Na. Zitto Kabwe.
Hiii
ni sehemu ya 2.5 katika hotuba ya Waziri Kivuli na Msemaji Mkuu wa
Kambi Rasmi ya Upinzani Wizara ya Fedha na Uchumi Mh Kabwe Zuberi Zitto
kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha
2012/2013.
2.5 MKOPO WA KUNUNUA RADA ILIYOGUBIKWA NA UFISADI
Mheshimiwa
Spika, sehemu ya Malipo ya Deni la Taifa ni Mkopo ambao Serikali
ilichukua ili kununua Rada kutoka kampuni ya BAE ya Uingereza.
Suala
hili la rada limejadiliwa sana nchini kwa upande mmoja tu wa ufisadi wa
kupandisha bei ya Rada na hatimaye kurejeshwa kwa iliyoitwa chenji ya
Rada.
Hiyo
ilikuwa ni nusu tu ya ukweli kuhusu suala la Rada kwani Serikali
ilikopa kiasi cha dola za kimarekani 40 milioni kutoka Benki ya Barclays
ya Uingereza kwa ajili ya kununulia Rada.
Mkopo huo ulikuwa na Riba ya asilimia 4.9 juu ya kiwango cha riba zinazotolewa na Benki ya Dunia au IMF.
Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kujua kama mkopo huu umeshalipwa wote na jumla tulilipa kiasi gani cha fedha.
Ukilinganisha
fedha iliyorejeshwa kama chenji ya Rada na Fedha ambayo Tanzania
iliilipa Benki ya Barclays (Principal amount and Interest), je chenji ya
Rada ilikuwa na thamani yoyote kifedha?
Mjadala wa ununuzi wa Rada hauwezi kuisha kwa kufurahia kurejeshewa chenji tu.
Mjadala
huu bado mbichi kabisa kwani tunataka ukweli na ukweli mtupu uelezwe
kwa umma na kuona Taifa lilipata hasara kiasi gani kwa ufisadi huu wa
kimataifa na hatua stahiki za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wote
walioingiza hasara kwa Taifa letu.
SOURCE: Zitto Kabwe Blog
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!