“Mv
Skagit ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 pamoja na mizigo tani
26, hivyo kulingana na idadi ya abiria 288 walioondoka katika chombo
hicho isingeweza kuleta madhara kama hayo, ila tunawasiwasi waliongeza
abiria njiani au mawasiliano ya hali ya hewa” Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano David Mziray.
Kauli
hii inaufanya umma wa watu ambao sasa ni waelewa kwa asilimia kubwa
kuamini kuwa baadhi ya taasisi za serikali watendaji wake wanafanyakazi
pasipo kujua wanafanya kazi gani.
Haiwezekani
leo hii useme kuwa Boti ile inawezekana iliongeza abiria njiani...sasa
wapi kuna gati huko baharini na hao abiria wanatokea wapi? ilhali safari
ya boti kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar (Unguja) hakuna kituo hapo
njiani.
Lakini
labda SUMATRA wana gati mpya Bagamoyo au Mbezi Beach huko. Ila hakika
huu ni mtokoto wa mwaka 2012 na ni dharau kwa roho za watu na mali zao
kwa mamlaka yenye dhamana ya kusimamiusafiri nchini.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!