StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

November 16, 2012

HUU WIZI WA VIFAA VYA MAGARI DAR ES SALAAM UMEKITHIRI...HEBU SOMA HII

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Ni hoja aliyoianzisha mwanachama mmoja kwenye ukumbi wa Mabadiliko Tanzania:

Jamani imekua tabia sasa ambayo naona serikali hasa kwenye mji wa Dar imeshindwa kabisa kuchukua hatua za kuzuia au angalau kulikemea hili suala, kwa ufupi mamlaka husika ni kama hazipo kutekeleza wajibu wake wa kisheria wa kulinda raia na mali zao!!!

Kuna tatizo kubwa sana la magenge ya majizi kuiba taa, side mirrors, vitasa vya milango au power windows na kila kinachoweza kuchukulika katika magaari ya watu mchana kweupe au hata usiku.

Binafsi nimepatwa na hili tatizo kama mara 3 au 4 hivi, nikaambiwa niende eneo la Gerezani, na kweli nikavipata, ila sasa nikatumia ukamanda kwa kushirikiana na jamaa zangu wa jeshini nikavichukua kwa nguvu bila kuvinunua.

Kununua maana yake ningeliuziwa mali yangu mwenyewe, na hilo lilikua linanikera sana sana kabisa. Ndio maana pamoja na kuvichukua kwa nguvu pia tukatembeza kichapo kwa hawa wezi...

Nimewahi kuripoti suala hili polisi ila kumbe kuna baadhi yao wanashiriki katika hii kazi haramu na inaumiza sana watu kwani sio tu wanaiba hivo pia wanachukua laptops za watu na kusababisha hasara kubwa sana kwa wakazi wa huu mji wa Dar.

Kibaya zaidi ni tabia ya watu hawa kuiba mchana na usiku kwenye foleni au maeneo ya Mlimani City, Vyuoni, Makazini... yaani kwa ufupi kila mahala ukisimamisha gari lako sio salama na unaenda roho inakuuma, je ntalikuta salama?!!

Mamlaka husika zinajua na kama hazijui hazifai kuwepo. Kwa nini ile sentensi intelijensia haitumiki hapa kukomesha wizi huu?

Imefikia hatua nawapa changamoto watu wa Dar ambao unaibiwa mchana na wao wanaona wanakaa kimya kama hawaoni, acheni tabia hizi za ovyo maana leo wewe kesho mwingine. Mimi mara zote nawakabili kwa nguvu, labda nisiwakute, ila nikiwakuta huwa simwachi salama lazima awe kilema, nahakikisha hataiba tena! Watu hawa nimeshuhudia mara 5 wakiwavamia akina mama na kuwanyanganya laptop na hapo usaidizi ukijaribu unashindwa maana na mimi sitaacha gari ili waibe, ila ukikabidhi mwenzio ni rahisi tukawakabili na watajua kwamba sasa sio rahisi kuiba, na sisi kama jamii tutajinusuru bila kutegemea polisi.

Nawasilisha.

Heche Suguta
hechesuguta29@yahoo.com



Nionavyo mimi...
Jeshi la polisi kwa kutokufanya kazi yenu barabara katika kulinda usalama wa raia na mali zao, ndiyo sababu ya kuchangia kuongezeka kwa watu kujichukulia sheria mikononi.

Wananchi kwa kutokusaidiana katika kukomesha tabia ya wizi

1. kwa kutokununua mali za wizi
2. kwa kutokudai risiti halali
3. kwa kutokutoa msaada pale tunaposhuhudia uhalifu unafanyika

tunachangia kukua kwa tatizo hili.


Subi

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat