Ikiwa imeingia katika siku ya pili ya usaili wa Epiq BSS Dar-es-Salaam ambao unafanyika Coco Beach
jijini hapa vijana wengi wamezidi kujitokeza kutoka maemneo mbalimbali
ya jiji kusaka nafasi ya kushiki katika shindano hilo kubwa hapa nchini
la kuibua vipaji vya wasanii wa muziki. Hadi jana usiku majira ya saa
moja zaidi ya vijana mia tatu bado walikuwa katika foleni ya kutaka
kuonana na majaji kwaajili ya usaili.
Jaji
Mkuu wa Shindano la EBSS Ritta Poulsen ‘Madam Ritta’ akitafakari jambo
wakati akimsikiliza mmoja wa washiriki waliojitokeza katika usaili.
Mmoja wa washiriki wa EBSS katika mchujo wa Dar es Salaam akichangia damu
Maofisa
kutoka kitengo cha Damu Salama wakiendelea na shughuli ya kutoa maelezo
na kupima damu kwa vijana waliojitokeza katika zoezi la uchangiaji damu kwa washiriki wa EBSS jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki
Banana Zorro nae alikuwepo Coco Beach katika usaili wa EBSS yeye hakuwa
mshiriki bali alifika kutoa sapoti kwa jopo la majaji na vijana
wanaoshiriki.
Hakuna
kazi rahisi hata siku moja, na hapa jamaa wakiuchapa usingizi baada ya
kusubiri sana zamu yao ifike na kuweka sawa mistari yao.
Foleni
ya washiriki waliokuwa wakisubiri kuonana na majaji katika usaili wa
EBSS katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Coco Beach Dar es Salaam.
Hizi ni swaga za kuondokea , jamaa akitoka ndani baada ya kuonana na majaji
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!