WADAU TUNAOMBA RADHI KWA PICHA MNAYOIONA HAPO CHINI LAKINI NDIO HALI HALISI.
Festus Pangani, Njombe Yetu
Mtoto Juliana Mwinuka wa kijiji cha Mbugani kata ya Mavanga wilayani Ludewa Mkoani Njombe, anaomba msaada kwa wadau mbalimbali ili kumsaidia kupata matibabu baada ya kuungua moto na hali yake ni mbaya sana.
Mtoto huyo ambaye kwa sasa anaishi na bibi yake ambaye hana uwezo, baada ya baba mzazi kumtelekeza mara tu baada ya kupatwa na mkasa huo miaka miwili iliyopita.
Juliana ameishi katika maumivu hayo kwa miaka miwili na hana mtu wa kumsaidia kufanikisha matibabu yake.
Account ni 6012300170 na kwa M-PESA ni 0755 008038.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!