StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 14, 2012

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI YAFANYA MKUTANO WA UANZISHWAJI WA ENEO HURU LA MAGONJWA YA MIFUGO KATIKA MKOA WA RUKWA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Picha ya pamoja kati ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang'a na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Winston Mleche pamoja na wataalamu wa Mifugo kutoka Mikoa ya Rukwa, Njombe, Katavi, Tabora, Mbeya, Singida, Shinyanga, Mwanza, Kigoma, Iringa, Kagera, Mara, Simiyu na Geita katika kikao kilichowashirikisha wataalamu hao katika kujadili mpango wa kuanzishwa eneo huru la magonjwa ya mifugo katika Wilaya za Sumbawanga na Nkasi Mkoani Rukwa kwa lengo la kuwezesha kufanyika kwa biashara ya mifugo na mazao ya mifugo kwa kufuata vigezo na masharti ya kimataifa.


Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambae pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla akiwakaribisha wageni hao Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufanya mkutano huo muhimu kwa maendeleo ya sekta ya mifugo mkoani Rukwa na Taifani kwa ujumla.


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Moshi Chang'a ambae pia ni Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kalambo akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya ambaye yupo safarini kikazi. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Winston Mleche ambae pia ni Mkurugenzi wa huduma za mifugo nchini. Katika hotuba yake hiyo alielezea changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi ikiwemo uimarishaji wa mifumo ya usafirishaji, uchukuzi na mawasiliano, kuboresha miundombinu ya masoko ya mifugo, kuendelea kuboresha aina ya mifugo na mifumo ya uzalishaji mifugo, kuboresha taratibu za umiliki wa ardhi na kuzuia magonjwa mbalimbali ya mifugo. Hata hivo Mkoa wa Rukwa umepiga hatua kubwa katika kupambana na magonjwa hatarishi ya mifugo ambayo kwa sasa yapo kwa kiwango kidogo sana.


Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa kitengo cha Uchumi na Uzalishaji Ndugu Respitch Maengo na Katibu Tawala Msaidizi kitengo hicho kutoka Mkoa jirani wa Katavi Ndugu Sesemkwa.


Daktari wa Mifugo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Loomu akiwasilisha mada ya fursa za mifugo zinazopatikana Mkoani Rukwa. Zipo fursa nyingi Mkoani Rukwa ikiwemo mifugo mingi na ya aina tofauti yenye afya pamoja na wafugaji mahiri wadogo na wakubwa. ,Maeneo ya malisho, uwepo wa kiwanda cha kisasa cha nyama cha Saafi kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndaji ni fursa nyingine.


Baadhi ya wadau wa Mkutano huo wakifuatilia mada tofauti ndani ya Ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kikao hicho kitadumu kwa muda wa siku mbili ambapo maazimio mbalimbali yantegemewa kufikiwa kwa ajili ya kufanikisha adhma hiyo ya kuufanya Mkoa wa Rukwa eneo huru la magonjwa ya mifugo kuimarisha bishara ya mazao ya mifugo kimataifa. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat