Papaa Musoffe
Jalada la kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Marijan Abubakari maarufu kama Papaa Msofe, lipo katika mchakato wa kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili aweze kufikishwa mahakamani.
Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema jalada la kesi hiyo litakapofika kwa DPP atapanga kesi hiyo ipelekwe mahakama gani ili mtuhumiwa huyo asomewe shitaka hilo.
Papaa Msofe alikamatwa kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mfanyabiashara mwenzake, Onesphori Kituli, mkazi wa Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa kabla ya mauji hayo, Papaa Msofe na marehemu walikuwa wakigombea nyumba ambayo ilikuwa imewekwa rehani kwa Sh. milioni 30 ambazo Papaa Msofe alimpa marehemu kwa makubaliano kwamba ikiwa atashindwa kuzilipa atachukua nyumba yake.
Papaa Msofe na mwenzake inadaiwa walikuwa wakimtishia maisha marehemu huyo ambapo alifungua kesi mahakamani, lakini siku ya hukumu alikutwa amekufa mbele ya mlango wa nyumba yake huku kukiwa hakuna mali yoyote iliyochukuliwa.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!