Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
MAMLAKA ya Elimu ya Ufundi Stadi (Veta), imevipa miezi sita vyuo 200
vilivyokuwa chini yake, ili kujitathmini na kufuata mwongozo wa mamlaka
hiyo vinginevyo hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.
Mkufunzi na
Mtathmini wa Veta, Joyce Mwinuka alibainisha hayo katika mahojiano na
mwandishi wa habari hizi akibainisha kuwa mwaka huu mamlaka hiyo
itakamilisha zoezi la kukagua vyuo vilivyo chini yake lilioanza mwaka
2009.
“Muda huo utaanza kuhesabiwa Novemba mwaka huu, mwanzo
tulikuwa na vyuo 900, lakini vilivyobaki sasa havifiki 700, vingine siyo
kama tumevifuta, bali tumevipa mwongozo wa kufuata,” alisema Mwinuka.
Alisema kuwa, tofauti na miaka iliyopita watu walikuwa wakifungua vyuo
na baadaye kwenda Veta kuvisajili vyeta, lakini sasa watatakiwa kupata
mwongozi wa mamlaka hiyo kabla ya kufungua vyuo hivyo.
“Hii ni
kwa sababu kuna taratibu zinatakiwa kufuatwa, kwa mfano ni wapi karakana
itakapokuwa, iwe na vigezo gani na vitu vingine kama hivyo,” alisema
Mwinuka. Naye Meneja Uhusiano wa Veta Grace Kabogo, alisema chuo hicho
kinahakikisha kuwa utoaji mafunzo yake ya ufundi stadi unasaidia vijana
kujiajiri. Alisema kuwa katika kuthibitisha hilo, mwaka huu mamlaka
hiyo imepata tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa kutoa mafunzo ya ufundi
pamoja na washindi wa pili.
Tuzo hizo zilizotolewa na Waziri
Mkuu Mizengo Pinda katika Maonyesho ya Sabasaba yanayofanyika katika
Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam. Pamoja
na mambo mengine, katika maonyesho hayo Veta imeweka kitanda tiba,
ambacho ni mahususi kwa watu wenye matatizo ya maumivu ya mgongo.
Akielezea
juu ya kitanda hicho Salumu Machapati ambaye ni mmoja wa wanafunzi
waliokitengeneza, alisema katika kitanda hicho mbali na mbao kuna
matofali maalumu yaliyotengezwa na udogo pamoja na mkaa.
July 5, 2012
VYUO 200 VYA VETA HATARI KUFUTWA
Millionfortune.com
SIASA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget