Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Bodi
ya ushauri ya masuala ya rushwa Afrika inakutana kwa wiki nzima jijini
Arusha hivi karibuni ili kuandaa taarifa ya hali ya rushwa
itakayowasilishwa katika mkutano wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika(AU)
utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao Adis Ababa Ethiopia.
Bodi
hiyo pamoja na mambo mengine,itapitia kwa mapana changamoto za rushwa
katika nchi wanachama wa AU, sanjari na kutathmini nchi mojamoja katika
maeneo yanayolalamikiwa mara kwa mara,ikiwa ni pamoja na rushwa katika
uwekezaji,huduma za jamii,na matukio ya rushwa katika chaguzi na siasa
ambayo yanatajwa kuwa chanzo cha migogoro barani Afrika.
Dk.Edward Hosea ambae ni mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) ,ametoa takwimu za kushtua zinazoonyesha hali halisi ya
wizi wa fedha za umma na rushwa katika nchi za Afrika ambazo hutoroshwa
kila mwaka na kuhifadhiwa katika nchi zilizoendelea. Amesema kiasi cha
Dola bilioni 148 hutoroshwa kutoka Afrika kwenda nchi za ughaibuni kila
mwaka kwa sababu ya Rushwa.
Hata
hivyo,Mkurugenzi huyo amesema nchi zilizoendelea ambazo mabenki yake
yanahifadhi fedha hizo,zinawajibika katika kuhakikisha fedha hizo
zinarejeshwa katika nchi zinakoibwa.
Wakati
huo huo,Dk.Hosea amesema wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika katika
mkutano uliopita,waliteua jiji la Arusha Tanzania kuwa makao makuu ya
Bodi ya Ushauri wa masuala ya rushwa barani Afrika na kwamba serikali ya
Tanzania tayari imetoa eneo ka ajili ya ujenzi wa makao makuu hayo na
kinachosubiriwa ni kuona serikali imetenga kiasi gani kwa ajili ya
ujenzi huo.
Wataalamu
mbalimbali wamealikwa kuwasilisha mada katika kikao hicho cha
maandalizi,ili kuwawezesha wajumbe wa bodi hiyo kupata uzoefu wa hali na
mazingira ya rushwa katika nyanja mbalimbali,huku mtoa mada wa kwanza
akiwa ni Mtanzania Jaji Augustin Ramadhani kutoka mahakama ya Afrika ya
haki za binadamu.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!