Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Benchi la kuhesabu kura za uchaguzi wa UWT wilaya ya Manyoni. Aliyesimama ni msimamizi wa bechi hilo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida Selestin Yunde.
Mwanamke ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja akiandika jina la mgombe aliyemchagua kwenye uchaguzi wa nafasi mbali mbali za uongozi katika UWT wilaya ya Manyoni.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi wa UWT wilaya ya Manyoni Mkuu wa Wilaya Queen Mlozi akitangaza majina ya washindi wa nafasi mbalimbali za uongozi.
Mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida Fatuma Tauofik (wa kwanza kulia) na Mwenyekiti wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa UWT wilaya ya Manyoni diwani Neema Salum, wakifuatilia kwa makini uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa maktaba ya kanisa katoliki mjini Singida.
Baadhi ya viongozi wa UWT wilaya ya Manyoni waliohudhuria mkutano mkuu wa uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa maktaba wa kanisa katoliki Singida.
Msimamizi wa uchaguzi wa UWT wilaya ya Manyoni na mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mloz akitoa burudani kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa UWT wilaya ya Manyoni.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida, wamemchagua Mwanahawa Issa Yusufu kuwa mwenyekiti wa umoja huo baada ya kuwagaragaza wapinzani wake wawili.
Mwanahawa ameshinda nafasi hiyo baada ya kuzoa kura 314 na kuwaacha kwa mbali wapinzani wake Elizabeth Bajile aliyepata kura 126 na Neema Mwitikizi aliyeambalia kura 95.
Elizabeth Bajile alikuwa akitetea nafasi yake hiyo.
Msimamizi wa mkutano huo mkuu wa uchaguzi Mwalimu Queen Mlozi aliwatangaza Neema Mwitikizi, Rehema Chizumi na Rose Madumba kuwa wameshinda nafasi tatu za wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT taifa.
Mlozi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Singida aliwatangaza Asinath Manase, Ezereda Mkowi, Magreth Mlewa, Lucy Mtinia, Mariamu Mahujo na Mwanamvua Nassoro wamechaguliwa kuwa wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Manyoni.
Amesema nafasi tatu za wajumbe wa mkutano mkuu UWT mkoa, zimenyakuliwa na Elizabeth Kidolezi, Mwanamvua Nassoro na Sauda Ngoy.
Msimamizi huyo wa uchaguzi mamesema Mwanne Samson ambaye alikuwa mgombea pekee katika nafasi ya uwakilishi katika mkutano mkuu CCM wilaya amepita bila kupigwa.
Mlozi amesema kuwa nafasi ya uwakilishi katika jumuiya ya wazazi, imechukuliwa na Elizabeth Paulo Lwanji na nafasi ya uwakilishi katika jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) ameshinda Leah Haule.
Amesema mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Manyoni Asinath Manase ameshinda nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Manyoni.
Wakati huo huo, katibu wa UWT wilaya ya Manyoni Mwanaidi Kaleghela amesema mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa maktaba wa kanisa katoliki mjiniSingida umehudhuriwa na wajumbe 531 kati ya 756 waliokuwa wakitarajiwa.
Aidha, katika taarifa yake amesema jumuiya hiyo mwaka huu ina wanachama 10,147 waliolipia ada ni 87 na ambao bado ni 10,060.
Kwa mwaka jana kulikuwa na wanachama 9,939 waliolipia ada ni 24 na ambao hawakulipia ni 9,916.
September 5, 2012
MWANAHAWA YUSUFU NDIYE MWENYEKITI MPYA UWT WILAYA YA MANYONI MKOANI SINGIDA.
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!