Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Na Anna Nkinda – Maelezo, New York
MSHIKAMANO wa pamoja unahitajika baina ya nchi
zilizoendelea na zinazoendelea ili kuhakikisha mtoto wa kike ambaye
hajapata nafasi ya kwenda shule anapata elimu, kuwainua wanawake
kiuchumi na kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto
vinavyotokana na tatizo la uzazi na ugonjwa wa kansa.
Hayo yamesemwa jana na Mke wa rais Mama Salma Kikwete wakati
akichangia mada kwenye mkutano wa The RAND African First Ladies
Initiative uliofanyika makao Makuu ya Taasisi ya Ford mjini New York
nchini Marekani.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA) alisema kuwa taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo
za kiserikali zinafanya jitihada kubwa ya kuhakikisha kuwa zinawasaidia
wanawake wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha tatizo
lililopo ni upungufu wa rasilimai fedha za kuweza kukabiliana na
changamoto hizo hivyo basi ushirikiano wa pamoja unahitajika ili kuweza
kufanikisha malengo hayo.
Aliendelea kusema kuwa watoto wa kike wakipata elimu ya kutosha
watakuwa na silaha muhimu katika maisha yao ya kuweza kupambana na
matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na maradhi, ujinga na umaskini
kwani elimu ni nguzo muhimu katika maendeleo ya taifa lolote Duniani
bila ya watu kuwa na na elimu nchi haiwezi kuendelea.
“Ukimuelimisha mtoto hasa mtoto wa kike ambaye amekosa nafasi ya
kupata elimu ni faida kwa mtoto, Taifa na Dunia kwa ujumla kwani hivi
sasa tumejionea wanawake wengi wakishika nafasi za juu za uongozi
kitaifa na Dunia pia wameweza kujikwamua kiuchumi tofauti na miaka ya
nyuma”, alisema Mama Kikwete.
Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya WAMA alisema kuwa nchini Tanzania
watoto wengi wa kike ambao ni yatima na wanaishi katika mazingira
hatarishi wameshindwa kupata elimu sawa na watoto wengine hivyo basi
aliamua kuanzisha taasisi hiyo ili aweze kuwasaidia watoto hao,
kuwainua wanawake kiuchumi na kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na
watoto na wanaougua ugonjwa wa kansa kwa kutoa elimu kwa wananchi na
vifaa tiba katika vituo vya afya na Hospitali .
Mkutano huo wa siku moja ulihudhuriwa na wake wa marais na wakuu wa
Serikali wa Afrika, mke wa rais mstaafu wa Marekani Laura Bush na mke
wa waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Cherie Blair, pamoja na viongozi
mbalimbali wa Serikali na mashirika binafsi kutoka nchi wa Afrika na
Marekani.
Katika mkutano huo mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na
kuangalia jinsi gani wake wa maraisi na wakuu wa Serikali wanaweza
kuleta mabadiliko katika nchi zao katika kuimarisha afya ya mwanamke,
kuhakikisha kuwa mtoto wa kike anapata elimu na na kuwainua wanawake
kiuchumi pamoja na changamoto wanazoweza kukabiliana nazo
September 28, 2012
MSHIKAMANO WAHITAJIKA BAINA YA NCHI ZILIZOENDELEA NA NCHI MASKINI ILI KUMSAIDIA MTOTO WA KIKE KIELIMU
Millionfortune.com
JAMII
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!