Rais Dkt Shein
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein leo amemuwaapisha Mhe.Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa
Miundombinu na Mawasiliano kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa
Wizara hiyo Mhe. Hamad Masoud Hamad.
Wakati huo huo, Dk. Shein amemuapisha Sheikh Daud Khamis Salim kuwa
Kadhi wa Rufaa Pemba. Sheikh Daud aliteuliwa Mei 26 mwaka huu.
Hafla hiyo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi
mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Idd,
Spika wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa
Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.
Othman Masoud.
Wengine ni Mufti Mkuu
wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Khamis Haji, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi
Khamis, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Mstahiki Khatib
Abdulrahman Khatib, Washauri wa Rais, Naibu Waziri wa Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano Mhe. Issa Haji, Naibu Mufti Sheikh Mahmoud
Wadi, Naibu Kadhi Sheikh Hassan Othman Ngwali pamoja na viongozi
wengine.
Dk. Shein jana tarehe 23
Julai 2012, alikubali ombi la Mhe. Hamad Masoud Hamad la kutaka
kujiuzulu ili awajibike kisiasa kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya
MV Skagit iliotokea tarehe 18 Julai, 2012 ambayo ilisababisha vifo na
majeruhi kadhaa.
Kutokana
nakujiuzulu huko kwa Mhe. Hamad, Dk. Shein alimteua Mhe. Rashid Seif
Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano katika Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!