Dk. Peter Slaa (wa kwanza kushoto) akiwaaga wanahabari leo makao makuu ya chama hicho.
Dk. Peter Slaa akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wanahabari leo.
Dk. Peter Slaa (wa kwanza kulia) akizungumza na wanahabari leo makao makuu ya chama hicho.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Peter Slaa (wa tatu kushoto) akizungumza na wanahabari leo makao makuu ya chama hicho.
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakiwezi kukubali
viongozi wake wanaodaiwa kutishiwa maisha kuhojiwa na Jeshi la Polisi
kama imevyoelekezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi
kwani hawana imani na Polisi. Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa
CHADEMA, Dk. Peter Slaa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari
Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akitoa
tamko hilo ambalo limepitishwa na Kikao cha Kamati Kuu iliyokutana
tangu juzi, Dk. Slaa amesema hawaoni sababu ya kuhojiwa na Jeshi la
Polisi kwa kuwa wamewahi kuwapa taarifa nyingi za vitisho dhidi yao na
hakuna hata moja imefanyiwa kazi.
“Hatuwezi
kwenda Polisi kwa sababu tumekuwa tukipeleka mambo mengi ya vitisho
lakini hayafanyiwi kazi…na hili tulisha waambia hatuendi kwao labda
watukamate,” alisema Dk. Slaa akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema
yeye mwenyewe licha ya kuwasilisha madai mbalimbali aliwahi kutegeshewa
vinasa sauti na kutoa taarifa polisi lakini tangu wachukue vifaa hivyo
hawajasema chochote hadi leo, jambo ambalo limewafanya waamini hata
wakienda huko hakuna chochote kitafanyika.
Dk.
Slaa alisema leo asubuhi alipigiwa simu na mmoja wa maofisa upelelezi
kutoka Makao Makuu ya Polisi akiomba miadi ya kukutana naye, jambo
ambalo amesema hayupo tayari kuhojiwa na wanausalama hao wa raia labda
wamkamate.
Alisema
tayari baadhi ya viongozi wa Serikali wameanza kuipuuza malalamiko yao
dhidi ya vitisho wakidai huenda viongozi wa CHADEMA wanatafuta umaarufu
wa kisiasa kwa kutoa taarifa hizo, kitendo ambacho amesema umaarufu wao
hautatokana na viongozi wa Serikali au CCM bali ni kwa kazi
wanazozifanya kwa wananchi.
Juzi
Dk. Nchimbi alisema taarifa za kutishiwa maisha dhidi ya viongozi wa
CHADEMA ni nzito hivyo haziwezi kupokelewa kirahisi Jeshi la Polisi
linaanza kazi ya kuwahoji wahusika ili kulifanyia kazi jambo hilo.
Alisema suala la usalama wa raia si hiyari bali ni la lazima hivyo hata
kama wahusika hawataki lazima taratibu zifanywe kuhakikisha usalama kwa
wahusika.
Wakati
huo huo CHADEMA inaanza ziara ya Oparesheni Sangara ambayo itafanyika
katika mikoa mitano ya Tanzania ikiwemo Dodoma, Morogoro, Iringa na
Manyara. Akizungumzia ziara hiyo ambayo itashirikisha viongozi wa juu wa
CHADEMA, Wabunge, Wajumbe pamoja na viongozi wengine wa ngazi
mbalimbali. Dk. Slaa amesema ni ziara ya kukiimarisha chama ikiwa ni
pamoja na kuangalia mchakato wa uchaguzi wa chama hicho unaoendelea
ngazi za chini.
Alisema
katika ziara hiyo ambayo kauli mbiu yake ni “Hakuna Kunywa, Kula wala
Kulala” inatarajiwa kuzunguka katika majimbo ya uchaguzi 44 ya mikoa
hiyo, Kata 806 na vijiji 4,000. Ziara hiyo inatarajia kutumia siku 104.
Akifafanua
zaidi kuhusiana na ziara hiyo amesema CHADEMA ni chama ambacho
kinajitofautisha na vyama vingine katika utendaji wake na ndiyo maana
wanaendelea kufanya ziara zao vijijini kuangalia maisha ya wananchi
mpango ambao ni mpya.
“Kuna
taarifa za baadhi ya watu wanabeza ziara zetu kwamba zinalenga posho…no
CHADEMA hakuna posho, kwenye ziara zetu tunakula hadi kwa mama ntilie
(chakula cha kawaida), tutaendelea kupiga kelele hadi pale haki za
Watanzania zitakapokuwa zikipatikana bila vikwazo…tunapigania haki ya
kila mmoja awe mwanafunzi, wafanyakazi, wakulima na hata madaktari,”
alisema Dk. Slaa.
Chanzo: www.hakingowi.com
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!