Kiiza akipambana na mchezaji wa APR
Wachezaji wa yanga wakishangilia walipopata bao
Said Bahanuzi 'Spider Man' akiwa amembeba Kiiza baada ya kufunga bao
Kiiza akipambana
BAO
pekee la mwanasoka bora wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 110,
limeipa Yanga tiketi ya kucheza Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo, na sasa
itamenyana na Azam FC keshokutwa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kiiza
alifunga bao hilo, kwa kichwa akiunganisha krosi ya karibu ya Haruna
Niyonzima ambaye alitumia mwanya wa mabeki wa APR kuzubaa wakisikilizia
maamuzi ya refa, baada ya Kiiza kuangushwa.
Yanga
waliinuka na wakaanzisha shambulizi la haraka lililozaa bao hilo.
Dakika tatu baada ya bao hilo, beki wa Yanga, Godfrey Taita alitolewa
nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na sasa ataikosa fainali.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!