Keita aondoka Barcelona Ahamia klabu ya Dalian Aerbin ya China
Uruguay yaaga olympic
Nyota na mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez amewashutumu mashabikii wa
Uingereza kwa kuizomea timu yake wakati wimbo wa Taifa lake
ukitumbuizwa.Uruguay ilishindwa dhidi ya Uingereza katika mechi kwenye uwanja wa Millennium kwa 1-. Katika michuano mingine Misri ilijiunga na Brazil katika robo fainali na itachuana na Japan iliyoichapa Belarus 3-1
Inter yapata wamiliki wa bara Asia
Klabu ya Uitaliano Inter Milan inasema kua kundi la wawekezaji kutoka
Uchina limejitokeza kua wawekezaji wa pili kwa ukubwa wa kumiliki hisa
za klabu hiyo. Wameahidi kujenga uwanja mpya.Klabu hio imetangaza kua Kamchi Li, Kenneth Huang na Fabrizio Rindi wote
watakua wakurugenzi kwenye bodi kutokana na uwekezaji huu.
Arsenal kusajili wawili kwa mpigo
Sahin na Cazorla watazamiwa wiki hii. Arsenal inajitahidi kukamilisha utiaji saini wa makubaliano ya mkataba wa kudumu na mchezaji Santi Cazorla kutoka klabu ya Malaga pamoja na mcheza kiungo mwenzake Nuri Sahin anayeingia kwa makubalino ya mkopo kutoka klabu ya Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!