StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 19, 2012

MTIKILA: KESI YA MGOMBEA BINAFSI KUSIKILIZWA NA MAHAKAMA YA HAKI ZA BINAADAMU AFRICA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends  
Lile jinamizi linalokuja kuitafuna na kuimalizia mbali CCM linazidi kukolea moto.
MAHAKAMA ya Haki za Binadamu Afrika (AfCHPR), imeapisha majaji wake na kusema baada ya hapo, itapanga tarehe ya kutoa uamuzi wa kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya mgombea binafsi.

Majaji walioapishwa jana ni Jaji Ben Kioko kutoka (Kenya) na Jaji Elhadji Guisse wa Senegal watakaoshikilia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka sita.

Aidha, majaji walimchagua Jaji Sophia Akuffo kutoka Ghana kuiongoza kwa kipindi cha miaka miwili ijayo. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa Mahakama hiyo,  Jean Pierre Uwanone, majaji hao watachagua Makamu wa Rais hivi karibuni.

Uwanone alisema mahakama hiyo imeapisha majaji hao na baadaye itapanga tarehe ya uamuzi wa kesi ya Mchungaji Mtikila ambaye alifungua kesi ya mgombea binafsi.

Kwa mujibu wa Uwanone, Mtikila alipeleka kesi mahakamani hapo kupinga uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kutupilia mbali rufaa yake kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kukataa kuwapo kwa mgombea binafsi (wasio na vyama) katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Majaji hao walikula kiapo jana mbele ya Jaji Gerard Niyungeko kutoka Burundi ambaye amemaliza kipindi chake cha urais wa mahakama hiyo na kumpisha aliyekuwa Makamu wa Rais, Jaji Akuffo kuongoza mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Baada ya majaji hao kuapishwa, Jaji Kioko alisema atahakikisha haki za binadamu zinazingatiwa, na kuziomba nchi za Afrika zinazoingia katika uchaguzi mbalimbali, kuacha kukiuka haki za binadamu badala yake, zifanye uchaguzi wa huru na haki.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat