Mpango wa Chakula Duniani WFP umetangaza kwamba kwa mujibu wa
uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa na serikali ya Zimbabwe watu
milioni 1.6 wanahitajia msaada wa chakula nchini humo mwaka huu. Felix
Bamazon Mkurugenzi wa WFP amesema, tayari maafisa wa shirika hilo
wameripoti dalili za njaa katika maeneo ya vijijini kutokana na kilimo
duni suala lililosababishwa na mvua zisizokuwa na uhakika na ukosefu wa
mbegu na mbolea. Suala hilo pia limepelekea Waziri wa Fedha Tendai Biti
atabiri kwamba ukuaji wa uchumi wa Zimbabwe utashuka toka asilimia 9.4
hadi asilimia 5.6 mwaka huu wa 2012.
Mwezi Disemba pia Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa
Mataifa ilisema kuwa watu milioni 1.45 watahitajia msaada wa chakula
nchini Zimbabwe.
July 28, 2012
Milioni 1.6 wanahitajia msaada wa chakula Zimbabwe
Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!