Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
SERIKALI imekiri kuwa wakulima wengi wamekuwa wakipatiwa mbolea ambayo
haina kiwango na ubora jambo linalopunguza ufanisi katika utendaji
kazi.
Hayo yalibainishwa jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula
na Ushirika, Adam Malima ambaye alisema kuwa Serikali inazo taarifa za
wakulima kununua mbolea isiyo na ubia na kuitumia mashambani mwao.
Malima
alikuwa kijibu swali la Jenista Mhagama (Peramiho-CCM) aliyetaka kujua
kama Serikali ina taarifa kuwa wakulima wananunua mbolea ambazo hazina
ubora kabisa.
Mhagama pia alitaka kujua ni kwa nini sheria
iliyounda TFC isibadilishwe ili chombo hiki sasa kitafute wadau wa
kuanzisha kiwanda cha mbolea na akataka kiwanda hicho kijengwe mkoani
Mtwara.
Naibu Waziri alisema Kampuni ya TFC imeendelea kuwa ni
kampuni ya umma chini ya Serikali na inafanya kazi ya kusambaza mbolea
yenye ubora na wakati.
Malima alisema kufuatia uamuzi wa kufunga
kiwanda cha uzalishaji wa mbolea kilichokuwa Tanga mwaka 1991, kitengo
cha mauzo cha Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Dar es Salaam, kiliundwa
upya na kuwa kampuni ya umma.
“Hii ilitokana na uwezo mkubwa wa
TFC katika miundombinu ya usambazaji, wataalamu wenye uzoefu na imani
kubwa iliyonayo kwa wakulima na kwa wakati, Serikali iliamua pia
kutobinafsisha mali zilizokuwa za Kiwanda cha TFC za usambazaji
mbolea,’’alisema Malima.
Kuhusu uanzishwa wa kiwanda, Naibu
Waziri alisema juhudi hizo zinaendelea na kwamba upo uwezekano mkubwa wa
kuanzishwa kiwanda cha mbolea kwa kutumia gesi asili katika siku za
usoni.
Alisema kwa mantiki hiyo na kwa ilivyo sasa ni lazima
Kampuni ya TFC ikaendelea na jukumu la kufanya kazi ya kusambaza mbolea
nchini hasa sehemu ambazo hazifikiki kirahisi ili kuhakikisha wakulima
wanapata mbolea kwa wakati.
July 5, 2012
Serikali yakiri kuwapo mbolea feki
Millionfortune.com
SIASA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget