StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

August 4, 2012

Ligi Kuu bado haijapata mdhamini

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
WAKATI Ligi Kuu ya Tanzania (TPL) imepangwa kuanza Septemba Mosi ikiwa chini ya Kampuni, mpaka sasa bado hajapatikana mdhamini wa Ligi hiyo ya msimu wa 2012/2013.

Hata hivyo tayari mazungumzo yanaendelea na kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom pamoja na kituo cha televisheni cha Super Sports cha Afrika Kusini.

Mmoja wa viongozi waliofanikisha mchakato wa Ligi kuendeshwa kwa kampuni aliiambia Mwananchi kuwa juzi viongozi wa klabu zote 14 za Ligi Kuu walikuwa na kikao kwenye hoteli ya JB Belmonte na kupeana taarifa mbali mbali kuhusiana na mchakato unavyoendelea.

"Mkataba wa Vodacom na TFF ulikuwa ni mkataba wa siri, hata hivyo umemalizika, tumekaa nao kuangalia jinsi ya kuongeza fedha katika mkataba wao na kama tutakubaliana nao basi wataingia mkataba na Kampuni na sio TFF,"alisema kiongozi huyo.

Alisema kuhusu Super Sports ambao awali walisema hawawezi kudhamini ligi ya Tanzania mpaka iondoke mikononi mwa TFF na iendeshwe na chombo huru alisema,"Super Sports pia mazungumzo yanaendelea na tunatarajia itaingia udhamini na kampuni ikishaanza kufanya kazi yake na itaonyesha ligi yetu kama wanavyofanya Kenya."

Tayari Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyokutana siku mbili Jumamosi na Jumapili imeridhia Ligi kuendeshwa na chombo huru na kikao cha juzi pia kilijadili marekebisho madogo madogo ya kisheria ambayo Kamati hiyo ya Utendaji iliomba yafanyike katika muundo huo wa kampuni.

Baadhi ya vipengele ambavyo vipo kwenye muundo huo wa TPL ni kuwa itafahamika kama Ligi Kuu na iwapo atajitokeza mdhamini atanunua jina hilo kwa kipindi fulani na kuweka la kwake ikiwamo kubadili logo ya ligi na atalazimika kutumia logo ya Ligi Kuu kama logo yake mpya na atalazimika kuruhusu angalau kwa asilimia chache jina la Ligi Kuu kuendelea kutumika kwenye ligi.

Pia muundo huo unaonyesha Kampuni ya TPL itaruhusu ligi kudhaminiwa na wadhamini zaidi ya mmoja ambao wanafanya biashara zisizoshindana sokoni na mdhamni yeyote wa Ligi Kuu atazuiwa kuweka logo ya kampuni yake kifuani, ila endapo atatoa fedha kubwa ambayo bodi ya wakurugenzi wa TPL wataridhika kuvaa nembo yake, basi nembo hiyo itawekwa begani na siyo kifuani.

"Kutakuwa na wadhamini wadogo wadogo ambao watauziwa haki ya kutumia logo ya Ligi Kuu kwenye promosheni zao na TPL itawajibika kusaka mdau wa matangazo ya televisheni ili kuweza kupata fedha ya udhamini, nia ni kuboresha mazingira ya udhamini wa Ligi Kuu na udhamini wa klabu,"alisema kiongozi huyo kwa sharti la kutotajwa jina kwa vile si msemaji wa suala hilo.

Alisema kwa kushirikiana na viongozi wa klabu, meneja masoko wa TPL atakuwa na wajibu wa kusaidia klabu kupata udhamini pia afisa mipango na uendeshaji wa Ligi atafanya kazi chini ya mratibu wa mashindano na atashughulika na klabu kuhakikisha viwanja vina viwango, mechi zinaanza kwa wakati, taratibu zote kabla ya kuanza kwa mechi zinafuatwa na haki za wadhamini wa Ligi Kuu zinalindwa.

Pia mratibu wa mashindano amependekezwa atoke nje ya nchi na atashughulika na mambo yote ya kiufundi kuanzia Usajili, Upangaji wa ratiba, utengenezaji wa kanuni za ligi, mafunzo kwa makocha, waamuzi, mameneja, mweka hazina pia atatoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TPL.

Muundo huo pia umependekeza meneja mawasiliano TPL atafanya kazi kama ofisa habari na meneja mawasiliano wa TPL, pia atatunza rekodi na taarifa zote zitakazohitajika kwa wana habari na pia ataendesha tovuti ya TPL kwa kushirikiana na kampuni itakayoteuliwa kuendesha tovuti ya TPL sambamba na uandaaji wa vipindi vya TV vya TPL kwa kushirikiana na kituo cha televisheni kitakachokuwa na haki za matangazo ya TV.
SOURCE: MWANASPOTI

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat