BAADHI ya warembo , wanamitindo na waigizaji kadhaa kutoka Bongo movie watajumuika pamoja katika tukio maalum la kuosha magari litakalofanyika klabu ya Matongee mjini Arusha Julai 14, mwaka huu.
Tukio hilo la hisani linalenga kuchangisha pesa kwa ajili ya kuwasaidia watoto walio katika mazingira magumu walio katika kituo cha kulelea watoto cha kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Kituo hicho kinafahamika kama Good hope, kipo eneo la USA river nje kidogo ya jiji hilo kina watoto wapatao 50 wenye umri kuanzia mwaka na nusu hadi yani wanashida sana
Msemaji wa tukio hilo mwanamitindo Angel Justice amesema, baada ya kutembelea kituo hicho na kuona mapungufu yaliyokuwako, wameona ni vyema wakahamasisha jamii kuchangia pesa kwa ajili ya kuwasaidia watoto walio katika kituo hicho.
“Watoto hao wana shida sana , wanahitaji betri kubwa sita kwa ajili ya umeme kwenye kituo chao, mavazi chakula na kila kitu kinachofaa kwa ajili ya watoto. Kwa kuwa hatuna uwezo wa kuwapa kutoka mifukoni kwetu, tumeona ni bora kuwachangia kupitia vipaji vyetu” , alisema Angel.
Angel ameliambia Starehe kuwa mrembo Sylivia Shaali na Jackline Wolper watawaongoza warembo washiriki wa Kinyang’anyiro cha Miss Arusha katika shughuli hiyo ya kijamii.
Shughuli hiyo itaambatana na disco la aina yake litakaloporomoshwa na Jambo squad pamoja na wamamuziki wengine kibao kutoka ndani na nje ya Arusha alisema.
Tumepanga kufanya shughuli hiyo mwezi ujao, lakini kwa sasa tunachokifanya kwa sasa ni kuhamasisha watu wenye mapenzi mema kuleta magari yao kwa ajili ya kuoshewa na pia kuwachangia watoto hawa wenye mahitaji muhimu kwa ukuaji wao.
Tukio hilo limeandaliwa na kampuni ya ‘Tour visual promotion’, na litakuwa likifanyika kwa mara ya kwanza. Lengo lao ni kufanya kama kampeni kwa kuzunguka maeneo mbalimbali ya nchi wakilenga kusaidia zaidi.