HUKU wadau wakiwa na shauku kubwa ya kumjua mshindi wa shindano hili la kumsaka staa wa kike mwenye mvuto ambaye hajaolewa ‘The Ijumaa Sexiest Girl’, hatimaye kura za wasomaji zimeamua msanii wa filamu, Jackline Wolper kutoa mkono wa kwaheri.
Mratibu wa shindano hili, Imelda Mtema alisema: “Mtifuano ulikuwa mkali sana na hii ilitokana na ukweli kwamba, wote waliobaki ni wakali kuanzia sura hadi maumbo yao. Wopler ametolewa na sasa kimbembe ni kati ya Wema na Agnes.”
Kufuatia matokeo hayo ya Wolper kuchapa lapa, sasa wanabaki Wema na Agnes ambao watapigiwa kura kwa wiki mbili kabla ya kumpata mshindi. Ili kushiriki katika hatua hii muhimu ya kumpata mshindi, andika jina la mshiriki kisha litume kwenda namba 0786-799120.
global publishers
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!