Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline
Liana baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza ambako alifunga
sherehe za maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa kitaifa kwenye
uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza Julai 1, 2012. Kushoto ni Mkuu wa
Mkoa huo, Mhandishi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ametoa kauli hiyo jana wakati akifunga maadhimisho ya nane ya Siku ya Serikali za Mitaa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa Katiba ya ALAT, Jumuiya hiyo inao wajibu wa kuzisimamia Halmashauri kwa iliundwa ili kudumisha na kukuza maendeleo ya shughuli za Serikali za Mitaa Tanzania kwa kuondoa vikwazo na matatizo yote.
“Serikali za Mitaa zinakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa nilizozianisha ni ukusanyaji mdogo wa mapato, usimamizi duni wa matumizi ya fedha na baadhi ya Halmashauri kushindwa kupata ruzuku ya maendeleo,” alisema.
Akizungumzia kuhusu ukusanyaji mdogo wa mapato, Waziri Mkuu alisema uko chini licha ya Halmashauri nyingi kuonesha kuwa zingekusanya mapato na kuongeza vyanzo vya mapato.
Chanzo: Mjengwa blog