa.

Mjumbe huyo wa mkutano mkuu alisema kuwa, mafisadi wametenga jumla ya shilingi bilioni tano kwa lengo la kupitisha wajumbe wao wa NEC ambao watasimamia maslahi yao ya Urais.

Alisema kuwa kuna haja ya kukataa na kupinga mipango michafu kama hiyo yenye lengo la kukifedhehesha chama na kukitia aibu na kuonekana kuwa ni chama cha watu fulani.

Mjumbe huyo wa mkutano mkuu alisema kuwa yuko tayari kutoa ushahidi kutokana na hayo anayoongea kwani ana ushahidi nayo.

“Mimi ni mwanasheria ninajua ninachokiongea kwani wakati mwingine ni lazima tukisaidie chama kule kinakopelekwa siko,” alisema.

Matefu alisema kuwa, kwa niaba ya Umoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wa nane wa UVCCM wanaopinga matokeo ya uchaguzi huo wanaendelea kusikitishwa na vitendo viovu vinavyopangwa kufanya usiku wa kuamkia uchaguzi mkuu na watahakikisha wanawaibua na kuwatangaza wanaofanya hivyo ili njama zao zijulikane.

Mgeja akanusha kumhujumu JK

Naye Kareny Masasy akiandika kutoka Shinyanga, anaripoti kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamisi Mgeja ameibuka na kukanusha uvumi anaozushiwa kwamba amezunguka katika baadhi ya mikoa kuwagawia fedha wajumbe watakaopiga kura siku ya Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama hicho (NEC) ili kumuangusha Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga alisema: “Kuna maneno yamezushwa kuwa nimeonekana na wajumbe mkoani Tabora na Zanzibar nikigawa Sh milioni tatu kwa wajumbe. Wanaozusha uvumi huo ni kundi la wahuni waliokaa na kutaka kuleta fitna, nakiomba chama kiwe macho na watu hao”.

Alisema kuna pepo mbaya ambaye anakiandama chama hicho na kuwaomba wanaCCM wote kukiombea chama hicho ili kuondoa pepo hilo.

“Hii inataka kujirudia tena, hata mwaka 2002 tuliwahi kushushwa kwenye treni wakati tukisafiri kuelekea kwenye uchaguzi kama huu tukiwa mimi, John Shibuda na Edward Ng’wani na tukaelezwa kuwa ni agizo la Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye kwa vile eti kulikuwa na tetesi kwamba tunataka kufanya fitna dhidi ya Mwenyekiti mstaafu Benjamini Mkapa.”

“Kwa bahati nzuri chama kimeruhusu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutuchunguza, naomba nichunguzwe ili ibainike ukweli wa jambo hili maana nimechoshwa na siasa uchwara, sababu wanayoieleza mbona hawasemi kuwa tukimng’oa Rais Kikwete tutamuweka nani?
Taarifa ifuatayo imeripotiwa na GSengo kwenye blogu yake:

Habari za sasa toka chumba cha uchaguzi zinamtaja diwani aliyepitia vigingi vingi huku akiwaburuza wenzie kortini mara kadhaa akidai haki zake mh. Henry Matata wa kata ya Kitangiri Ilemela jijini mwanza ameukwaa umeya wa Ilemela ...

Wajumbe wenzake wote kupitia CHADEMA walisusia kushiriki uchaguzi  wakabakia wa CCM na CUF, akidi ikawa imetimia nusu, sheria na kanuni ikaruhusu uchaguzi kuendelea, amini usiamini akashinda kwa 100%

Naibu wake ni Swila Dede (CCM) ambaye ni Diwani wa kata ya Sangabuye.
Picture
Bango pekee lililokuwepo wakati Rais Jakaya Kikwete akizindua ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara na Lindi kwenda Kinyerezi, Dar es Salaam. Katika gazeti moja linalotoka kila siku limetoa habari kuwa Rais Kikwete alakiwa kwa mabango wakati lililokuwepo ni hilo tu. Aliyeshika bango hilo kwa lengo la kufikisha malalamiko kwa Rais, hakupata kashikashi yoyote kutoka kwenye vyombo vya usalama. (picha: Kamanda wa Matukio)
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania limeteua wadau 10 kwa ajili ya kusaidia timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys itakayopambana na Congo (Brazaville) katika mechi ya raundi ya tatu ya michuano ya awali ya Mataifa ya Afrika.

Uteuzi huo umefanywa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga baada ya Kamati ya Vijana ya TFF kufanya kikao chake kujadili kwa umakini ushiriki wa timu hiyo na kupeleka mapendekezo yake kwa rais huyo wa shirikisho.

Kutokana na umuhimu wa mechi hiyo itakayoamua timu itakayofuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, TFF imeona umuhimu wa kuwa na kamati ambayo itakuwa na majukumu mawili makubwa ambayo ni:

1. Kuhamasisha vijana waone umuhimu na kuwa na ari ya kushinda mechi hiyo

2. Kuhamasisha umma uone umuhimu wa mechi hiyo na hivyo kuisaidia iweze kufuzu.

Walioteuliwa kuunda kamati hiyo ni:
  1. Ridhiwani Kikwete                                    Mwenyekiti
  2. Ahmed Seif (Magari)                                Mjumbe
  3. Nassoro Bin Slum                                      Mjumbe
  4. Henry Tandau                                            Katibu
  5. Ahmed Mgoyi                                            Mjumbe
  6. Aboubakar Bakhresa                               Mjumbe
  7. Angetile Osiah                                           Mjumbe
  8. Kassim Dewji                                             Mjumbe
  9. Abdallah Bin Kleb                                   Mjumbe
  10. Salim Said                                                   Mjumbe

Baada ya kuvuka raundi mbili za kwanza bila ya kucheza mechi kutokana na wapinzani wake kujitoa, timu ya Serengeti Boys inahitaji kufanya kila iwezalo kuweza kuiondoa Congo kwenye mashindano hayo na kuweka rekodi ya kufuzu kucheza fainali hizo za Afrika ambazo pia zitatoa wawakilishi wa Afrika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.

Mechi za kwanza za raundi ya tatu zitachezwa kati ya Novemba 16 na 18, 2012 na mechi za marudiano zitachezwa kuanzia Novemba 30, 2012 hadi Desemba 2, 2012
Picture
Eliakim Maswi

Tafadhali bofya kifute cha pleya hapo kumsikiliza Spika wa Bunge, Anne Makinda akisoma Bungeni leo, ripoti ya Kamati Ndogo ya Bunge iliyochunguza kashifa iliyomhusisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini na Nishati, Eliakim Maswi akiwatuhumu baadhi ya Wabunge kula rushwa kutoka kwenye makampunmi ya mafuta.

Baada ya kusoma ripoti, Spika alitoa uamuzi wake.

Ripoti hiyo ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa (Mlalo-CCM), Brigedia Jenerali mstaafu Hassan Ngwilizi iliundwa Julai 2 mwaka huu na ilishakamilisha kazi yake na kuiwasilisha kwa Spika, Septemba 20, 2012.

Pamoja na Mwenyekiti Ngwilizi, wajumbe wengine wa kamati hiyo walikuwa Said Arfi (Mpanda Kati), John Chiligati (Manyoni Mashariki), Goesbert Blandes (Karagwe) na Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Omary Juma.

00:00
00:00
Ripoti ya Kamati ya Bunge - Spika, Anne Makinda
Text document (maandishi) ya kilichopo kwenye audio imepachikwa hapo chini (embedded document).


Source: http://www.wavuti.com/index.html#ixzz2BnIQzYRa

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat