UONGOZI wa Simba umeandaa kiasi cha euro 500,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 900, kwa ajili ya usajili unaoendelea kushika kasi.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alisema hawana wasiwasi wala papara ya usajili kwa kuwa tayari wana kiasi hicho cha fedha mfukoni, hivyo wanaweza kumpata mchezaji yeyote wanayemhitaji.
Tayari Simba imefanikiwa kuwasajili wachezaji kadhaa wakiwemo Patrick Nkanu Mbiyavanga, Lino Musombo kutoka DR Congo, Mussa Mude (Uganda), Salum Kinje (Mtanzania aliyekuwa akikipiga na AFC Leopard ya Kenya), Abdallah Juma na Paul Ngalema (Ruvu Shooting).
“Hatuna shaka na usajili, kwani umesogezwa hadi mwezi wa nane ligi itakapoanza, tuna euro 500,000 kwa ajili ya usajili, hivyo hatuna wasiwasi wowote.
“Usajili wa sasa ni mzuri kwani tuna kipindi kirefu cha kusajili wachezaji, pindi atakapoonekana yule anayefaa kwa wakati husika,” alisema Kaburu.
Alisema wanahitaji kusajili kikosi kilicho imara zaidi kitakachokuwa na ushindani wa hali ya juu ili kuhakikisha wanapata ubingwa katika michuano mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!