BAADA ya kuachana na mumewe Hamisi Bwela, msanii wa filamu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amenasa SHATI (PENZI) jipya kwa msanii wa Bongo Fleva, Joseph Rushalu `Bwana Misosi’.
Habari zilizopatikana kutoka katika chanzo chetu makini, zinasema kwamba, wawili hao hivi sasa hawasikii wala hawaoni kutokana na kuzama katika penzi motomoto.
“Amanda amekufa ameoza kwa Misosi, sasa hivi mapenzi yao siyo siri tena... ni njenje na wanapendana sana hakuna mfano kwa kweli,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi mwandishi wetu aliwasiliana na Amanda ili kupata ukweli wa habari hizo ambapo bila hiyana alikiri kutoka na Bwana Misosi na kwamba anampenda kuliko maelezo.
“Ni kweli Misosi ni mpenzi wangu na ninampenda sana na sijui ni kitu gani kitakachonitenganisha naye,” alisema Amanda.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!