StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 19, 2012

MHESHIMIWA JK ALITEUA MAJAJI WASIO NA SIFA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends  

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete na Jaji Mkuu Othman Chande, kuunda tume maalumu kuchunguza tuhuma za majaji walioteuliwa kukosa sifa, lengo likiwa ni kujenga imani kwa wananchi.

Akizungumza masuala ya kisheria yaliyojitokeza ndani ya miezi sita iliyopita, Rais wa TLS, Francis Stolla alisema tangu kutolewa kwa tuhuma hizo bungeni, si Rais au Jaji Mkuu aliyeweza kujibu hoja.

“Tuhuma za uteuzi wa majaji ambao hawana sifa zizolitolewa Bungeni, TLS haijafanya utafiti wowote kupata ushahidi wa kweli wa tuhuma hizo, hivyo ni bora Rais na Jaji Mkuu, wakaunda tume ya kuchunguza tuhuma hizo,” alisema na kuongeza: “Kama itabaini ni kweli wapo, basi itamshauri Rais ili naye aueleze umma maana wale wenye kesi zao zinazosikilizwa na majaji hao, wanakosa imani”.

Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), akitoa hotuba ya upinzani ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria alieleza kuwa baadhi ya majaji walioteuliwa hawana uwezo.

Lissu alisema baadhi yao wamekuwa wakishindwa hata kuandika hukumu kwa lugha ya Kiingereza inayotumika mahakamani hivyo kuchelewesha uandaaji wa rufaa kwa watuhumiwa.

Pamoja na hatua ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kumtaka Lissu kufuta maneno yake hayo kugonga mwamba, Spika alipeleka suala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

Akizungumzia kuhusu mauaji yaliyotokea hivi karibuni yanayohusisha vurugu na vyombo vya dola, Stolla alisema si utaratibu muafaka wa kuunda tume za kuchunguza mauaji kama ile iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na badala yake Jaji Mkuu anatakiwa kuunda Mahakama ya Coroner inayotakiwa kuchunguza vifo visivyo na sababu vinavyotokea pale nguvu za zaida zinapotumika, utekelezaji wa amri ya Mahakama na mtu kufa akiwa mikononi mwa vyombo vya umma.

Alisema Jaji Mkuu akiunda Mahakama hiyo itafanya kazi ya kuchunguza mauaji hayo kubaini kama vifo hivyo yanatokana na matumizi ya nguvu za ziada, wakati wa utekelezaji wa amri ya mahakama au la na kupeleka taarifa Mahakama Kuu ambayo itapeleka taarifa hiyo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka ambaye ataagiza kufunguliwa kwa kesi.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat