StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 18, 2012

BAVICHA TAIFA WAKUTANA MOROGORO KUWEKA MIKAKATI YA KUIMALISHA CHAMA CHAO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Baadhi ya wajumbe wa Bavicha Taifa wakipitia ajenda za kikao hicho

Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa zamani wa TBC, Jerry Muro ( kulia ) akifurahia jambo na Viongozi wakuu wa Bavicha Taifa akiwemo Mwenyekiti wake , John Heche ( wapili kulia ) viongozi hao walimwalika Muro kuwasalimia wajumbe wa Kamati ya Utendaji cha Bavicha Taifa iliyoketi Mjini Morogoro kuanzia Septemba 14 hadi 18, mwaka huu.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Bavicha Taifa wakiomba dua kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati ya Utendaji cha Bavicha , Septemba 17, mwaka huu katika ukumbi wa Hoteli ya Top Life ya Mjini hapa.

Wajumbe wakisimama kwa dakika kadhaa kukumbuka waliopoteza maisha

Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa zamani wa TBC, Jerry Muro ( kushoto) akito salamu zake kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji cha Bavicha Taifa iliyoketi Mjini Morogoro kuanzia Septemba 14 hadi 18, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Bavicha Taifa , John Heche , Septemba 17, 2012 alifungua Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha kilichohudhuriwa na wajumbe kadhaa kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

Baadhi ya wajumbe wa Bavicha Taifa wakipitia ajenda za kikao hicho.



Picha na Habari na John Nditi
Mwenyekiti wa Bavicha Taifa , John Heche , jana Septemba 17, 2012 alifungua Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha kilichohudhuriwa na wajumbe kadhaa kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
Kikao hicho kilipanga kujadili ajenda mbalimbali za Vijana na baadaye kufikia kutoa tamko la pampoja kuhusiana na masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Hata hivyo katika Kikao hicho , Bavicha kupitia Mwenyekiti wake wa Taifa , walimkaribisha Mwandishi wa Habari na Mtangazani wa zamani wa TBC, Jerry Muro ili aweze kuwasalimia wa wajumbe wa Baraza hilo walioanza kukutana tangu Septamba 14 hadi 18, mwaka huu.
Katika salaamu zake , Muro alisema, yenye ni mwanaharakati na mtu anayependa kusema ukweli, hivyo kwake mtu kama huyo ni lazima amuunge mkono kama ilivyo kwa vijana wa Bavicha wanavyosimamia kusema ukweli na kuamua kuwaunga mkono kwa hilo.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat