Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Maya Kodnani.
MAHAKAMA moja nchini India imempata na hatia waziri wa serikali kwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya waisilamu tisini na tano wakati wa ghasia za kidini katika jimbo la Gujarat miaka kumi iliyopita.
Maya Kodnani aliyekuwa waziri wa mambo ya wanawake, alituhumiwa kwa kuchochea ghasia dhidi ya jamii za waisilamu katika wilaya ya Naroda Patiya mjini Ahmedabad.
Alipatikana na hatia akiwa na mshtakiwa mwenzake ambaye ni kiongozi wa wapiganaji wa kihindu Babu Bajrangi pamoja na washukiwa wengine thelathini.
Ghasia za Gujarat zilizuka baada ya mahujaji sitini wa kihindu kufariki katika ajali ya Treni.
Zaidi ya watu elfu moja wengi wao wakiwa waisilamu waliuawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.
August 31, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!