Je, unayaendeshaje maisha yako ya kila siku, na watu wanajifunza nini
kutoka kwako? Je, unawezaje kukubalika na watu vile ulivyo? Na pia
unawezaje kuwashawishi watu wakupende, au labda ukawa mtu muhimu kama
wao?
Haya ni baadhi ya maswali muhimu sana ya kujiuliza kwa kila mmoja wetu sisi.
Mtu Yeyote Yampasa Kujijua Vema Vile Alivyo. Yale Mtu Asiyopenda Kufanyiwa, Naye Asipende Kuwafanyia Wengine.
Endapo Umefanikiwa Kimaisha, Penda Kujishusha Sana. Usichukulie Kigezo Cha Uwezo Wako, Kunyenyekewa Na Ndugu Au Marafiki. Kwani Itafika Muda Ambao Heshima Itaondoka Kwa Watu Hao. Ni Vizuri Kujiona Kuwa Wewe Ni Mtu Wa Kawaida Sana Ili Aliyenacho Na Asiyenacho,
Endapo Umefanikiwa Kimaisha, Penda Kujishusha Sana. Usichukulie Kigezo Cha Uwezo Wako, Kunyenyekewa Na Ndugu Au Marafiki. Kwani Itafika Muda Ambao Heshima Itaondoka Kwa Watu Hao. Ni Vizuri Kujiona Kuwa Wewe Ni Mtu Wa Kawaida Sana Ili Aliyenacho Na Asiyenacho,
FORTUNAS WILBARD, MWASISI WA MILLIONFORTUNE.COM
Aweze Kukufikia Kwa Ukaribu Kwa Ajili Ya
Kubadilishana Mawazo Nawe.
Mara nyingi mtu anapokubalika katika jamii inayomzunguka, huwa na
maendeleo ya haraka kwa kuwa, hushirikiana nao kimawazo, hata wakati
mwingine kiuchumi.
Na pale mtu anapokuwa na mafanikio yoyote, yanaweza kuwa ya elimu,
ushauri mbalimbali, ushirikiano mzuri kwa jamii ama mafanikio ya
kiuchumi, ni rahisi sana hata kuwa na marafiki wengi na wa karibu,
wakiwepo ndugu na wale wanaoamini kuwa utakuwa mmoja wa watu maarufu,
kujulikana na kuwavutia.
Katika mafanikio hayo, watu hao wataamini kuwa kwenye shida mbalimbali
watakazokuwa nazo, wewe ndiye utakayekukuwa kimbilio lao, hata kwa
upande wa wakwe na shemeji zako watakupenda na kukuthamini. Hii yote ni
kwa sababu ya mafanikio yako.
Lakini pia, kuna baadhi ya watu ambao pasipo sababu yoyote hawapendwi,
wala kukubalika na wengine. Hata kama watafanya jambo zuri, bado ndugu
au marafiki wataona ni bure. Kwa kifupi unaweza kusema kuwa, watu hao,
wametengwa na jamii.
Watu wa aina hii, huishi maisha ya shida, yenye huzuni, upweke na
maumivu makali moyoni. Kwa sababu hujihisi wamebaguliwa, kutengwa na
ndugu pamoja na marafiki bila kujua sababu ya msingi ya kufanya iwe
hivyo.
Siku mmoja katika mkutano, mtu mmoja alimuuliza mfanyabiashara mmoja
maarufu, aliyejaliwa akili za kipekee pamoja na upendo kwa watu, kuwa
kwa muda mrefu amekuwa akijitahidi kuwa karibu na watu bila mafanikio,
matokeo yake watu humkimbia.
Mtu huyo aliuliza huku akimgeukia mfanyabiashara yule “Au ninaonekana
nina ringa sana, najidai, mzuri sana au mpole kupita kiasi?,” aliendelea
kuuliza mtu huyo,”kama mtu hakupendi, unatakiwa ufanye nini?”
Mfanyabiashara huyo alimjibu kwa busara kuwa, ajitahidi kutokuonyesha
hali ya huzuni kwa hao wanaomtenga, aonyeshe hali ya furaha na
unyenyekevu muda wote. Pia asiwe na wivu kwenye mafanikio ya watu
wengine, afurahi nao na kutoa ushirikiano pale unapohitajika.
