Mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, leo itaanza kusikiliza utetezi wa kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. Bilioni 11.7, inayomkabili mawaziri wa zamani, Basil Mramba, Daniel Yona na Katibu mkuu wa Hazina, Gray Mgonja baada ya kukutwa wana kesi ya kujibu.
Utetezi huo utasikilizwa mbele ya jopo la mahakimu watatu wakiongozwa na Jaji John Utamwa na Sam Rumanyika wa Mahakama Kuu waliopewa kibali na Jaji Mkuu kuendelea kusikiliza kesi hiyo wakisaidiana na Saul Kinemela.
Upande wa Mashtaka unaongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Osward Tibabyekomya akisaidiana na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kupambana na Kuzia Rushwa (Takukuru), Ben Linkolin.
Upande wa utetezi unawakilishwa na mawakili, Herbat Nyange, Cathbert Tenga na Elisa Msuya.
Mapema mahakama hapo bila kuacha shaka iliwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.
Awali mahakamani hiyo, upande wa mashtaka ulifunga ushahidi wake baada ya kuita mashahidi 13 na kuwasilisha vielelezo 26 mahakamani.
Katika kesi ya msingi, washitakiwa wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka.
Ilidaiwa kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart (ASSAYERS) Government Business Corporation waliingia mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!