Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki amesema,
Kamati ya Urithi wa Dunia imekubali ombi la Tanzania la kurekebisha
mpaka wa Pori la akiba la Selous na kuruhusu kuanza mchakato wa
uchimbaji wa Madini ya Urani.
Balozi Kagasheki alisema hayo jana
Jijini Dar es Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari kuwa, Kamati ya
Dunia ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(Unesco) katika kikao cha 36 kilichoanza Juni 24 ambacho kinafikia
kilele kesho huko Saint Persbburg nchini Urusi imeridhia ombi hilo.
“Kufuatia
kukubaliwa kwa ombi hilo la nchi yetu, nachukua fursa hii kutoa
shukrani kwa Kamati ya Urithi wa Dunia (IUCN), Kituo cha Urithi wa Dunia
na Taasisi mbalimbali ambazo walichangia katika kufanikisha ombi letu
kukubaliwa” alisema Balozi Kagasheki na kuongeza:
Uamuzi
uliotolewa na Kamati ya Urithi wa Dunia utatupatia uwezo na fursa nzuri
ya kutimiza malengo yetu kiuchumi na kijamii kwa wananchi.
Executive Director wa UN-World tourism Organization (UNWTO) Mr. Frederic Pierret (kushoto) akizungumza na waandisi wa habari, kulia ni Mkurugenzi wa utalii –Ministry of Natural Resources and Tourism Mr. Ibrahim Mussa.
Waziri
huyo alisema ombi hilo kwa mara ya kwanza lilipelekwa katika kikao cha
35 cha Kamati hiyo ya Urithi wa Dunia ya Unesco, Januari Mwaka jana na
kuhamishia mjadala huo mwaka huu.
“Uamuzi huo ulifanyika ili
kuruhusu Tathimini ya Athari ya Mazingira (EIA), kukamilishwa na kutoa
muda kwa wataalamu wa IUCN kufika eneo lililohusika ili kuliona na
kulihakiki kabla ya kuruhusu ombi letu” , alisema Balozi Kagasheki.
Balozi
Kagasheki alisema, Kampuni itakayopata nafasi ya kuchimba madini hayo,
itatakiwa kuhakikisha kiasi cha fedha kinachopatikana kinawasaidia
wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo.
“Kitu cha kwanza ni
kuwanufaisha wananchi kielimu, huduma za afya na kiasi kingine cha fedha
kitatumika katika kuhifadhi hifadhi hiyo ili iendelee kuwa katika hali
nzuri,” alisema na kuongeza:
Eneo ambalo limeruhusiwa kurekebisha
mpaka huo ni asilimia 0.8 (Kilomita 400), ya eneo la Pori ambalo lina
ukubwa wa Kilomita 50,000 ambapo ni moja kati ya Hifadhi kubwa duniani
zenye viumbe mbalimbali.
Balozi Kagasheki alisisitiza kuwa madini
hayo ni ya watanzania na kinachotakiwa hapo ni kuhakikisha wananufaika
wao kwanza kabla ya kuanza kujinufanisha kwa baadhi ya watu.
Kwa
mjibu wa Unesco, wanyama wanaopatikana katika hifadhi hiyo ni Vifaru
Weusi, Duma, Twiga, Viboko,Mamba pamoja na Mbuga na Misitu ya Miombo.
July 5, 2012
KAGASHEKI: UNESCO YARIDHIA OMBI LA TANZANIA
Millionfortune.com
SIASA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget