Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
WAKATI Yanga ikiwa katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili kwa
ajili ya msimu ujao, suala la namba katika kikosi cha kwanza ‘First 11’
ndiyo tatizo.
Baada ya mazoezi ya takribani wiki moja, tayari kikosi
cha kwanza kimeanza kujipanga huku baadhi ya namba zinaonekana zitakuwa
na utata mkubwa kutokana na viwango vya wachezaji wake.
Mashabiki wanaohudhuria mazoezi ya Yanga kwenye Uwanja wa Kaunda wamekuwa wakijaribu kupanga vikosi vyao bila ya mafanikio.
Lakini hata kama Yanga itamchukua Kocha, Tom Saintfiet raia wa Ubelgiji, hawezi kukikwepa kikosi kitakachochambuliwa hapa chini.
Inaonekana
ni ushindani mkali kati ya wachezaji waliokuwepo awali na wale wapya
huku kila mchezaji akijitahidi kupambana ili apate nafasi bila ya kujali
ni mgeni, mwenyeji, mkongwe au chipukizi.
Sasa Yanga inafanya
mazoezi chini ya kocha Fred Felix Minziro na juzi aligawanya vikosi
ambavyo huenda vikawa vinatoa picha ya nani ataanza nao katika mechi
zake za kirafiki zinazotarajia kuanza kucheza hivi karibuni.
Kipa:
Haina ujanja, Ally Mustapha
‘Barthez’aliyesajiliwa akitokea Simba itabidi asubiri kwa Yaw Berko
ambaye ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Yanga.
Walinzi:
Pembeni
hasa kulia kuna utata, nahodha Shadrack Nsajigwa anapata upinzani mkali
kutoka kwa Juma Abdul kutoka Mtibwa Sugar ambaye ameonyesha kiwango
kizuri mazoezini. Bado inawezekana Ladislaus Mbogo kutoka Toto anaweza
kucheza pembeni wakati Godfrey Taita pia yuko tayari.
Beki ya kushoto haina upinzani mkali zaidi na inaonekana ni Oscar Joshua na Stephano Mwasyika kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Kwa
beki ya kati, pia hakuna utata kwa kuwa waliokabidhiwa namba nne ni
Kelvin Yondani, ‘kitasa’ au tano ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo
mkabaji anasimama Athumani Iddi ‘Chuji’.
Kiungo:
Katika
hali ya kawaida, inaonekana kiungo mkongwe, Haruna Niyonzima atasogea
mbele kucheza namba 10 na kumpisha kinda Frank Domayo aendeshe timu pale
namba 8.
Lakini kazi ipo kiungo cha pembeni namba 7 ambako kuna Nizar Khalfan, Ally Shamte na kinda Simon Msuva.
Upande
wa kushoto yaani namba 11 ndiko kuna shughuli ya kutoa machozi, jasho
na ikibidi damu kati ya Said Bahanuzi aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar
na Hamis Kiiza ambao hawapishani sana kiuwezo. Usisahau kuna Rashid
Gumbo na Idrissa Rashid.
Ushambuliaji:
Hapa
hakuna kazi kubwa, lazima Mohammed ‘Meddie’Kagere ambaye anatua kutoka
Polisi Rwanda itabidi amiliki namba hiyo na kama atasaidiana na
Myarwanda mwenzake, Niyonzima huenda ikawa poa zaidi. Hata hivyo,
inabidi Myarwanda huyo afunge mabao, la sivyo namba yake itabaki kwa
Jerry Tegete.
Chanzo: Global publishers