Makamu
wa Pili wa Rais Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd leo amezindua ujenzi wa
Skuli ya msingi iliyopewa jina la Urafiki inayofadhiliwa na Serikali ya
Jamhuri ya Watu wa China.
Balozi Seif Idd aliyasema hayo katika
skuli ya Mwanakwerekwe C wakati akizindua ujenzi wa skuli ya urafiki
inayofafdhiliwa na Serikali ya China kwa Dola za Marekani 1.6.
katika
sherehe za uzinduzi wa Skuli hiyo yenye madarasa kumi na mbili,Makamu
wa Rais amesema kwamba wananchi wa Zanzibar wanathamini mchango
unaotolewa na Serikali ya China.
Pia
alisema Serikali inaupa kipaumbele sana mchango huo kwa kuchangia
katika sekta ya Elimu kwani bila ya elimu hakuna maendeleo.
Aidha,
Balozi Seif Idd amesema kwamba Serikali itachukua kila jitihada
kuhakikisha tatizo la vikalio linamalizika katika skuli zote za Unguju
na Pemba alisema.
Utoaji wa madeksi hayo
Mbali
na ujenzi wa Skuli hiyo, pia Serikali ya China kupitia Jimbo la Sichuan
imetoa jumla ya madawati 480 kwa ajili ya Skuli mbalimbali za Unguja.
Kwa
upande wake, Balozi mdogo wa China Zanzibar, Chen Qiman alisema
Serikali ya China itaendelea kuisaidia Zanzibar katika nyanja
mbalimbali.
Ameipongeza
Serikali kwa juhudi inazochukuwa kutekeleza mipango yake mbalimbali ya
kuwalatea maendeleo wananchi wa Zanzibar akitoa mfano suala zima la
elimu.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali,Ali Juma Shamuhuna ameipongeza Serikali ya
China kwa msaada wao kwa Wizara ya elimu hasa ujenzi wa Skuli hiyo
pamoja na msaada wa madawati.
source: fullshangwe blog
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!