StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

August 23, 2012

MH, YAJUE HAYA KUHUSU USAFIRI WA PANTONI NA KERO YA WAKAZI WA KIGAMBONI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends




Boti ya TPA Ikizuia Pantone ili meli iweze kupita huku Panton imepatia abiria



Meli inapita huku abiria wa Pantoni wamesubiri karibu saa nzima

Kwa takribani miezi 9 sasa tangu nimeungana na wenzangu waishio Kigamboni nimejikuta katika wakati mgumu hususan, wakati natumia Kivuko jambo lililonipa msukumo wa kukaa chini na kuandika mada hii. Kwa mtazamo wangu, nadhani hakuna mawasiliano kati ya Afisa wa Mamlaka ya Bandari (TPA) anayeongoza Meli zinazoingia na kutoka Bandarini na Afisa wa TEMESA (Mamlaka yenye dhamana na Vivuko) anayehusika kuruhusu vivuko.

Inawezekana nisiwe sahihi, lakini nataka kutahadharisha kuwa haya ni mawazo yangu binafsi. Katika kipindi chote ambacho nimeanza kujihusisha na shughuli za kuhamia Kigamboni nimekutana na kero ambazo nilidhani katika hali ya kawaida kuna Afisa anapaswa kusimamia pale Kivukoni. Cha kushangaza ni kuwa sioni na sidhani kama wenzetu wameona hili. Pamoja na hilo naomba kueleza mambo yafuatayo:-

1. MUDA WA KUINGIZA NA KUTOA MELI BANDARINI:
Ndugu zangu ni jambo la kushangaza mno kukuta eti wakati wananchi ama wanawahi kazini asubuhi au wanarudi majumbani jioni baada ya pirika za ujenzi wa Taifa ndipo Afisa Muoongoza Meli anapojaribu kuruhusu Meli kubwa kutumia njia. AJABU KWELI! Kwa wale wasiojua, Meli hizi ni kudwa mno na hulazimika kupita taratibu sana kuepusha misukosuko au tafrani kwenye Vivuko kwani vinaweza kuanguka. Wachache wenu ambao wamewahi kukutana na dhoruba za namna hii wakati Boat za kwenda Zanzibar zinapopita watakuwa ni mashahidi wazuri. 

Pata picha ya Idadi ya watu waliozuiliwa na meli: Wakitoka kwenye Pantoni

KERO ZINGINE KATIKA VIVUKO HIVI NI:-

1. MATUMIZI YA VYOO:
TEMESA wamekuwa busy na kukusanya pesa lakini cha ajabu utaratibu wa vyoo ni mbovu kupindukia. Fikiria wale wanaotumia magari madogo kwa mfano; Kila siku wanalipia Tsh. 3,000/= lakini mtu huyo akihitaji kujisaidia lazima akalipe Tsh. 200/= tena inakuwa kama ni adhabu hadi kupata mahali ambapo kuna vyoo ambavyo vinanuka kwa kukithiri na uchafu. HAIINGI AKILINI HATA KIDOGO.

2. PARKING YA MABASI/DALADALA:
Utaratibu ni mbovi, abiria na magari yanatuamia njia moja halafu mlangoni mnakuta daladala zinasubiri abiria, sasa subiri uone kasheshe yake!
USHAURI KWA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA:

1. Mamlaka zinazohusika kuandaa utaratibu ambao utazuia Meli kubwa kupita wakati watu wanawahi au wanatoka vibaruani kwa wingi. Meli hizi hutumia zaidi ya saa 1 kupita hali ambayo husababisha usumbufu mkuwa kwa wananchi.

2. Uandaliwe utaratibu wa kusafisha vyoo, kujenga vyoo ambavyo ni rafiki kwa abiria wa miguu na wanaotumia magari binafsi. Aidha, uwezekano wa wanaolipa gharama za magari kutumia vyoo bure uangaliwe upya. Hawa watu wanalipa pesa nyingi wakati huduma ni duni.

3. Vile vile mamlaka husika isimamie na kutenganisha abiria na magari kutumia lango moja la kutokea kuepuka na usumbufu na hatari zinazoweza kujitokeza. Hali huwa mbaya sana wakati wa kutoka haswa upande huu wa Dar es Salaam.

TUNAOMBA MAMLAKA HUSIKA ZISHUGHULIKIE HAYO, WANANCHI TUNAKERWA SANA!

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat