Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Koffi Anan, anatarajiwa kuwa mwenyekiti katika mkutano wa kimataifa wa Jukwaa la Mapinduzi ya Kijamii (AGRA) ambao utafanyika mkoani Arusha kwa ajili ya kuboresha usalama wa chakula.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa viongozi kutoka nchi 21, wakiwemo marais na mawaziri wa kilimo watashiriki.
Alisema AGRA imeandaa mkutano kwa viongozi wa Afrika kwa ajili ya kuendesha mpango wa kukuza uwekezaji na sera ya kuongeza uzalishaji wa kilimo na ukuaji wa kipato kwa wakulima wa Afrika.
Chiza alisema viongozi hao watapata fursa ya kujadili sera ya mapinduzi ya kilimo na uchumi wa Afrika, njia za kukuza masoko pamoja na kubadilisha mfumo mzima wa kilimo.
August 24, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!