Vile vile awe mwenye moyo wa ukarimu na upendo, kwa kuwa ni silaha yenye nguvu katika maisha yake yote.
Hivyo ndugu yangu, endapo kuna njia au tabia mbaya inayochukiza jamii,
ni vema ukaachana nayo. Kwani ndizo zinazokuletea vikwazo katika jamii
ile inayokuzunguka.
Tabia hizo zaweza kuwa za kutukana, kusengenya, ulevi kupindukia,
kupenda anasa kupita kiasi ama nyingine zinazofanana na hizo.
Mtu yeyote yampasa kujijua vema vile alivyo. Yale mtu asiyopenda kufanyiwa, naye asipende kuwafanyia wengine.
Ni vizuri kukubali kosa lako na kuomba msamaha pale unapokosea. Tabia hii inapendeza na kufurahisha.
Tabia ya kutokubali makosa na kuomba msamaha, mara nyingi huwa nayo
watendaji wenye madaraka makubwa katika ofisi mbalimbali. Kwa kuwa,
hufikiri kuwa huwa hawakosei.
Matokeo yake, ni mahusiano mabaya baina ya bosi na walio chini yake, kama vile kujengeka hali ya ujeuri ama kudharauliana.
Endapo umefanikiwa kimaisha, penda kujishusha sana. Usichukulie kigezo
cha uwezo wako, kunyenyekewa na ndugu au marafiki. Kwani itafika muda
ambao heshima itaondoka kwa watu hao. Ni vizuri kujiona kuwa wewe ni mtu
wa kawaida sana.
Aliyenacho na asiyenacho, aweze kukufikia kwa ukaribu kwa ajili ya kubadilishana mawazo nawe.
Ni vizuri kujenga tabia ya kuwasaidia watu wengine ili nao wajipende wao wenyewe na kujiona ni wa thamani katika dunia hii.
Penda kuwatia moyo wale waliovunjika moyo, hata kama huna uwezo wa
kumpa fedha ama mahitaji yake muhimu, maneno yako pekee iwe dawa katika
maisha yao. Jenga tabia ya kuwatembelea. Usipende wewe utembelewe tu
mara zote.
Toa ushauri wa kimaisha na kiuchumi. Shiriki nao katika masuala ya harusi, misiba, maongezi na matembezi.
Jifunze kuwasaidia watu kwa kujua hisia zao, si mpaka uombwe msaada.
Kwa hali hiyo, watu watakupenda, watakuthamini pale tu utakapoonyesha
moyo wa upendo kwao, si kwa sababu ya wingi wa mali ulizonazo.
Unapokuwa na moyo wa kujali, moyo wa shukrani, kutokubagua, kuwajali
walionacho na wasionacho, bila kuangalia elimu ya mtu, utakuwa ni mtu wa
watu wote katika jamii inayokuzunguka.
Ni Vizuri Kujenga Tabia Ya Kuwasaidia Watu Wengine Ili Nao Wajipende Wao Wenyewe Na Kujiona Ni Wa Thamani Katika Dunia Hii.
Penda Kuwatia Moyo Wale Waliovunjika Moyo, Hata Kama Huna Uwezo Wa Kumpa Fedha Ama Mahitaji Yake Muhimu, Maneno Yako Pekee Iwe Dawa Katika Maisha Yao. Jenga Tabia Ya Kuwatembelea. Usipende Wewe Utembelewe Tu Mara Zote.
Toa Ushauri Wa Kimaisha Na Kiuchumi. Shiriki Nao Katika Masuala Ya Harusi, Misiba, Maongezi Na Matembezi. Jifunze Kuwasaidia Watu Kwa Kujua Hisia Zao, Si Mpaka Uombwe Msaada. Kwa Hali Hiyo, Watu Watakupenda, Watakuthamini Pale Tu Utakapoonyesha Moyo Wa Upendo Kwao, Si Kwa Sababu Ya Wingi Wa Mali Ulizonazo.
Na Mwisho
Unapokuwa Na Moyo Wa Kujali, Moyo Wa Shukrani, Kutokubagua, Kuwajali Walionacho Na Wasionacho, Bila Kuangalia Elimu Ya Mtu, Utakuwa Ni Mtu Wa Watu Wote Katika Jamii Inayokuzunguka.