Meneja
Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi
(kushoto) na Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli,
wakionesha chupa za bia hiyo zenye muonekano mpya asubuhi hii katika
mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam . PICHA NA KAMANDA
MWAIKENDA
Bia ya Ndovu Special Malt
inayotengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), leo
imezindua muonekano wake mpya ambao umeiongezea bia hiyo yenye hadhi ya
juu hapa nchini na kimataifa mvuto zaidi.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika uzinduzi huo uliofanyika Jijini Dar es
Salaam, meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema; Tunayo furaha
kubwa sana siku ya leo kuzindua muonekano mpya wa Bia hii ya Ndovu
Special Malt. Lengo kuu la maboresho haya yaliyofanyika ni kuipa Bia hii
ya Ndovu muonekano wenye mvuto zaidi, lakini pia kuvipa muonekano
zaidi vitu muhimu vinavyoitambulisha bia hii.
Ukiangalia
katika lebo ya mbele, picha ya mnyama Tembo, au kwa jina jingine Ndovu
imeongezwa ukubwa, hii ni kwa sababu maalum za kumpa uzito unaostahili
mnyama huyu ambae ndio kitambulisho namba moja cha bia hii. Maboresho
mengine yaliyofanywa ni pamoja na kuboresha nembo ya kiungo muhimu
kinachoitofautisha bia ya Ndovu na bia nyingine “Cristal Malt”, pia lebo
inayozunguka shingo ya bia hii (foil) ambayo sasa ina mg’ao angavu wa
dhahabu. Wapenzi wa Bia hii ya Ndovu special Malt watapata pia historia
ya bia hii katika lebo ya nyuma hivyo kuwawezesha kuielewa bia yao
vizuri zaidi. Tunatarajia maboresho haya yatawavutia zaidi wadau wa
Ndovu Special Malt na hivyo kuongeza mafanikio ya bia hii. Alisema
Pamela.
Kwa
upande wake Meneja Uhusiano na Habari wa TBL Bi. Edith Mushi alisema;
Bia hii ya Ndovu Special Malt, imeendelea na itaendelea kuongoza katika
ubora wa Bia za Kitanzania katika soko la ndani na nje pia. Hii
inatokana na umakini unaotumika katika kutengeneza bia hii, ikiwemo
kiungo cha “Cristal Malt” kinachoitofautisha na kuifanya bia hii iwe
juu ya bia zote hapa nchini. Yote haya yanathibitishwa na ushindi
mkubwa na wa kishindo ambao Bia hii imekuwa ikijitwalia katika tuzo za
kimataifa kutokana na ubora wake. Mwaka huu kwa mara nyingine tena Bia
hii ya Ndovu Special Malt imeshinda tuzo yenye hadhi ya juu kabisa ya
bidhaa za kimataifa kwa mara ya pili. Tuzo hizi hutolewa na Taasisi ya
kimataifa inayoangalia ubora wa bidhaa ya “Monde Selection
International Quality Institute” iliyopo Athens, Ugiriki. Tuzo hii
inajulikana kama “Grand Gold Quality Award” na hushindanisha
bidhaa toka Mataifa mbalimbali. Hivyo hii inawathibitishia wadau wote
wa bia hii kuwa wanafanya uchaguzi na maamuzi sahihi kwa kuchagua
kutumia Ndovu Special Malt, kwani ubora wake unajidhihirisha kimataifa.